Ajabu wanawake wengi nilioongea nao wala hawajui. Hawana habari Kombe la Dunia la Kandanda limekuwa likichachatika na kuchacharuka kule China kwa majuma kadhaa:
”Ah, Mpira sipendi…”
“Ni wanawake wenzio wanacheza.”
“Ah, mpira unaniboa.”
“Lakini wanacheza bab kubwa.”
“Ah mpira mambo ya wanaume.”
“Ni wanawake wenzio wanacheza.”
“Aka…”
Archive for September, 2007
Baada ya Ujerumani kuchukua tena Kombe la Kina Dada, Beijing…
Posted in Uncategorized on September 30, 2007 | Leave a Comment »
Moja ya sehemu iliyogeuka kuwa Maarufu London
Posted in Uncategorized on September 17, 2007 | 1 Comment »
Miaka miwili iliyopita kijana mwenye miaka 27 toka Brazili, Jean Charles de Menezes, alipigwa risasi saba mfululizo na askari wa kuzuia ugaidi mjini London na kufa katika kituo cha treni cha Stockwell. Menezes alikuwa, tukitafsiri Kiingereza kuwa Kiswahili, ”mahali pabaya; wakati mbaya” au Kiswahili: na siku ya kisirani. Kosa lake? Aliishi nyumba aliyopanga pia mmoja wa magaidi toka Afrika Mashariki waliojaribu [...]
Washiriki katika Pati ya Afrika Mashariki London
Posted in Uncategorized on September 17, 2007 | Leave a Comment »
Mbongo, ambaye alipiga baadhi ya picha za pati, mcheshi, mchapa kazi na mkazi wa London, Kiondo Kiondo, akipozi na washikaji toka Bongo na Kenya, kuendeleza ujirani mwema. Bonyeza picha ujionee wajihi mkubwa zaidi.
Washiriki katika Pati ya Afrika Mashariki London
Posted in Uncategorized on September 15, 2007 | 2 Comments »
Baadhi ya washiriki katika sherehe ya “networking” ya Afrika Mashariki iliyofanyika klabu kubwa ya The Cross Keys, wakiwahi wahi milo ya nyumbani : sambusa, chapati, pilau, ndizi za kuoka, kachumbari na kadhalika. Picha hii ilipigwa na Mtanzania, Kiondo Kiondo, aliyedumbukia humu kwa moyo wote. Ambaye hakuhudhuria na sahani yake pia haikuwepo…
Washiriki katika Pati ya Afrika Mashariki London
Posted in Uncategorized on September 15, 2007 | Leave a Comment »
Pati la Waafrika Mashariki mjini London halikukosa pia wapenzi kutoka Uzunguni ambao kama mnavyoona katika sura zao walifurahia makutano. Picha tumeletewa na Mbongo aliyeshiriki kwa bidii na moyo, Kiondo Kiondo toka Kilimanjaro.
Picha zaidi za Walioshiriki “network” ya Waafrika Mashariki London
Posted in Uncategorized on September 15, 2007 | Leave a Comment »
Wacheza dansa la shoo mseto wa ngoma na vituko vya Kinyarwanda, Sheena, Nadia na Kelly. Walinidokezea kwamba bado wako masomoni jijini London; na huenda miezi ijayo wakawa jukwaani na bendi ya Kitoto. Wee hata kama sio mwizi utaacha kuwaiba? Si ndiyo ujirani mwema huu? Afrika Mashariki Oyeee…
Waafrika Mashariki Wakutana “ku-network” London
Posted in Uncategorized on September 12, 2007 | Leave a Comment »
Wikiendi iliyopita, Jumapili, Septemba 9, wanajamii wa Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda na Bongo walikutana kula, kunywa, kucheza na kuongea. Mkutano huu usiozeleka sana kwa Wabongo hujulikana kama “networking.”
Baadhi ya Watayarishaji na Wageni rasmi wa shughuli
Posted in Uncategorized, tagged Business, Development, East Africa, Maendeleo, Networking, People, Ushirika on September 12, 2007 | Leave a Comment »
Kushoto aliyekatwa kiduchu (sore bradha), mwanasiasa mpigania haki, Julius Mutyambizi-Dena (Zimbabwe), Dada Luna Keza( Burundi), King Omogo (Kenya) huyu alikuwa na kofia mbili. Ya kuwakilisha ugeni rasmi wa kiuongozi na kutongoa mashairi makali kwa Kiluo na Kiingereza. Mwanzo kulia ni John Bunyeshuli aliyekuwa MC na mtayarishaji mkuu wa sherehe. Ingawa John ni mzawa wa Rwanda husema yeye ni Mwana-Afrika Mashariki. Ndiyo [...]
Baadhi ya Wana- Kitoto Band waliotumbuiza…
Posted in Uncategorized on September 12, 2007 | Leave a Comment »
Wanamuziki wakongwe wenzangu wa “Kitoto Band” waliokuja nami kupiga bila kudai hata senti tano, wakiwakilisha wenzetu wengine. Tena wala si wazawa wa nchi zilizoshiriki. Unaona moyo huo? Mpiga besi moto moto, Andre Mathurin (toka visiwa vya St. Lucia) na mpiga ngoma Gwang (tamka Gwanji) toka Grenada huko huko visiwa vya Karibi. Niko nao hawa jamaa miaka saba sasa….wanaipenda Afrika, [...]
Watayarishaji wa shughuli ya Afrika Mashariki
Posted in Uncategorized on September 12, 2007 | Leave a Comment »
Mtanzania pekee aliyehusika katika utayarishaji wa shughuli hii bab kubwa…Salim Mhando (mzawa wa Tanga) akiwa na Annet Alinda toka Uganda. Mhando alisema aliheshimu namna wenzetu walivyoshirikiana na kujitolea ili tu kukutana na kubadilishana mawazo yaani networking. Salim kaapa, ingawa wazalendo wa Bongo walimichia shughul hii, hautakuwa mwisho. Ushirikiano na umoja tu ndiyo njia pekee ya kuleta maendeleo Afrika.