Zamani nikidhani sisi wamatumbi ndiyo mabingwa wa kukatika viuno. Lakini miaka inavyokwenda ndivyo nazidi kuona baadhi ya tabia na desturi nyingi zetu zikidakwa, zikiigwa na wenzetu wa mataifa mengine. Kumbe pia si tu kuigana, tamaduni nyingine pia zina mikatiko. Kifupi, kuna viuno aina nyingi.
Ipo chakacha, ambayo asilia ni ngoma ya mama mzazi kurekebisha tumbo la uzazi, kutoa unene, halafu kuna viuno vya makalioni. Hivi vimetangazwa sana na Wajamaika siku za karibuni hasa baada ya mtindo wa Ragga (uliochepua mwaka 1990 na Shabba Ranks) ambapo wasichana wanaonyesha matako kwa ustadi sana, mara nyingine hata kuzidi ustadi, kuwa utani. Umesambaa sana : unaitwa “booty”….
Kuna kiuno cha Kisindimba ambapo kiuno kinagongwa huku na kule kama mshale. Ngoma ya Sindimba imeigwa sana na hapa Uingereza kilikuwepo kikundi cha ngoma : Adzido. Hawa walikuja kuuisomea Bongo. Kuna kiuno cha Samba ambacho kule Brazili bibie anakatika halafu anakwenda chini kisha anapanda tena. Mtindo huu ni wa mashindano-masihara; na huapa wale wasiokuwa na miguu mizuri shida ya kwenda na kupanda tena.
Kuna kiuno ninachokiita cha kitandani ambacho bibie anakatika; anageuka anainama chini anafanya kama anakuna , kama anapekua shuka. Kiuno njoo, kiuno chukua, chuma mboga.
Viuno vingi. Hata havina hesabu. Kipo cha wasenge, niliwaona siku moja usiku hapa London (mji wa ufirauni) wamelewa. Mmoja kambeba mwenzake mgongoni, hao, wanafanyiana masihara. Kila wakisimama wanapokezana, aliyebebwa anabeba tena. Kila akibebwa anamchapa mwenzake kofi makalioni, kisha wanacheka. Aliyechapa kofi anatikisha makalio. Haya mambo yanavuruga akili lakini ndoo utamaduni wa Majuu huo. Ajabu mmoja alikuwa mweusi mwenzake mzungu.
Msomaji najua unaweza kuongezea yako, lakini inayosisimua sana miaka ya karibuni ni hii ya Kiarabu, yaani, Belly Dance. Bibie anakwatua kila kipande cha tako, kiuno, paja, mgongo, kimoja moja: anagawanyagawanya na kutawanya tawanya….ufundi… Limefanywa maarufu na mwimbaji Shakira (toka Columbia)…mabinti wa Kizungu wametokea kuupenda maana unasaidia mambo mengi ikiwepo kuondoa unene. Kuna huyu anaitwa Culito New…toka You Tube. Tumeulizana anatoka nchi gani (utamaduni upi)…
Huyu hajapishana sana na mwenzake. Mikatiko ya mahesabu, isiyokuwa na haraka wala simile; si tu ya matako kama wengi wanavyofanya. Inakutania na kukutekenya na kukuchokoza uwe mwanamke au mwanaume:
Baadaye nikagundua kumbe kuna mashindano mtandaoni (You Tube) ya nani anakatika zaidi. Lakini haya mashindano si ya tu ” nani anajua zaidi” ni majibishano…tena ya kimataifa. Kuna huyu Mkyuba mwenye kiuno laini: cha uji, uzi, siagi…
Akajibiwa na Msomali …ambaye bahati mbaya kaogopa kuonyesha uso wake.
Suala la kuficha uso labda linatukumbusha tofauti za kitamaduni na namna baadhi ya jamii ambazo ingawa mambo haya yapo (kama Msomali anavyoonyesha) bado zina hatari zake.
Suala la makalio na matako kuwa msingi wa kukatika (kwa wanaojifunza) bila shaka linaonekana zaidi katika hii:
Mmoja wa wasomaji mwanamke chini kaeleza namna jamaa alivyomwacha mpenzi wake (Bongo yetu) kwa kuwa anakata sana viuno. Wengine wanalilia wanawake wanaokatika viuno baadhi tunaona mbaya…
Mtindo wa Ndombolo ambao wabongo pia tumeufia kuliko hata sindimba zetu:
…Kukata kiuno si umalaya wala uchafu bali sanaa ambaye kila mwanamke (na hata mwanaume) anastahili kujua…Kwako msomaji.
Ama kweli,hiyo ndio dunia ya viuno au mauno.Nakumbuka pale nyumbani Tanzania kuna tangazo moja la kwenye luninga liliwahi kutengenezwa likimuonyesha mtoto mdogo hivi akimwaga “uno” kwa kufurahia mtindi(maziwa mgando).Lile tangazo nasikia lilisitishwa kwa sababu ya ‘ukosefu wa maadili”.Kama hilo ni kweli,basi ni sababu tosha ya kuelezea kwanini tamaduni zetu zinaigwa na wageni huku nasi tukihangaika kuiga za kwao.
Nimependa ulipokumbusha kwamba mauno huwa ni dawa tosha ya kuhahakisha wadada na wakinamama wanabakia na afya bora!Yetu macho..tukialikwa basi ngoma tutaicheza!
Hi Freddy
Mambo?
Bab kubwa lakini lazima nitoe maoni yangu kuhusu Kukatisha Viuno. Shoga yangu mmoja aliachwa na mchumba wake kwa sababu siku yao ya kwanza alimkatikia sana jamaa. Jamaa hakupenda akamuuliza nani kakufundisha huu mchezo?Akampachika majina ya kila namna (akimsuta) kisha akampiga buti. Hebu nieleze, je huyu bwege alitaka bibie alale tu kama mfu na kumsubiri jamaa amalize kazi yake?Sasa nawakanya wanawake wenzangu fikirieni mara mbili kabla ya Kukatisha Viuno vyenu kwa maboyfrendi na wachumba zenu. Msije mkajikuta mmenini…mmeachwa. Hili ni onyo tu maana dunia ya leo kuna jamaa mafala wamejaa ushamba sijui waliumbwa viwanda gani!!!
Poa basi,
Angel
Leo wakati naenda kazini nilikuwa nawaza ziara ya rafiki yangu Alain Dekula Kahanga Vumbi ambayo anaenda kuifanya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Vumbi anaenda kuungana na waliokuwa wana Marquis Du Zaire kufanya onyesho. Katika kuwaza timu ya Marquis ya miaka ile nikakumbuka safu ya wacheza shoo wa Marquis. Nikamkumbuka Dada Ngalula Chandanda na Dada Frida Shirima. Nilipomfikiria Dada Frida nikasema kimoyomoyo wanaosema mauno wenyewe Wamakonde wanapotosha. Dada Frida alikuwa anazungusha kiuno kama pia na alikuwa Mchagga.
Nikakumbuka pia Mzee Makassy aliporudi toka Mwanza alikuja na mcheza shoo mzuri ile mbaya alikuwa anaitwa Hanifa. Duh, Hanifa alikuwa mzuri sana. Yule msichana nadhani alikuwa Msukuma au Mnyanturu alikuwa anakata kiuno siyo mchezo. Nikamkumbuka na yule mcheza shoo mwingine wa Mzee Makassy Dada Anjelina wa Kupenda. Anjelina alikuwa mzuri wa umbo na sura hali kadhalika na kiuno alikuwa anakikata hatari tupu.
Nikakumbuka wanafunzi wenzangu na baadhi ya walimu wetu kule Chuo cha Sanaa Bagamoyo walikuwepo mafundi stadi wa kukata viuno.
Hitimisho
Nimezungumzia zaidi viuno vya kina dada sina maana kusema kiuno ni shughuli ya kina dada. La hasha, kama umewahi kuona ngoma za Wangoni za Kitoto na Lizombe utakubaliana na mimi wapo wanaume wanaokata viuno kupita wanawake. Wapo wanaume waliokuwa wanakata viuno kama kina Kaka Mkulu Wabangoi, Marehemu Omar Naliene na wasanii wengine wengi tu.
Mauno yapo kwenye dansi nyingi sana. Dansi ya Mapouka toka Ivory Coast nayo ina mauno ya aina yake. Halafu kuna ile ngoma Waganda. Halafu na Sunsumia ya Zenji. Mauno ya Wasomali kwenye dansi ya Niiko. Wazaramo kwenye Mganda au Mdundiko huwa wanakata viuno huku wanakimbia na kwa kufuata mirindimo ya ngoma.
Mauno ni sanaa yenye ladha ya namna yake.
Fidelis.
Fidelis anasukuma mada pale nilipotaka iende…yaani kuangalia viuno vya aina mbalimbali (sasa kaweka kuhusu wanaume) ila…
Je nimuulize Fidelis.
Mada yangu si tu wanawake na wanaume bali mimi mwenyewe kudhani (zamani) kuwa sisi Wamatumbi tu ndiyo wakata viuno. Ndiyo moja ya lengo la blogu niliyoiandika.
Na je nikuulize wewe Fidelis ndiye yule aliyekuwa bondia miaka ya 80?
Bro,
Ujumbe wako nimeupata. Asante sana.
Fidelis bondia ni rafiki na somo/wajina na y/wangu.
Tukirejea mada ya viuno sadfa na tafakari zimepeleka kukumbuka viuno anuai toka pande mbalimbali za Tanzania na dunia nzima.
Nyumbani Tanzania nimekumbuka viuno vya bara mpaka pwani: Viuno vya Bara kuna vya Wangoni, Wamanda na Wandendeule wa Songea. Vile vya Wabwari, Waha, na Wamanyema wa Kigoma. Wasukuma, Wanyamwezi, Wanyamwezi, Wafipa, Wamambwe, Walungu na Wanyiha wa Rukwa almaarufu Sumbawanga kadhalika viuno vya Waruguru wa Morogoro.
Kule Pwani kuna viuno vya Wazaramo, Wakwere na Wadengereko wa Mzizima na Mkoa wa Pwani. Kuna vile vya Wazigua, Wasambaa na Wabondei wa Tanga. Vya Wayao, Wamakua na Wamakonde wa Mtwara na ndugu zao Wamachinga na Wamwera wa Lindi. Na viuno vya Kiunguja na Pemba.
Nikaambaambaa Bahari ya Hindi mpaka Visiwa vya Ngazija nako kuna viuno vyake. Hadi Ushelisheli, Mauritius na Reunion ambako kuna viuno vya ngoma ya Sega.
Hadi Bahari ya Pasifiki huko nikakumbuka viuno vya Kimaori wa New Zealand. Na vile vya Kisamoa na Kitonga.
Na Hula Hula za Kihawaii.
Hitimisho:
Viuno sote tumezaliwa navyo si haki kwa yeyote kudai au kuhodhi miliki ya kiuno. Kila mwanadamu anacho kiuno na hukitumia kukimu matakwa, wakati, nafasi na raha zake.
Kweli au si kweli?
Fidelis sawa.
Ama kweli unazidi kupanua mada…lakini
Bado unaongelea zaidi makabila mbalimbali ya Tanzania…je “mataifa” mengine ukiacha Wabongo? Umegusa Wangazija, Wamaori …hebu endelea kwengine zaidi…au kama yupo msomaji anayeweza kupambanua zaidi…Wahindi…Wachina…Waarabu…Wahispania….?
Papaa Fredrick,
Kiuno. Mbuno kama alivyokuwa anaviita dada yangu wa Mtaa wa Konga, Morogoro havina mwenyewe. Nikimuangalia Tshala Muana na Frida Shirima na Aisha Madinda siwezi kuwotofautisha na kina Hema Malini wa Bollywood au Mchina Mei Fung wa Chungua (China).
Kuna kiuno cha Kisomali kinaitwa Niikko. Ushakiona? Na Mkongo na Ndombolo. Na vya Wakameruni kwenye makossa. Na vya MuIvory Coast na Mapouka walahi ni balaa!
Kuna viuno vya Kibashabasha vya kina Ally Tall na vile vya kina Abdulrahaman, Moddy, Aunt U (Yu) na wengineo nadhani unavikumbuka wakati wa Mbowe kabla haijawa Billicanas. Na vya chakakacha za kina Faruku na Jumanne pale Kidongo Chekundu, Gerezani. Na vile vya mashoga wa Zaitun Restaurant Clock Tower makutano ya barabara za Independence, Uhuru na Nkrumah.
Nimekumbuka mijinadume ya Kizaramo inavyosepetuka wakati ikipewa chambi ngomani.
Fredrick, cìao for now and thanks.
haya mambo ya viuno hata mimi nimegundua ni muhimu sana…nikweli watu wengi walikua na nadharia ya kufikiria kuwa kuwa ni wa matumbi tu ndio wanaokatika… kaka macha umesaidia sana kwa kuiweka wazi hii mada…
historia inajionesha kila jamii ina ngoma zake kama vile wazaramo na segere, ama wamakonde na sindimba kama ulivyosema.
kwakuongezea tu na wazanzibari nao wanakidumbaki hucheza kwa aina yake, wapigaji ngoma wanatengeneza duara katikati huweka meza ama kistuli wakina mama mmoja wao hupanda hapo juu na kuanza kulichezesha tumbo kuanzia juu kuja chini na kuchanganyia na kiuno na mara nyengine huenda mpaka chini wakafikia chuma mboga na baadae kurudi juu…basi wakina kaka wanapoona mambo yamewashinda basi nawao mmoja wao hujichanganya na kuanza kukizungusha kiuno mbele ama nyuma ya yule dada pale juu ya meza, (nafikiri hapo huonesha ni jinsi gani kukata kiuno si kwa akina mama tu bali hata kwa akina baba wamo)..
basi halikadhalika na huko ughaibuni nako kulikua hivyo hivyo wamanga ama waarabu na “belly dance” kukatika kiuno kwa waarabu ni kitu muhimu mno katika utamaduni kwani wao huanzishwa kukata kiuno wakiwa na umri mdogo sana mabibi zao huwapigia makofi na wao wakicheza hadi kufikia vigori, hatimae kuwa wari, ilikua ni aibu kubwa mwanamke wa kiarabu asijue kuuchezesha mwili wake…
na wahindi pia hawakua nyuma kwa kukata mbuno ijapokua ni kwa aina tofauti na wengine, yao kwa jina maarufu lilozoeleka wanaiita “nachi” wao kiuno chao hukatika kwa kutikisa maeneo ya kitovuni na pia kupeleka kiuno kulia na kushoto na si kukizungusha duara kama wamatumbi tufanyavyo….
natumai na mimi nimechangia mada hii maana imenigusa mno….hahahaa!!!!