
Leo nimepokea mawasiliano toka kwa mwanayansi, mwana blogu na mtunzi wa mashairi mzawa wa Kenya, Serina Kalande. Ni mmoja wa waandishi kadhaa waliopitia kitabu changu cha hadithi fupi za Kiswahili. Wengine walikuwa Mwafrika Merinyo, Padre Privatus Karugendo na Pastory Nguvu.
Soma mapitio yake dada Serina hapa:
http://serinaserina.wordpress.com/2009/02/19/kitabu-mpe-maneno-yake/#comment-371
Nimeshtushwa na kufurahishwa kwamba nina wasomaji (kama huyu) nje ya Bongo na kwamba lugha yetu tukufu ya Kiswahili inaenziwa. ”Mpe Maneno Yake” ni sehemu ya kwanza ya kitabu kilichotolewa na E & D Limited mwaka 2006. Cha pili kiko jikoni kinapikwa na kukaangwa kaangwa. Vyote vitakuwa mtindo huo huo mmoja wa visa vifupi vya kudokoa dokoa na kunyofoa nyofoa toka sehemu mbalimbali nilizopita na ninazoendelea kupita na kuishi duniani.
Kuna tatizo kubwa lakini…
Bado Bongo tuna maduka machache sana ya vitabu; halafu wasomaji wetu wanazidi kupungua. Uvivu wa kusoma uliokuwepo tangia zamani unazidi kuiva na kuota nywele, vipele na manyasi. Mmoja wa waandishi mashuhuri wa riwaya nchini William Mkufya kasema katika jarida jipya la fasihi , SOMA, kuwa idadi ya Watanzania milioni 35 milioni wanaosoma imepungua kwa asilimia 50 karibuni. Bado mtazamo kwa wengi unaimaanisha tunasoma tu tukiwa shule, kufaulu mitihani. Tukishamaliza shule basi tena kitabu hakishikwi, kinaonekana utoto; hakuna muda. Muda unainyoosha mikono yake miwili kupokea pombe, kazi, kulea, kukaa barazani kupiga soga. Haya yote ni muhimu ndiyo; lakini ukweli mmoja.
Kusoma ni sehemu mahsusi ya maendeleo ya jamii yeyote duniani. Na kusoma si tu kwa ajili ya elimu-ufundi au elimu-taaluma bali kusoma kujifunaisha kilugha na kistarehe. Haya hupatikana ndani ya fasihi, tamthiliya, sinema, muziki na sanaa.
Moja ya matokeo ya tatizo hili kubwa la kutokusoma fasihi na hadithi za kubuni linaonekana namna leo watu wengi (wazee kwa vijana; viongozi, wanasiasa , waandishi wa habari na wataalamu) wasivyoweza kuandika au kusema sentensi chache bila kuchanganya changanya maneno ya Kiswahili na Kiingereza. Bado sisi wabovu tunadhani tutaeleweka zaidi ( na kuonekana wajanja) tukiandika Kiswahili hapa; Kiingereza (kibovu) pale; Kiingereza hapa na Kiswahili (kibovu) kule. Ulemavu huu unatokana na kukosa msamiati.
Utamsikia mtu anasema eti hawezi kuandika Kiswahili maana eti hajui neno hili na lile linaitwaje au kwamba eti Kiswahili “hakina” msamiati wa kutosha!!!
Msamiati siku zote hupatikana kwa kusoma fasihi na fasihi simulizi. Wenzetu wa lugha nyingine kubwa mashuhuri duniani kiwe Kiingereza, Kispanyola, Kiarabu hata Kisomali hawababaiki vile. Moja ya siri zao kuu ni kusoma, kusoma na kusoma tena…
Mapambano Yanaendelea…
UKITAKA “MPE MANENO YAKE ”:
- Kama unaishi Bongo wasiliana na wachapishaji E & D Limited : Simu namba ( +255) 78481-8282 au (+255) 754275347.
- Kama unaishi Dar es Salaam : nenda maduka ya vitabu ya E & D Limited, TPH barabara ya Samora Avenue, au duka la vitabu Chuo Kikuu Dar es Salaam.
- Kama unaishi Ughaibuni wasiliana nami kwa simu +44-7961 833040 au ntumie barua pepe : kilimanjaro1967@hotmail.com
Baadhi ya maoni ya wapitiaji wengine:
Mchambuzi wa Guardian, Pastory Nguvu, Mei 25, 2007:
“Napendekeza kitabu hiki kwa yeyote mwenye haja ya kujua matatizo ya kijamii. Dhamira zake zinaweza kuchangia kutatua matatizo ya ubaguzi wa mbari na rangi na unyanyasaji wa watoto yatima au wasio na mlezi.”
Mwafrika Merinyo katika Mwananchi, Mei Mosi, 2007:
“…Mpe Maneno Yake ni hazina ingine katika fasihi ya leo ya Kiswahili. Kitabu hiki kinatupa fursa ya kuyachungulia maisha kwa mtazamo tofauti na kujitazama sisi wenyewe kama binadamu ambao tusipokuwa makini tunajikuta tukisombwa na dunia ya maangamizi tuliyoiumba wenyewe lakini ambayo hatuitaki! Ni moja ya vitabu adimu ambavyo vinaweza kuzua mijadala chanya ya kimaisha; tofauti na maandishi yaliyolenga zaidi kusisimua na kumlevya msomaji kama bangi ya kijamii ya kuwatajirisha wachapishaji na waandishi na kuwaacha wasomaji na maneno matupu…. Uzuri wa mtindo wa visa uliotumiwa na mwandishi ni kwamba msomaji halazimiki kusoma kwa muda mrefu sana na kuchoshwa akili kama usomaji wa riwaya.”
Padre Privatus Karugendo - gazeti la “Mtanzania” tarehe 28 Machi, 2007:
“…Kwa mtu anayesoma Mwananchi Jumapili, atakuwa amevizoea visa hivi vya Freddy Macha, vyenye ucheshi na kejeli na kuficha masuala muhimu ya kijamii, hasa yale yanayowakumba watu wa hali duni. Visa hivi ni vifupi vifupi na vingine viko kwenye mtindo wa barua, hivyo havimchoshi msomaji, bali vinavunja mbavu, vinasisimua na wakati huo huo vinaumiza kichwa. Mtu atakisoma kitabu hiki akicheka kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho, lakini hawezi kutoka mikono mitupu…..”
Habari yako ndugu yangu mwna habari mwenzangu na mTanzania mwenzangu, nimefurahia sana hii website yako japo nimeisoma kwa kifupi as siunajua hapa kwetu Tz internet ilivo tyt,shida yangu ni kwamba nimejitahidi sana mpaka nikaweza kufungua bloggu yangu lakini bado kuna mambo yananitatiza katika kui up date, nina mengi yajuwaambia lakini nakosa pakuyaweka especialyb kuhusu mambo ya elimu kwa ujmla ya Bongo, naoma tuwasiliane nipate kufikia makusudio yangu km wewe.
Thanx
Kwanza pole, Bhalilo, maana mtandao nyumbani kweli mgumu.
Lakini mambo yanabadilika pole pole kutokana na hicho chombo kilichofunguliwa Mombasa karibuni kusaidia mawasiliano ya simu, tv na intenati Afrika.
Ningekushauri uwe unajiendeleza tu mwenyewe kwa kujaribu kutembelea blog nyingine pia zile za nje utapata mawazo; vile vile weka “links” (Blogroll) na blogu zote (za wenzetu nyumbani na nje) usiwe mchoyo, maana blogging maana yake ushirikiano, mawasiliano, uraia wa ulimwengu. Tatu, tafuta namna ya kuhudhuria warsha za kila aina kujiendeleza. Ukisikia kuna mtaalamu anafanya warsha (kama sasa hivi Prof Mbele yuko Bongo, cheki Michuzi kwa habari tarehe 7 Sept) pia warsha mbalimbali za wanablogu. Cheki blogu ya Ndesanjo Macha : http:// http://www.jikomboe.com upate mpya mpya.
Mwisho endelea kuandika kama ulivyosema, hiyo ndiyo siri, kutoacha kuandika, kuandika kila wakati.
ningefurahi sana kama ningepewa njia namna nitakavyoweza kukisoma kitabu chako. mimi ni mwanafunzi wa shahada ya mawasiliano ya umma. nipo Uganda.
Fika maktaba mbalimbali za vitabu kama Soma Cafe iliyoko Mikocheni, Chuo Kikuu; au E & D Limited iliyoko Shekilango karibu na Afrika Sana.
Ukishindwa nitumie barua pepe:
kilimanjaro1967@hotmail.com