Karibu ndani; karibu chakula….sikiliza moja ya nyimbo zangu penzi unaoongelea namna mbalimbali za Uhuru; … na jinsi Uhuru ulivyo muhimu kuliko kitu kingine chochote duniani.
Niliutunga mwaka 1980 wakati bado naishi “geto” moja pale Mwananyamala Kisiwani, Dar es Salaam. Usiku nilioupika sikulala kutokana na kilio cha mwanamke aliyekuwa akikandikwa makonde, mateke, matusi na mumewe aliyemkuta kaomba Sabuni toka kwa jirani sababu ya hali ngumu ya uchumi. Ongeza pia kwamba kipindi (enzi hizo) hakukuwa na uhuru wa kusema au kujieleza kama leo….
Wanaopiga nami kushoto piano -Kaz Kasozi ( Uganda) ; besi- mdau mwenzangu wa Kitoto, Andre Mathurin (visiwa vya St Lucia); tumba (congas) -Trevor Antonio mwenye asilia ya Kiafrika na Kijamaika.
Aliyesimamia kazi hii ni Kaz Kasozi mwenyewe akishirikiana na Krawl (kamera): marafiki na ndugu katika muziki, maudhui na sanaa….
Kasozi ambaye ana vipaji vingi alikuwa pia fundi mitambo wa CD yangu ya mwaka 2000 : “Constipation…”
Wimbo mzuri na maudhui murua Kaka Fred!
Utajiri wa lugha kwako pia si haba.
Nashukuru Subi…
Sijui wasanii wetu wanaangalia nini, wanawafuata kina nani na wanapenda waje kuwa kama kina nani? Sijui ni kwanini hawatambui kuwa wanavikimbia vvuli vyao na kutamani kuonekana kama vivuli vya kina fulani? Sijuyi kwanini hawatambui kuwa muziki mzuri ni ule unaoumudu na mara zote lugha si kikwazo?
Nimeandika saana kuhusu muziki na wanamuziki. Nimewapa mifano ya kina Mtukudzi na wengine kama Sisi Tambala, Ngoma Afrika, Tatunane na wengine ambao wamefanya kazi ndani ya midundo ya asili na kufanikiwa kuliko hawa wanaoiga wasiyoweza.
HONGERA SAANA KAKA FRED. Muziki mzuri, maudhui mema na kwa tulioelewa kisa chake, inaleta hisia zaidi.
Pengine wanamuziki wetu wajifunze kutoka kwa wenye uzoefu na upeo wa muziki kama ninyi.
Ni mengi a kujivunia kuhusu uwepo wako na mengi ya kushukuru kuhusu kazi zako.
Baraka kwako Kaka
mmmmhhh!!! utajiri wa lugha ulionao umeudhihirisha ipasavyo humu…umejaribu kugusa jamii nyingi, naamini ujumbe umewafikia wengi….
huu wimbo nausikiliza na kuuangalia karibu mara tano sasa, na bado unanitoa machozi…sijui ni kwa sababu hichi kisa kinataka kufanana na changu kidogo?!!! sielewi!!! nnachoelewa ni kwamba wimbo wako umetugusa wanawake wengi sana!!!!! hakika umesema yaliofichwa kwa miaka mingi….wengi wanalifumbia macho jambo la uhuru…wengine hadi wanakufa wanaulilia…kama ulivyosema kwenye wimbo wako: ‘mkate si kitu mbele ya uhuru’ wanaume wanafikiri wanapokufuga ndani nakukupa kila unachotaka ndo imetosha na ndicho unachostahili….
sichoki kuzihusudu kazi zako mdau wa kitoto….umezaliwa kuwa msaniii kwahiyo hapa sasa unawakilisha wajibu wako.