
Nasibu Mwanukuzi au anavyojulikana kwa jina la kisanii, Ras Nas…katoka na kibao ambacho pia ni jina la Albam yake ya pili kinachoutukuza na kuughani mji wa Dar es Salaam karibuni.
Moja ya magazeti makubwa nchini humo: Dagsavisen liliipa albam hiyo nyota tano. Nyota tano si mchezo kwa mwanamuziki wa Kiafrika anayetumbuiza Uzunguni.
Niliwahi kufanya kazi na Nasibu Mwanukuzi tukiwa katika bendi ya “Sayari” mjini Dar es Salaam kati ya 1981-84. Ni mtu mwenye vipaji vingi. Anachora, mwanamichezo, mwandishi wa habari (alifanya kazi Daily News na Africa Magazine) pia kasoma si kidogo. Ana shahada ya sheria (Chuo Kikuu cha Dar, 1984) na shahada ya Mawasiliano chuo kikuu cha Oslo (1985).
Kawahi pia kutoa mkusanyiko wa mashairi ya kiingereza (Double Focus, 1989) …ndani ya kitabu mna utenzi aliomtungia Mzee (Madibo) Nelson Mandela, na aliutongoa na muziki wakati Madibo alipotembelea Oslo baada ya kutoka jela mwaka 1992.
Usikilize wimbo huu wa Dar es Salaam:
Nasibu ni kati ya Watanzania wenye moyo was kujituma na mchapa kazi halisi. Mathalan moja ya mengi anayonikosha nalo ni hili. Wakati tukiwa Sayari alikuwa mpiga ngoma, mwigizaji, mtunzi na mwimbaji. Leo hayo yashaongezeka zaidi. Leo licha ya kutunga nyimbo za Kiswahili (kama zilizomo katika albam yake ya awal, “Cut It Loose” iliyotoka 1997) anacharaza gitaa kama mnavyomwona juu….
Inatia moyo sana kuwa na Wabongo kama Ras Nas.
Ukitaka kujua au kusoma habari zaidi hebu tembelea tovuti yake motomoto :
http://www.kongoi.com.