Muda mrefu wasomaji kadhaa wameniomba nifafanue mada hii. Ni mada muhimu sana. Wastani wa maisha ya Mtanzania ( na Waafrika wengi) hata wale waliosoma au wanaojiweza kiuchumi ni miaka 40-50. Kati ya sababu kuu zinazopunguza uhai wetu ni afya, unene na kutojua kujiangalia vyema.
1-ULAJI
Ipo mifumo miwili ya kula. Chakula unachokula na namna unavyokila.
Unavyokula.
-Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku; au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache. Tumbo lina musuli zinazofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unapalilia zaidi mafuta mwili.
(PENDEKEZO la kwanza. Asubuhi, kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo chai na vitu vingine kama mkate au maandazi…)
-Wapo wanaodai kwamba wanakula matunda na mboga.
Tatizo ni kwamba mipangilio yao huwa ya makosa. Mathalan wengi hula matunda baada ya chakula. Vimeng’enya chakula (enzymes) tumboni hufanya kazi namna tofauti. Mathalan vile vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomeng’enya vitu vigumu zaidi kama nyama au wanga. Matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine. Hivyo ni bora kula matunda dakika10-20 kabla ya chakula. Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea tu juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya damu kupitia utumbo mdogo, uwengu, moyo, ini, nk.
Tatizo jingine ni kupika sana mboga hadi zikapoteza nguvu.
-Mseto wa vyakula pia ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (“acid”) na vile vinavyomumunyuka haraka (“alkaline”) havitakiwi viliwe pamoja. Mfano ni matunda. Matunda chachu kama machungwa, mananasi na maembe yatakiwa yawe pamoja; na yale laini zaidi: ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk yaende kivyake, maana yana mfumo tofauti, wa kumeng’enywa.
Hali hiyo pia iko katika nyama. Nyama nyeupe (ndege na samaki) tofauti na nyama nyekundu (ng’ombe, kondoo, nk) ziliwe tofauti.
Chakula unachokula
Waafrika hatuna tabia ya kula mboga mboga mbichi. Tunafuata ladha na mazoea kuliko thamani.
Bara letu lina mboga na vyakula bora kuliko bara lolote duniani lakini sisi tunakufa mapema na kwa utapia mlo kuliko wale wanaotoka nchi kame. Ulaya nzima imejazana mboga mboga zinazoagizwa toka Afrika. Kenya na Tanzania zinauza mboga za maharagwe mabichi (green beans), matunda toka Afrika Kusini na Ivory Coast; nk. Waafrika tunapenda kujaza matumbo. Unene umekithiri hata wale walio matajiri waliosoma bado wanakufa kwa kisukari shauri ya kutokula mboga mbichi.
Ulaji wa mboga mbichi ni upi?
Ni mathalani ulaji wa salad. Tanzania tunaita kachumbari. Lakini si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza kuchanganya matango, nyanya kwa maparachichi; au vitunguu saumu, giligilani na karote. Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukienda na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku huchangia sana katika unene.
(PENDEKEZO LA 2. Ugali kwa samaki; mboga ya majani ya matango kwa nyanya. Usiweke chumvi kwenye hiyo mboga mbichi ya majani.)
2-UNYWAJI MAJI
Waafrika hatunywi maji, hasa wanawake. Wanaokunywa maji zaidi ni wacheza michezo. Wengi wetu hunywa zaidi soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Mirinda ,Tangawizi na gesi za kisasa kama Red Bull) zilizojaa gesi inayoleta vidonda tumboni; na chai. Kuliko maji. Na maji haya hutakiwa dakika 10-20 kabla ya chakula au nusu saa kuendelea baada ya chakula. Ukila chakula huku unasakatia maji huimanisha mtu una kiu. Ulaji chakula na unywaji maji ni vitu viwili tofauti. Ila utawaona watu wanakula huku wakibugia maji. Unapokula chakula huku unabugia maji unapunguza nguvu za chakula, unajaza tumbo maji na kuchelewesha mmeng’enyo wa chakula (digestion).
Chakula kisipomeng’enywa vizuri kinaketi tu tumboni. Matokeo wengi wetu tuna matumbo makubwa. Kama hufanyi mazoezi lile tumbo linakwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo linaleta maradhi kama kisukari, kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbo, nk. Kizungu huitwa “love handles.”…
3-SUALA LA UMENG’ENYAJI
Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa (kwa lugha iliyozoeleka) mdomoni. Mate yako mdomoni ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia chakula bila kutafuna sawasawa unasababisha mambo mawili. Moja chakula kutochambuliwa vizuri, pili chakula kwenda kukaa tu tumboni, au kama kikipita hakisaidii lolote mwilini. Utafunaji wa taratibu husaidia umeng’enyaji. Chakula kinapofika tumboni hukaa pale dakika ishirini. Hapo huchanganywa na asidi (ya manjano iitwayo Hydrochloric) inayokibadilisha tayari kupelekwa utumbo mkubwa, kupitia kongosho. Kule uchafu utapelekwa chini na rutuba kusafirishwa na utumbo mdogo kuelekea katika uwengu, moyo. Moyo utadunda chakula kilichoshageuzwa damu kuelekea mwilini kufanya kazi na akiba hubakishwa katika ini.
Sasa kama usipotafuna vizuri, ukila huku unakunywa sana maji au vinywaji vingine chakula hakimeng’enywi vizuri. Ndiyo maana unawaona watu wengine wanakula sana lakini hawana afya. Wanaugua ovyo ovyo, wanatoka jasho ovyo, wanajamba ovyo, wana matumbo makubwa, wanavimbiwa, wanakaa siku nyingi bila kwenda choo (inatakiwa mtu kwenda haja kubwa mara moja au mbili kwa siku) nk.
4-ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA
Mafuta ni suala muhimu sana mwilini. Ila ulaji wake shurti uwe wa mpangilio. Yaani unaowiana. Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula vya nguvu, yaani “wanga” (ugali, ndizi, wali, viazi mbalimbali, mikate, mahindi, nk), ujenzi yaani “protini” (mboga na nyama), “madini” (mbegu mbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi) na “vitamini” (matunda, maziwa, mayai, nk).
Waafrika tunapenda nyama. Nyama ni muhimu sana maana ina madini aina ya chuma (nyama nyekundu) protini,nguvu na mafuta. Ila mafuta yaliyoko katika nyama mara nyingi si mazuri shauri hayatoki, huganda. Chukua nyama ya kuku na samaki ambayo huwa na ngozi. Wengi wetu hupenda sana kula ile ngozi ya wanyama hawa kwa kuwa tamu. Lakini haya ni mafuta mabaya.
Mafuta ya samaki lakini ni mazuri. Samaki anayo mafuta ya Omega-3 ambayo husaidia mwili na kinga maradhi mwilini.
Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima tule pia mboga za majani (mbichi) na si vizuri kula nyama kila siku. Kama huwezi kukaa bila nyama kila siku, fanya mazoezi ya mwili.
PENDEKEZO LA 3- Kula mbegu mbegu za korosho, karanga au mlozi (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi) kati kati ya siku. Haya ni mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za mafuta.
Chips za Magimbi zilizopikwa na kuonyeshwa ndani ya tovuti ya Miriam Rose , dada wa Kibongo anayetukuza mapishi ya Kitanzania duniani. Habari zaidi tembelea : http://www.tasteoftanzania.com
5-MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO
Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene.
Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu (wanachuruzikwa jasho) kwa hiyo hayo ni mazoezi. Ila kazi na mazoezi ni vitu viwili tofauti. Ingekuwa kufanya kazi ni mazoezi basi kusingekuwa na wastani mfupi wa maisha kwa maskini hasa sisi Waafrika.
Wengine watadai kwamba walipokuwa wadogo shuleni walifanya mazoezi sasa wamekuwa watu wazima (miaka 40 kuendelea) kwamba eti mazoezi ni suala la ujana; kumbe kadri unavyokuwa ki umri ndivyo kadri unavyotakiwa kufanya mazoezi na kujitazama zaidi kiafya.
Watazame Wachina na Wajapani wanavyoishi maisha marefu.
Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme (mapafu na moyo kwenda kasi), viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na usafishaji wa damu. Mazoezi yanayosaidia haya ni pamoja na kutembea kasi, kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha (kama mpira wa miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk); michezo ya kupigana na kujilinda yaani masho ati(karate, kung fu, judo, capoeira, krav maga, jiu jitsu, systema, kickboxing, thai boxing, kempo, kalari payatu, aikido, nk) …
Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali ya viungo mara mbili tatu kwa juma. Si vizuri kufanya kila siku kwani musuli na mishipa inahitaji kupumzika na kukua.
Kama unapenda kuinua vyuma lazima uwe na mwalimu wa kukuelekeza; na si vizuri kufanya kila siku. Wastani wa mara mbili tatu kwa juma inatosha kabisa.
6-UPO UFANYAJI MAZOEZI WA AINA MBILI
Mazoezi ya nguvu ya kuhema niliyotaja hapo juu (cardio-vascular) na yale laini ya kujinyoosha yaani ambayo hutumia zaidi nguvu za ndani na pumzi. Haya ya pili ni kama Yoga (India) , Tai Chi Chuan (China) na aina mpya mazoezi iliyoanza Majuu miaka ya karibuni yaani Pilates (hutamkwa hivyo hivyo ilivyoandikwa Pilates). Haya laini yanawafaa zaidi watu wazima na nchini China na Japan mathalan utawakuta wazee wa miaka 80 hadi 90 bado wanayafanya. Husaidia moyo, damu na akili.
Michezo na mazoezi ya mwili ni njia kuu ya kupunguza unene, kurefusha maisha, kuchangamsha ubongo, kupunguza ulevi, uvutaji sigara, dawa za kulevya, tabia mbaya za uvivu, ugomvi, nk. Mataifa yenye watu wanaofanya mazoezi kama Japan, Brazili, India, China nk huwa na wachapa kazi wengi na wananchi wanaoipenda jamii yao.
7-KULA SANA CHUMVI SI VIZURI
Ulaji chumvi mwingi hutokana na suala la ladha. Kisayansi vyakula vyote vina chumvi asilia sema tu tumezoea kuongezea madini hii iitwayo Sodium. Sodium inachangia sana kufupisha maisha. Huifanya mishipa ya damu ichoke; ni kama bomba lolote la maji ukilitazama baadaye hugeuka rangi kutokana na yale maji kupita pale kila siku.
Kwa wale tunaoishi nchi za joto na kutoka sana jasho kula chumvi ni muhimu. Ila tatizo letu ni kwamba hatunywi maji ya kutosha. Mtu ukiwa na kiu unakunywa soda au kinywaji cha sukari; inakuwa kama unaendelea kuutesa mwili. Kwa vipi? Mishipa inayopitisha damu mwilini badala ya kusaidiwa kwa maji inawekewa kazi zaidi ya kusafisha sukari na chumvi. Ndiyo maana vifo vingi vinatokea mapema; wastani wetu wa maisha haupiti miaka 50.
Utafiti uliofanywa chuo kikuu cha California, Marekani mwanzoni mwa 2010, umethitibisha kwamba vifo vingi duniani husababishwa na maradhi ya moyo na saratani ambavyo hutokana na uvutaji sigara, unene, ulevi na ulaji sana wa chumvi na sukari. Tukipunguza ulaji wa chumvi tunasaidia pia kupunguza maradhi ya moyo, utafiti unasema.
8-TAFITI ZA VYUO KADHAA ULIMWNGUNI KUHUSIANA NA AFYA
-Jarida la Kimarekani la sayansi lilieleza mwaka jana kwamba utapunguza ugonjwa wa moyo (ambao husababishwa na unene , wasiwasi na purukshani) kwa asilia mia 42 kama utakula matunda na mboga za majani peke yake kila siku, juu ya msosi wa kawaida.
(PENDEKEZO LA KULA- Na 4- Kula mlo wako. Baada ya saa mbili au tatu, sakatia tunda au matunda; baada ya mlo mwingine, kula sahani ya mseto wa mboga mbichi kama karote na matango. Utaona tofauti ya afya, ngozi, wajihi, kinyesi, usingizi, nk. Kidesturi tumezoea kunywa chai au soda za sukari sukari na gesi kati kati nya milo badala ya matunda na mboga mbichi za majani).
-Utafiti uliofanywa na wanasayansi chuo kikuu cha South Carolina mwanzo wa mwaka 2010 kuhusu faida za kuogelea.
Zoezi la kuogelea lina faida zaidi ya kukimbia au kutembea kwa vile huchanganya mazoezi makali na pumzi, kusaidia mapafu na moyo. Utafiti ulithibitisha kuogelea hupunguza hatari za kifo kwa asili mia hamsini.
-Utafiti wa jarida la chuo cha uganga Ulaya umeeleza (desemba 2009) kwamba kulala nusu saa kila mchana (“nap”) husaidia kupunguza ugonjwa wa moyo kwa asilimia 37.
-Uchunguzi wa chuo cha michezo cha Hispania mwanzoni mwa 2010 umethibitisha kwamba ukikimbia mara tatu kwa juma (jogging) unaongeza nyege mwilini kwa asili mia 75. Hasa kwa watu wa makamo mnaoanza kupoteza nguvu za urijali.
-Uchunguzi chuo kikuu cha Leeds, Uingereza mwanzoni mwa 2010 umeonyesha unapotembea kwa miguu, ukikwepa barabara kubwa zisisokuwa na mioshi ya magari (pollution) unapunguza matatizo ya maradhi ya hewa chafu kama pumu, mapafu na appendix.
-Uchunguzi wa chuo kikuu cha Texas mwaka 2010 umegundua kwamba kula tunda la divai nyekundu mara kwa mara husaidia kupunguza kupata ugonjwa wa kisukari.
-Hapo hapo tunaelezwa kwamba watu weusi na bara la Asia wanakumbwa zaidi na ugonjwa wa kisukari kutokana na vinywaji vya sukari sukari na gesi (fizzy drinks). Ukinywa kiasi cha miligramu 300 za vinywaji hivi (Cocacola, Red Bull, Fanta, nk) kwa siku unajitahadharisha kupata kisukari.
9-KUFUNGA
Neno kufunga linatambuliwa rasmi kuhusiana na Waislamu (mwezi Ramadhani) au Wakristo (Lenti nk). Ufungaji huo una masharti mengine ya kidini tofauti na haya ya kiafya.
Mathalani wafungaji hawa hula chakula kingi usiku; ukihesabu wanafunga wastani wa saa 12 tu. Kawaida ukitaka virusi na takataka nyingine mwilini zitoweke, au viungo vipumzike wahitaji saa 20 kuendelea.
Ufungaji ninaouongelea ni ufungaji wa kutokula kabisa kwa saa 24, 36 hadi 48 kuendelea…
Ufungaji ni nini?
Kama mashine yeyote mwili wa mwanadamu unahitaji kupumzika na kujisafisha. Hata tukiwa tumelala bado viungo mbalimbali mwilini vinafanya kazi. Kwa hiyo faida ya kwanza kabisa ya kufunga ni kuupumzisha mwili kama mfanyakazi yeyote anapokwenda likizo.
Faida ya pili ya kufunga ni kusafisha mwili kutokana na uchafu ambao haukutoka (kinyesi hakitoi mabaki yote toka utumbo mkubwa), dawa na takataka za mazingira tunayoyavutia hewa, virusi au kuyanywa katika maji na vyakula mbalimbali na pia uchafu wa hisia, yaani hasira, huzuni, nk.
Kuna ufungaji wa aina mbalimbali.
1-Kufunga kwa kunywa maji tu, saa 24 kuendelea…
2-Kufunga kwa kutokunywa maji au kula chochote, saa 24 kuendelea…
3-Kufunga kwa kula tu matunda au mboga zilizopondwa kama karote, matango nk, saa 24 kuendelea…
Ufungaji huu unatakiwa ufanywe kwa mpangilio. Kitu muhimu si tu kufunga bali NAMNA unavyofungua. Ukianza kula tena, unaanza taratibu. Kawaida ni vizuri kuanza na maji, kikombe au bilauri ya kwanza taratibu. Subiri tena nusu saa, bilauri nyingine, halafu hadi ya tatu, halafu ndiyo matunda yasiyo ya chachu, na kadhalika. Kuanza kufungua kwa kunywa chai ya maziwa, uji au vyakula vingine vya wanga hakusadii sana mfungo huu.
Maana lengo lake ni kusafisha mwili.
PENDEKEZO LA 5- Kwa wenye imani za kidini. Unaweza pia kufunga hivi ukawa pia unasali au kuvaa mavazi yanayokufanya mtu wa amani. Ukifanya hivi unajitakasa kimwili na kiroho. Si lazima ungojee ile miezi ya kufunga na wengine.
10-USINGAJI
Usingaji au masaji ni njia nzuri sana ya kupunguza unene. Ikiwa unaangalia namna unavyokula, unafanya mazoezi na kusingwa mara moja au mbili kwa mwezi unaupalilia mwili vizuri. Nini faida ya usingaji? Kusinga husaidia ngozi, mishipa ya damu na sura nzima ya mwili na taswira yako mwanadamu. Wengi wetu tunaposikia neno kusinga tunafikiria usingaji wa mapenzi. Hivi ni vitu viwili tofauti kwani usingaji wa mapenzi unaimanisha mahusiano ya kihisia.
Kifupi mwanadamu unatakiwa uwe unautunza na kuungalia mwili wako kama nyumba au hekalu lako. Wengi wetu tunaoga, tunajipaka marashi, tunasuka, tunanyoa nywele au ndevu; lakini miili yetu kiundani inaoza taratibu…
Kama alivyosema mpiganaji, msanii, mwanafalsafa, mwigizaji, mwandishi mashuhuri marehemu Bruce Lee katika shairi lake Mazingira Yako Kimya (toka kitabu “Msanii wa Maisha”, Turtle Publishing, 2001):
“NYAKATI NZURI, HAZITAKAA ZIRUDI TENA…”
(akiwa na maana yakabili maisha yako sasa hivi, usisubiri; nyakati hazirejei nyuma).
Kaka Freddy,
Makala safi sana. Nimeelimika kwa kiasi kikubwa. Nashukuru kwa sababu umekuwa msitari wa mbele kabisa katika kuendesha harakati za kuelimisha waswahili kutilia mkazo katika suala la kula kwa nidhamu. Nimekuwa nikifuatilia maandiko yako kwenye gazeti la nyumbani. Elimu unayoigawa bure kwa watanzania wenzako, si bure.
Hii leo nchi inakabiliwa na janga la vitambi. Tunapima maendeleo ya mtu kwa kutizama mtuno wa tumbo lake. Harakati kama hizi zinasaidia. Tufike mahali tuanze kuona fedheha kuning´iniza matumbo yetu kwa sababu tu eti hatujui kula kwa adabu. Pengine hiyo itasaidia.
Kikwazo kingine tunachokabiliana nacho nyumbani pia ni walimu wengi waongo. Vyombo vya habari vimeingiliwa na wafanyabiashara uchwara wanaojiita madaktari ambao kwa kweli wanapotosha jamii. Wao wenyewe ukiwatazama wana miili iliyofura mafuta, lakini hapo hapo wanadai kuelimisha watu.
Juhudi kama zako ni za kupigiwa makofi na kwa kweli nikuombe uziongeze zaidi.
Asante sana mkubwa kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kujiweka vizuri kimwili. Inapendeza watu wa umri kama wako kuwa na miili mizuri namna hiyo.
Kwakweli nakushukuru kwa elimu yako ambayo kwa kiasi kikubwa inatusaidia kujitambua. Mimi nina tatizo kubwa la kunenepa haraka nilapo sana mpaka nguo zinakuwa hazinipendezi kabisa, lakini mwili wangu ni rahisi kukubali kururdi sawa nikiu condition.
Lakini mpaka sasa bado siajapata jinsi ya kuweza ku uconditin niwe na mwili standard na wenye afya. Natumaini elimu yako inatusaidia wengi
nimependa sana ushauri wenu lakini kama huna pesa za kununua matunda itakua aje?au haina tatizo ukifatilia maadili mengini ahsante.
Je iweje baadhi yetu tuna pesa ya kununua pombe, sigara au hata kuhonga lakini tunashindwa matunda? Matunda ughaibuni ni aghali kuliko Afrika lakini watu wanajitahidi. Sisi tuna unafuu sana wa matunda. Ukweli nyama ni aghali kuliko matunda Bongo…
Big up my brother.dah nimefurahi sana sana kwa yote uloandika.mungu akupe kila la heri.Its me mtanzania mpenda maendeleo.
nimefurahia sana na jarida hili hasa kwa kuwa mnajali afya za watu. nimesoma ila bado sijaanza kufanyia kazi, bali nahaidi kulifanyia kazi ingawa huku niliko matunda ni ya shida.
swali ni kwamba, wanasema kuwa kutokula kwa muda unaotakiwa kunasababisha vidonda vya tumbo, je we we unasemaje?
Zingatia kwamba sisi tumeumbwa kufuata majira …ndiyo maana tunaambiwa mlo wa asubuhi, mchana na usiku…
Moja ya faida kubwa ya mate ni kutayarisha ulaji. Unaposikia harufu ya chakula unatokwa mate (ambayo ni sehemu ya maji yanayomeng’enyua chakula tumboni)…pia unatokwa mate unaposikia njaa …wanyama kama mbwa au kuku hufungua kinywa na kutoa ulimi nje. Watoto wadogo hulia wakiwa na njaa.
Sasa usipokula yale mate ndiyo huanza kufanya kazi ya kuvuruga tumbo (ndiyo maana unasikia mtu akiwa na njaa tumbo linanguruma)…tatizo likirudiwa rudiwa mara kwa mara ndiyo mtu anapata vindonda tumboni.
Kuna aina nyingi za “ulcer…” ile ya chakula (kama hii tunayoisema hapa) na ya kutokana na mawazo na hisia za wasiwasi (ambayo huwapata zaidi akina dada kutokana na mabadiliko yao ya mwili na hedhi au tuseme hormones kwa kimombo). Unaweza kuipata kutokana na wasiwasi, huzuni nzito, nk.
Kwa hiyo ulivyosema kwamba kutokula wakati unaotakiwa kunababisha vidonda ni sawa.
Moja ya njia za kuzuia tatizo ni kula vitu vidogo vidogo (Wazungu wanaita “snacking” yaani kula “snacks”) katikati ya milo mikubwa. Unaweza “Kusnaki” (si kwa kunywa chai kavu tu) bali kula vitafunio vidogo vidogo (vya afya) tunda, mboga kama nyanya, kunywa maji au juisi ya machungwa, kula mkate mdogo wenye kitu ndani, kula mbegu mbegu mbichi (si za kukaanga) kama korosho, karanga, nk
[…] https://kitoto.wordpress.com/2010/04/13/njia-kumi-kusaidia-kupunguza-unene/ […]
Makala yako ya njia kumi kusaidia kupunguza unene imenisaidia sana,nimekubali kwa 100%.Ninaomba sasa unisaidie zaidi Bw.Macha.MIMI NAUMWA KIUNO,HAJA KUBWA SIPATI NA MIGUU YANGU INAPATA GANZI,JE NITUMIE DAWA AU CHAKULA GANI ILI NIPONE?PIA KAMA KUNA KLINIC AU HOSPITAL INAYOTIBIA MATATIZO NILIYONAYO UNAYOIJUA TAFADHARI NIJULISHE.kwa:- 3manywa5@vodamail.co.tz
Itabidi uniandikie kirefu zaidi., mwananchi.
Itabidi ueleze unakula nini, unafanya mazoezi gani(kama unafanya), je una umri gani, wee mwanamke au mwanaume, je tatizo limeanzaje? Kazi gani unafanya?
Mara nyingi unapoumwa na kiuno, mgongo au mabega hutokana na shughuli unazozifanya. Kuna mathalan shughul zinazosababisha maumivu ya mwili kutokana na marudio rudio . Kwa mfano kama unaendesha gari muda mrefu (teksi, mabasi) utasumbuliwa na mabega na mgongo. Kama unakaa sana katika tarakilishi (kompyuta) utasumbuliwa na mabega na mgongo. Kama wewe mwanamke na unabeba sana mtoto (watoto) mgongoni, unafanya kazi za kuinama utasumbuliwa na mgongo sehemu ya nyuma katika kiuno (lower back). Inategemea unafanya nini. Ukiweza ama niandikie kirefu hapa au kama hutaki watu wasome, nieleze kirefu kwa barua pepe :
kilimanjaro1967@hotmail.com
Mara nyingi ukieleza matatizo hadharani majibu yatasaidia wasomaji wengine. Lakini uamuzi ni wako…
nimependa sana maoni yenu naomba mnitumie zaidi jinsi ya kupunguza mwili pamoja na tumbo
Ahsante Rose. Lakini mbona makala zinaelezea namna ya kupunguza “mwili pamoja na tumbo”?
Au hukuelewa ilivyoandikwa?
Kimsingi ni kutokula vyakula vya mafuta, kujali unakula nini na kufanya mazoezi. Hakuna la zaidi.
Naomba ufafanuzi nini hukuelewa…
Dah safi sana kaka! naomba ushauri kutoka kwako sababu mi mwenyewe ni mnene kiasi ila siyo sana na umri wangu bado mdogo sana nina miaka kama 22 na ni mfupi kama futi 5 hivi sasa nina uzito wa kgs 75. kitambi kimeanza kutoka.
Duuu Marco kama unaulizia nataka kufahamu moja. Je umesoma makala nilizoandika. Je umezielewa? Ngoja nirudie tena masuala ya msingi kuhusu kupunguza na kuangalia Unene:
1.Je, katika familia yako kuna unene wa kiasili (genetic)? Kama ni hivyo chunguza ni upande wa mama au baba? Na nini hasa kilichosababisha?
2. Kama si hayo angalia unavyokula. Je unapakia vyakula vya mafuta, wanga na pombe (hasa bia) kwa wingi? Je ulaji wako unakwendaje? Je unakula milo mingapi kwa siku? Mara nyingi Watu weusi tunatabia ya kula milo michache mizito, mikubwa. Ulaji wa aina hiyo huchangia tumbo kujaa haraka. Ulaji mzuri ni ule wa kula vyakula vidogo vidogo lakini mara 4-5 kwa siku. Tuseme unakula vyakula 2-3 vikuu na kati kati unaweka vitu vidogo vidogo; ili mradi usikae muda mrefu bila kula. Kama huna muda hakikisha unapokula mpangilio wa wanga (ugali, wali, chapati, mihogo, nk), protini (mboga, mboga mbichi, nyama, nk), madini (mbegu mbichi , mboga za majani kama Karote) na mafuta (mbegu mbichi, nyama za samaki nk) vimewiana. Pia kula matunda kusaidia kinyesi, kuongeza nguvu na kuondoa mafuta…Matunda lazima yaliwe wakati tofauti na ule wa chakula. Usile matunda wakati unakula msosi, bali kabla ya msosi au baina ya msosi wa mchana na jioni, nk.
3. Suala jingine muhimu ni Mazoezi. Kufanya kazi , kutembea, kuendesha baiskeli ni shughuli zinazosaidia kukimbiza damu mwilini lakini peke yake si mazoezi. Mazoezi ya viungo yanataka, Uheme, moyo uende haraka, utokwe jasho na MUHIMU ZAIDI ujinyooshe nyooshe (stretching) …Kutembea, kukimbia au kuendesha baiskeli bila kujinyoosha haitoshi maana ngozi, mishipa na mifupa yahitaji kunyooshwa. Mfano mzuri ni wanyama kama paka na mbwa ambao utawaona wanajinyoosha nyoosha kila mara.
Angalia video chini kama moja ya mifano ya kujinyoosha:
Yapo mazoezi mengine kama Yoga, Tai Chi, nk. Angalia baadhi ya makala kuhusu mada hizi ndani ya Blog hili.
4. Je unakunywa maji kiasi gani kila siku. Sehemu kuu ya mwili wa mwanadamu ni maji. Hivyo jihifadhi na maji. Ukisikia kiu usinywe Soda au Cocacola. Hivi vinywaji vina gesi tu havisaidii mwili. Vimejaa sukari. Vinaweza kunywewa kama starehe lakini si KInga Kiu.
[…] kuwa afya bora huanzia katika ulaji mzuri na mazoezi? Fanya yafuatayo kuboresha afya yako: [h=2]NJIA KUMI KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE[/h]April 13, 2010 by Kitoto blog Muda mrefu wasomaji kadhaa wameniomba nifafanue mada hii. Ni mada […]
Je unataka kusema nini , Jamii Forums???
kaka asante, ila mimi ninakilo 90,na ni mnene na sio mrefu wala mfupi naomba niambie nifanyaje ili nipungue plz naomba msaada,pia kuruka kamba inasaidia, ni vyakula vp nile vya mchemsho kama vp?
Pendo…uko mji gani Bongo?
Maana kama uko Dar ntakuwa pale tarehe 11 na 12 Oktoba nikifanya semina za afya, michezo, sanaa, nk katika ukumbi wa Fasdo, Tandika.
Mpigie simu Chande akupe maelezo zaidi.
0713-310-755
Au…
Nassib : 0713-261011
Nikuulize.
Huo unene umeanzaje?
Ulianza kwa kuzaliwa? Je, kuna ndugu wanene kwenu? Maana kama ni hivyo majibu yatakuwa mengine.
Kama ni unene wa kula, kutofanya mazoezi basi itabidi usome makala zangu vizuri.
1. Unene husababishwa na ulaji mbaya wa vyakula vya mafuta au kula sana bila kufanya mazoezi ya viungo
2. Kutokula vyakula vinavyopunguza unene kama mboga za majani mbichi, matunda na kunywa maji.
Bsi nifafanulie zaidi. Niandikie email : kilimanjaro1967@hotmail.com
upendo nyalusi
Nashukuru sana kwa maoni yako kwani unaisaidia jamii kwa kiasi kikubwa, kuwaelimisha watu kuhusu mpangilio wa chakula. Na kuiweka jamii vizuri ktk maisha haya . kweli inapendeza sana na shukrani nyingi sana kwako. Ubarikiwe sana na Mungu akujaarie sana endelea na moyo huohuo, kwani huu ni mfano mzuri wa kuigwa, Nimeipenda sana hiyo, Bwana akuongezee ufaham zaidi na akujarie afya njema na maisha marefu ili kuendelea kuelimisha jamii yetu ya Africa pic.
Tungependa utuorodheshee aina ya mazoezi yanayofaa kwa kupunguza tumbo
Nadhani imeelezwa katika makala nini cha kufanya
1. Kuanzia ulaji 2. Kufanya mazoezi
Hayo ndiyo mambo mawili muhimu; je una maana makala haikufafanua vizuri na kwa undani namna ya kupunguza unene?
Nashukuru kwa ufafanuzi wako juu ya namna ya kupunguza unene na uzito . nina hakika utanisaidia, na nitajitahidi sana kuwashauri watu wengine kuzingatia hayo. ikizingatiwa kuwa mimi ni mwalimu.
nashukuru kwa kuwa ele misha wana dam mazo wezi ni muhimu sana kwa muwili wa mwana dam
Nashukuru kwa kusoma makala hii kwani nimepata elimu nzuri na muhimu sana. Pamoja na yote naomba unisaidie majibu ya maswali yafuatayo.
Kweli mimi ni mnene na nahitaji sana kupungua lakini kwa sasa ni mjamzito wa miezi zaidi ya mitano yaani naelekea mwezi wa 6 na unene huu unanatesa na unasababisha kuvimba miguu, nifanye nini ili kupunguza unene huu kwa maana kuwa nile vyakula vya aina gani na mazoezi gani katika hali hii?
Kwa kuongezea natembea sana na ofisi ninayofanyia kazi iko ghorofa ya ano na hakuna lifti.
Pili ninapenda sana kula matunda na katika matunda ninayopenda kula ni parachihi lakini watu wanasema eti parachichi lina mafuta hivyo huongeza unene, je ni kweli parachichi linasababisha unene?
Mwisho nimeambiwa nina dalili za vidonda vya tumbo, ana sana nina aidi nyingi tumboni, je nile vyakula gani kupunguza asidi hii? Kipimo cha asidi kinaonesha PH 6.5.
Duuuu…Jane samahani sana nimechelewa kukujibu. Kwa sasa utakua mja mzito zaidi na siku zimekwenda.
Ingekuwa vyema ukaniandikia Barua Pepe : kilimanjaro1967@hotmail.com
Lakini ntakujibu haraka.
1. Parachichi lina mafuta ndiyo – lakini ni mafuta asilia na bora sana katika mwili. Mafuta mabaya ni yale ya wanyama na ndege (kuku, bata mzinga). Mafuta mazuri ni ya matunda, mbegu mbichi (karanga, korosho,nk) na samaki …Hayana madhara, tena yanasaidia sana.
2. Kuvimba miguu ni dalili ya mzunguko mbaya wa damu na maji mwilini. Unalotakiwa kama unaishi mji mkubwa kama Dar es Salaam ni kutafuta madarasa ya Yoga kwa kina Mama. Zamani nikiishi hapo Wahindi na Wazungu walikuwa wakitangaza sehemu za akina mama tu kufanya mazoezi haya…bado yapo…maana siku hizi kuna wazungu zaidi Bongo kuliko enzi nikiishi hapo miaka ya Themanini.
Jingine ni kutafuta sehemu ya kufanyiwa usingaji- lakini msingaji (maseuse) awe anajua anachokifanya. Si wale wa mitaani, wasiosomea.
Kama ukitazama matangazo yanayowekwa katika majarida ya Wazungu katika miji mikubwa Bongo utakuta wanatangaza Maseuse/ Massage. Ungetafiti hilo.
Usingaji kwa kina mama waja wazito ni muhimu sana.
Pia unaweza kujisinga mwenyewe miguu ukishakoga. Unaanzia mapajani , magotini hadi chini kabisa. Unajisinga kwa mafuta ya mboga (si yale yenye marashi au wanayoita Moisturiser)…mafuta ya mboga (“Vegetable oil”)
3. Tatu, kutembea ni muhimu sana, na kuwa unafanya shughul zote, (kuwa “active”) badala ya kula na kukaa tu. KUpanda ngazi sana si vibaya lakini isikutese. Ila si vibaya maana itasaidia utakapojifungua. Mradi huteseki.
4. Ulaji matunda unakuwa na nguvu mwilini ukiwa kabla ya chakula. Nusu saa kabla. Au unakula matunda asubuhi kabla ya chai na staftahi. Au jioni kabla ya mlo wa usiku, nusu saa kabla. Au kati kati ya milo mikubwa. Usile matunda na chakula. Pia matunda usichanganye yale ya “acid” (mananasi, machungwa, maembe, nk) na “alkaline” (ndizi mbivu, parachichi, tikiti maji, nk) pamoja. Ukila aina moja leo, kesho au saa nyingine aina nyingine.
5. Je unakunywa maji mara kwa mara? Pia usinywe maji na chakula. Kunywa maji nusu saa kabla au baada ya msosi
6. Kama una “acid”- je imetokana na nini ? Ni ile acid ya vurugu mechi (“stress”) au ya vidonda tumboni?
Kama ni ya stress unatakiwa ufanye vitu vinavyokufurahisha uepuke vurugu , ugomvi na tafrani. Ya vidonda tumboni yataka ule sana mboga mbichi za majani. Hizi ni “salad” kwa Kizungu. Husaidia sana tumbo. Mboga hizi za majani ziwe sehemu ya milo yako yote. Kama mathalan unakula chakula chenye wanga sana (wali, ugali, nk) na nyama au mchuzi wowote, lazima uwe na mboga ya majani mbali na mchuzi(hata kama ni wa majani au maharagwe)…ukipikwa si “salad.”.
Mboga nzuri kwa waja wazito ni kama nyanya, karote, matango, nk. Jaribu kula tofauti kila mara. Karote ni nzuri na muhimu sana kwa kina mama hasa ngozi, kucha na nywele…
7. Unapokula usijaze sana tumbo, kula hadi umefikia hatua ya kubakisha nafasi tumboni. Baadaye kidogo ukisikia njaa ule vitu vidogo kama matunda, mbegu mbichi (korosho, karanga, nk)
8. Pia kama una vidonda tumboni usiweke pilipili au chumvi nyingi katika chakula. Jaribu kula mboga na supu iliyochemshwa na kunywa maji kw awingi (si pamoja na milo yako). Ukweli chumvi na pilipili si vizuri vikizidi au kuwa mara kwa mara hasa kama una vidonda tumboni. Kama una mazoea navyo hakikisha unakunywa sana maji (si na chakula, mbali ya chakula)…
Basi niandikie barua pepe kama ukitaka maelezo ya undani zaidi, maana sifungui Blog kila mara.
Nakutakia kheri:
kilimanjaro1967@hotmail.com
asante kwa ushauri.mimi nilipokuwa mdogo nilikuwa mwembamba sana lakini sasa ni mnene,nina umri miaka 22,kilo 73,jinsia male,ni miezi mingapi inatosha kupunguza unene kwa kufanya mazoezi ya kukimbia?huwa nazunguka uwanja wa mpira mara kumi kwa kukimbia,je hii inatosha au niongeze round za kukimbia?je,ukifunga saa 72 kila wiki huku ukiendelea kufanya mazoez inaweza kuwa na hatari?je unyanyuaji wa vyuma(gym) hupunguza unene?
Steven, samahani nimechukua muda kukujibu. Mazoezi ya mtu kama wewe yanatakiwa yaangaliwe kwa kina sana. Itakuwa vyema kama ukiniandikia Barua Pepe nikufafanulie mambo kwa undani zaidi. Niandikie : kilimanjaro1967@hotmail.com
Ila kijuu juu naweza kukujibu hivi.
1. Mazoezi hayafui dafu kama huangalii unavyokula. Kama chakula chako kimejaa mafuta, wanga sana au unakula vyakula vikubwa vikubwa mara chache kwa siku….badala ya milo midogo midogo michache…haitoshi.
Tunaweza kuangalia hilo kwa undani zaidi.
2. Mazoezi ya viungo yamegawanyika sehemu kuu mbili – Cardio (Cardio vascular) na Strength/fitness/relaxation.
Unapokimbia hiyo ni Cardio. Hutakiwi ukimbie kila siku. Pumzika siku moja au mbili kisha ufanye mazoezi ya ujenzi wa nguvu kama vyuma. Na uinaji vyuma una mipango yake. Naweza pia kufafanua zaidi nikijua unatumia vyuma gani. Kifupi badili siku moja Cardio (mbio, kuogelea, yaani mazoezi ya kuhema) pumzika kabisa siku moja, halafu inayofuata fanya yale mengine. Kila unapofanya lazima uhakikishe unaweka “stretching”…je unafaham stretching ni nini? Kama unaye rafiki anayefanya Karate, Ngumi, Mpira au Judo muulize atakufafanulia maana ya “stretching” – kifupi ni kujinyoosha, kama Paka anavyofanya kila mara. Ndiyo maana ana maisha marefu kuliko wanyama wengine.
3. Ulaji wako lazima uzingatie mazoezi. Mathalan siku unayofanya mazoezi makali hakikisha mlo wako na unywaji maji vinafuatana. Siku unayopumzika unakula vyakula vya kujenga mwili kama maziwa, mboga mboga za majani, nyama, nk. Usile hadi ukajaza sana tumbo, ila uwe unakula milo midogo, midogo kwa wingi. Na usile usiku sana ukalala na tumbo limejaa. Maana kuna Waafrika tuliozoea kula saa nne , tano usiku kisha tukalala na matumbo mazito. Hiyo ndiyo moja ya sababu watu weusi tuna matumbo makubwa sana. Hakikisha unakaa saa tatu nzima kabla ya kulala baada ya kula. Nausinywe maji( au vinywaji vingine) na chakula bali nusu saa kabla au baada ya kula. Hii inasaidia zaidi umeng’enywaji wa msosi.
Ahsante sana ntajitahidi kula matunda hasa matango na carrot kwakuwa awali nilidhani ni matunda cyasiyo na hadhi
Mungu akubariki kwa maelezo yote uliyowaelekeza wadau wenzangu hapo juu, tatizo langu ni kama la pendo na nimesoma yote uliyomuelekeza, nitayafuata na kujitahidi kufanya mazoezi na kupunguza mlo. Be blessed!
JE INAKUAJE MTU KUKAA MUDA MREFU BILA KULA MAANA UKIJA KULA AU KUNYWA KITU CHOCHOTE TUMBO LINAUMA
Beatrice, unaonaje ukiniandikia…barua pepe. Maana hilo ni suala la kufunga. Kuna ratiba zake.
: kilimanjaro1967@hotmail.com
Nimependa sana na pia nimeelimika sana laki nilikua na ombi kama ungeweza kuandika kila chakula tunacho kula kina kaz gan mwilin ningefurahi sana. Kua na moyo huu wa kuelimisha jamii ya Kitanzania . Cku njema
I really appreciate this topic,,,,,,thank you alot,,give us more and more.
Yap this is goood news big up mwanangu
Ahsante sana kwa kutuelimisha kiafya ila mm ni mnene kupita kiasi na yote hayo nimeyafanya na sioni mabadiliko je nifanyaje////?????
“Yote” umefanya yapi kaka? Ingebidi ueleze kirefu zaidi…maana huenda kuna jambo unalifanya kwa makosa…au pia kuna unene wa kuzaliwa…ambao yabidi ukaliwe kwa makini…
Kifupi, nifafanulie kirefu kwa barua pepe unafanya nini, unakula je ili tuone la kufanya na kujaribu…
kilimanjaro1967@hotmail.com
nashukuru sana kaka kwa kutuelimisha kwa kwel;i nimefarijika sana na uelimishaji wako kwani mmi nilikuwa sijui mambo mengi..mungu akubariki sana.
swali langu ni kwamaba vinywaji kama Bia vinaongeza ukubwa wa tumbo yaani unapovitumia kwa sana?
Ndiyo bia kwa wingi huongeza tumbo ndiyo. Lazima ufanye mazoezi mara 2-3 kwa wiki kama wewe mnywaji sana. Halafu inasababisha kisukari, maradhi ya ini nk.
Nashukuru kwa ushauri wako mzuri je maji ya uvuguvugu ni mazuri kutumia kwenye kupunguza mwili?
Zainabu….Kawaida maji (au vinywaji) vya moto au vuguvugu ni bora kuliko vya baridi…shauri ukichunguza… ndani ya mwili vitu ni vya joto…hivyo tunavyoweka baridi tunaupa sana kazi mwili…maana inabidi kupoozesha kwanza halafu kuyafanyia kazi…(ni kama kuwasha gari moto ambalo limekaa katika barafu mda mrefu)…lakini kuhusu kupunguza unene au kuufanya uwe mwembamba watu husema kila aina ya mambo. Kwa mfano wapo wavuta sigara wengi wanaosema …au kuamini sigara inasaidia kupunguza unene. Lakini je, athari za sigara ndani ya mapafu, ngozi, moyo, nywele, uzuri na viungo mbalimbali mwilini (ukiwemo ugonjwa wa saratani) ni ngapi na zipi? Nyingi sana.
Upunguzaji unene unategemea mawili: chakula unachoweka tumboni na mazoezi ya viungo(wastani wa mara 3 kwa juma). Kijumla, namna unavyoendesha maisha yako. Utafiti wa miaka mingi uliofanywa nchi zilizoendelea umethibitisha kwamba afya ya wanadamu inategemea sana wanachokula, wanavyokula na wanavyoendesha maisha yao(“life style”). Majuu wanasisitiza sana ufanyaji mazoezi na kula vyakula visivyo na mafuta, chumvi na sukari nyingi, nk.
Kurejea kwenye suala lako la maji.
Unywaji maji dakika 20-30 kabla au baada ya kula chakula una uzito zaidi kuliko kuyanywa wakati wa kula…wengi hawatambui hilo na hujaza maji (au vinywaji )tumboni wakati wanakula na kuchelewesha au kuupa sana kazi mwili wakati wa umeng’enywaji mlo.
kaka kuna dawa ya kupunguza mafuta yliyojaa mwilini,ambayo inabili fats to energy lakini inaambatana na mazoezi kwa muda usiopungua saa moja vp inafaa?
Miye hizo “quick fix” za aina hiyo siamini hata kidogo. Mafuta mwilini ni leseni ya kifo. Jaribu kuzingatia mazoezi na ulaji. Kwa kuanzia nikuulize kama huwa unakunywa maji. Si kunywa na chakula lakini. Kama wewe mnene na hunywi maji basi hapo kuna tatizo. Anza kwanza kwa kujibu na kuzingatia suala la unywaji maji- maana hilo ni mwanzo wa kusaidia kusafisha mzigo.
maji nakunywa sana bro 3lt/day, nikiaka asubuhi nakula matunda tu, mchana sili nakunywa sana maji, saa10 jion nafanya zoezi kukimbia na kucheza mpira saa1.30 nakula chakula kidogosana lakini bado uzito unaongezeka kaka nifanyeje?
safi sana inatia moyo, ubarikiwe na
nashukuru kwa ufafanuz mzur mungu akubariki
ninepata kufahamu
mie kiukwrli ni mnene sana tu nanahitaji sana sana sana kupungua….ninekuwa nikiamka tu nakunywa maji ya amdalasini glas nne na baadae kuendelea na shughuli mpk saa nne nakunywa chai na chapat mchana nakula ugali wa dona na samak dagaa au kuku jion napata matunda ndio nineanza je itanisaidia?na je maji kipimo gani kwa siku ndio kibafaa maana maji kwangu ni tatizo pia ila kwa somo hili nirayapa nafasi kubwa sana.ubarikiwe sana
Sabrina…tunatakiwa kunywa bilauri au glasi 8 kwa siku. Lakini si kunywa maji mengi kwa mpigo. Ukubwa wa tumbo lako kumbuka ni saizi ya ngumi yako.
Hivyo kunywa maji katikati ya milo. Ukiamka- ni vyema kunywa maji moto. Mi kwa mfano sinywi chai asububi. Nakunywa maji moto. Kisha matunda…halafu baada ya dakika chache (10-15) ndiyo napata staftai.
Kawaida sisi Waafrika hatujui kula kidogo kidogo. Milo mikubwa mitatu…ndiyo lakini yatakiwa katikati ya hiyo milo mikubwa tule vitu vidogo vidogo : kama mbegu za karanga, korosho (zote mbichi si za kukaanga na chumvi); matunda au hayo maji. Si kula chakula na maji meeengi. Hapana.
Vinywaji visiwe na chakula kama nlivyoandika katika hiyo makala yangu.
Kuhusu ulaji wako…umesema wala matunda. Ni sawa kabisa. Matunda yanaweza kuliwa wakati wowote lakini yasichanganywe na msosi. Wala yasiwe baada ya msosi bali kabla. Pili, hayo matunda usichanganye “ya chachu” (machungwa, maembe, mananasi) na yasio chachu (mapapai, tikiti maji, ndizi mbivu nk)…Leo ukila chachu kesho usile chachu,…jioni ukila chachu, asubuhi au mchana kula yasio chachu nk. Ili mradi usichanganye.
Mwisho, kama unataka kupunguza unene, pia lazima kufanya mazoezi ambayo yanakufanya uheme na kutota jasho (cardio-vascular exercise)…mara 2-3 kwa juma kati ya dakika 30-45 kila ufanyapo yatosha kabisa. Yaweza kuwa kuogelea, kukimbia au hata kutembea mwendo wa haraka kwa hizo dakika 45. Walakin…Si kufanya mazoezi kila siku. Lazima unafanya halafu unapumzika …siku moja au mbili.
Jambo jingine unaloweza kuongeza ni pia kufunga. LAKINI si kufunga kwa KIISLAMU. Maana mfungo wa Kiislamu, nk…. una misingi ya kidini; yaani kula usiku. Unafunga saa 36 kuendelea. Ukila leo jioni huli tena hadi kesho kutwa asubuhi au jioni.
Na muhimu sana kujua nini unafanya ukifunga.
1. Unaweza kufunga kwa kunywa maji tu -saa 36-48. Yaani unakunywa maji pale unaposikia njaa. Na maji unakunywa kidogo kidogo…kwa taratibu.
2. Unafunga kwa kula matunda kidogo tu jioni aina ya yale yasio chachu -mathalan mapapai, ndizi mbivu au maparachichi( mseto au aina mbili)
3. Huli kitu lakini unafanya mazoezi ya Pumzi kama Yoga au kusali tu. Lakini zingatia kwanza kama moyo wako uko sawa. Kama una presha au mja mzito usifanye hili.
4. Watu wengi wanafunga vizuri lakini hawajui kufungua. Hutakiwi unafungua kwa kula sana. Unaanza na maji moto. Una subiri dakika 30-60. Unakula matunda (sio chachu). Unasubiri dk 30-45, ndiyo una kula mlo mdogo, mathalan mlo wenye Salad mseto (nyanya, matango nk). Baada ya saa mbili-tatu ndiyo unakula mlo mzito. Kufungua ni muhimu kuliko kufunga.
Nimesahau kukuuliza kama ulisoma makala yangu katika Citizen karibuni kuhusu ulaji CHUMVI. Hebu pitia blog la MAKALA ZANGU
http://www.makalazangu.blogspot.co.uk/
Na unapokula usibugie…
Kama una maswali zaidi uliza tu…
Ningependa kujua unywaji wa maji mwisho lita ngapi kwa siku na tunashukulu kwa elimu yako maana sie wengine tulikuwa hatujui kabisa mamiili makubwa na hali ya maisha ngumu kweli Mungu akupe maisha marefu ili uendelee kuelimisha na wengine
Bwana Geofrey Mwatonoka, nashukuru kwa maneno yako na ahsante kwa swali. Sasa sikiza ndugu yangu. Mambo kadhaa ya kuzingatia kuhusu unywaji maji.
1. Miili yetu ni asilia mia 60 maji. Hivyo lazima kunywa maji kusaidia uma maji unaotoka kwa kutoa pumzi, haja kubwa na ndogo, jasho nk
2. Si rahisi kusema kila mtu anywe maji kiasi fulani maana kwanza inategemea mazingira ya mtu. Ukiwa mazingira ya kazi za sulubu za kutoka jasho zaidi unahitaji maji mengi kuliko yule anayekaa chini kutwa. Au kama wee mlaji wa chakula chenye chumvi nyingi unahitaji maji zaidi kufidia ile chumvi mwilini ambacho si kitu kizuri. Hivyo inategemea mtu na mtu.
3. Ila madaktari na wana afya wengi wamesema kwamba wastani wa kila mtu ni kunywa glasi au bilauri 8 kwa siku. Wengine wanasema mwanamke anywe vikombe 9 na mwanamume 13. Ila hilo la bilauri au glasi 8 kwa siku ndilo linaloelezwa dunia nzima.
Jaman nashukuru kwa mada,
mimi ni mnene nachukia unene ila najaribu kujinyima lakini ndo kama nakaribisha kitambi. nimeacha vyakula vya mafuta, sukari, lakini wapiiiiiiiii?
nakimbia kila siku napanda mlima, naendesha baiskeli, siungi chakula lakini kama ndo nakipalilia. Bia sinywi mwezi wa tatu sasa. nisaidieni wajamen.
Audax, ahsante kwa kuwa muwazi, na kutaka maoni.
Unene unaweza kusababishwa na mawili- maisha unayoishi kwa jumla(ntafafanua kidogo mbele) na hali ya kuzaliwa (familia, urithi wa wazazi nk).
Kwa hiyo kwanza jaribu kuchunguza kama katika familia kuna unene asilia.
Sasa tukija katika maisha kwa jumla – makala yangu imejaribu kuangalia njia za kupunguza lakini sikuangalia sana sababu kwa undani.
Kati ya sababu ni hivi:
1. Mtu unavyoishi – vyakula unavyokula mambo unayofanya. Kwa mfano unaweza kuwa unafanya mazoezi sana ya kukimbia, lakini je unajinyoosha (“stretching”) kabla na baada ya kupanda milima au kukimbia? Je, mazoezi unayoyafanya yako vipi? Ndiyo maana ni vyema sana kuwa na mtaalamu wa mazoezi unapoanza…
Kama unafaham mtu anayefanya Karate, huwa wanafanya mazoezi mazuri sana ya “stretching” na kujinyoosha.
Nimeona watu kibao wanakua Gym – anainua vyuma lakini anafanya mazoezi saa tatu nzima. Anafanya kila siku. Huko si kufanya mazoezi ni kuutesa mwili. Unatakiwa ufanye mazoezi mara tatu kwa juma, kifupi unafanya na kupumzika kuruhusu mwili kukua. Ni kama kuwa na mimea ukaimwagia maji kila siku. Itakua sawa kweli?
Kwa hiyo kwanza chunguza unafanyaje mazoezi.
2. Mambo madogo madogo yanaweza kuchangia kupunguza unene. Mathalan, utafiti uliotoka mwezi huu hapa Ulaya umesema wanadamu hatuli matunda na mboga mbichi za majani vya kutosha. Wengi tunatafuta zaidi ladha. Chumvi nyingi, mafuta ya kukaanga nk.
Jaribu kuwa unakula vyakula kwa kiasi kidogo, au kama unakula milo mikubwa kati kati ya njaa na msosi mkubwa unakula matunda. Ukitaka ufafanuzi zaidi kuhusu ulaji matunda -tazama makala nliyoiandika juma lililopita kuhusu mapapai na maparachichi. Matunda yanasaidia sana kuchuja unene. Na namna ya kuyala nimeeleza pale pia.
Suala la pili ni mboga mboga za majani. Je, Waafrika wangapi tunakula “salad”? Misosi mikubwa mikubwa bila mboga za majani mseto. Hata zikipigwa zinachemshwa hadi zinakwisha nguvu, au kama ni mbichi kama matango zinawekwa tena chumvi. Kwanini uweke chumvi katika mboga za majani? Na mchuzi wa chakula ushaujaza chumvi na pilipili?
Hivyo chunguza je unakulaje?
Tatu ni maji ya kunywa. Unene unaweza kupunguzwa sana na unywaji maji. Waafrika wengi tunaishi nchi za joto. Ukichunguza wengi tuna macho mekundu sana. Dalili hatunywi maji ya kutosha. Tukinywa “kitu” huwa cha “ladha” (sukari hasa , ambayo inaongeza unene) yaani soda, vinywaji baridi (kama juisi) au chai. Maji ni muhimu sana. Glasi au bilauri nane kwa siku – na kama unafanya mazoezi lazima unywe maji – kabla (nusu saa kabla) na baada.
3. Umetaja pombe. Pombe si kitu kibaya kama unakunwya kidogo. Mathalan bilauri au glasi moja ya mvinyo (“wine”) si kitu kibaya mara mbili tatu kwa juma baada ya msosi. Lakini ubaya wengi hawajui hivyo wanataka wazidishe hadi wanapepesuka. Mvinyo hata bia moja tu ni sehemu ya chakula na inasaidia mambo kadhaa mwilini- kama kinga maradhi nk.
Kifupi haya ndiyo baadhi ya mambo unayoweza kujaribu kuchunguza.
Tuendelee kuwasiliana.
Au ukitaka mawaidha ya karibu zaidi niandikie barua pepe…
kiukweli nilifika hapa kwa bahati ila tu niseme hii imetulia nimeipenda na labda niombe idhini yako niitoe nakala kwenye karatasi na kusambaza kwa watz wengine zaidi kwani maelekezo haya yataleta uponyaji zaidi
Ahsante Mjema…lakini unaposambaza lazima useme makala imeandikwa na nani na inatoka wapi. Maana unavyojua suala la haki miliki nchini kwetu haliheshimiki. Nashukuru
as
asante sana kwa makala hii kwasababu imenielimisha sana mana nilikuwa najiua
nimefurahi sana
asante sana kwa kutuelimisha, Mungu akubariki, mada imeeleweka sana, je ganzi ya mikono inatokana na nini? je mazoezi ya tumbo ya kulala chali na kuinuka yanafaa? naomba utaje mazoezi ya tumbo mengine hasa kwa mama aliyetoka kujifungua
Ganzi ya mikono wakati gani Mama Nego? Maana ganzi yeyote inaweza kuwa hitilafu la mzunguko wa damu mwilini.
Iikiwa mikononi au miguuni ina maana kuna upungufu wa madini au wingi wa wa kitu fulani mathalan chumvi sana …lakini mara nyingi ni mzunguko hafifu wa damu na maji mwilini. Ila….Naomba fafanua zaidi hiyo ganzi inakua lini na huchukua muda gani.
Kuhusu kulala chali na kuinuka (“sit-ups”) inafaa ndiyo ila mazoezi yeyote ya viungo yanatakiwa yafanywe kwa kuanza kuupasha kwanza moto (kutembea haraka, nk) kabla…na hayatoshi peke yake. Inabidi pia kuangalia mlo, na kufanya angalau mara 2-3 kwa juma. Yaani unafanya leo, kesho unapumzika,nk. Si kila siku.
Kwa kina mama waliojifungua mazoezi yanatakiwa yaanze taratibu…kuna Pilates, Yoga, Kuogelea nk. Jaribu kuangalia You Tube siku hizi mengi sana. Nimekuwekea hili moja halafu ukishatazama utaona mengine yanajitokeza:
dah me nataman miguu yangu ipungue iwe ya wastan coz hata kuvaa sketi nashndwa nikipita napata ma2c xana ni minene
Pole sana Catherine. Unene wako ni wa kuzaliwa au wa namna unavyoishi (kula, kutofanya mazoezi)?
Na je umechukua hatua gani ?
dah hata me ntafanya hvyo kupunguza uzito jaman
Nimependa ushauri wako na nimeelimika kwa kias kikubwa.mungu akubarik kwa kaz yako nzur ya kuelimisha watanzania
Nimependa sana somo lako,ila naomba utuwekee ratiba ya kula vyakula vya kufanya mwili uwe na muonekano mzuri,ikiwezekana tupangie kuanzia jumatatu hadi jumapili,pia sambamba na mazoezi tutafanya.
Wazo zuri sana Noel John. Ntajitahidi nipata muda. Vitambi, matumbo na maradhi ya moyo vimezidi
Nashukuru sana kwa ushaur wako nimeupenda sana utanisaidia kwa kiac kikubwa san maana na mm ni miongoni mwa waasirika wa kuwa na tumbo kubwa
Nimefurahi kusoma malaka hii japo ni ya sikunyingi ila imenijuza mambo mengi sana sikweza kuyajua zamani,ulaji mzuri kwa mpangilio ni tatizo kubwa sana kwangu.pia mazoezi nimejua kumbe ninaweza kufanya mazoezi hata ya pumzi yakanisaidia pia….Ehee tatizo langu lingine ni chumvi sana siwezi kula chakula chenye chumvi kidogo nabadilisha kwanzia leo…,,masaji nayo sikuitilia sana maanani na kumbe ni muhimu,pia kufunga sikujua kuwa kumbe natakiwa kulipa tumbo langu likizo hahaha..Thank you so much….
Nimebahatisha tu kuipata hii makala,nakupongeza kwa Kazi Nzuri unayoifanya maana nimeisoma ,nimeelimika sana. nashukuru pia kuwa huchoki kuelezea mtu akiuliza unakuwa tayari kurudia ilimradi aelewe,mungu akubariki sana popote pale ulipo na yoote uyafanyayo. Nakuombea Maisha marefu hakika.
nashukuru nimejifunza mengi mno kupitia somo lako nafikiri nitaanza kufanya hayo yote ili niwe na afya njema daima. mungu akubariki na akupe afya njema pia
Ahsante kaka nimekusoma vizuri. Mungu akuzidishie nguvu uweze kutuelimisha zaidi
cool
shukran za dhati zikufikie coz nimepata darasa nzuri thanx
ninakunywa maji ya moto lakini napungua mwili mzima naomba mnisaidie jinsi ya kupunguza tumbo peke yake
Kupunguza tumbo haitoshi kufanya jambo moja tu Mary. Wala halina ufumbuzi wa haraka. Yataka utazame suala zima ya namna unavyoishi, unavyokula, ufanyajaji mazoezi ya viungo, nk. Pia zingatia kama umeshazaa au ulizaliwa na unene nk. Je umesoma makala kuhusu namna ya kupunguza unene katika blog hili hili la Kitoto? Hebu itazame uisome kwa makini maana nimefafanua na kuchimba kwa undani.
Na je umenisoma ninavyoongea masuala ya unene, ulaji na mazoezi katika safu zangu za Mwananchi Kila Jumapili? Kama bado jaribu kuzitafuta au tembelea blog la Makala Zangu ambapo hutoa maandishi yangu ya zamani magazetini.
Naomba unitumie material ya kupunguza mwili na tumbo na nini nile yaani balance diet nashkru kwa mada email yangu ni atrash022@gmail.com
Naomba wewe uniandikie kupitia kilimanjaro1967@hotmail.com
Unifafanulie zaidi swali na kwa nini au kwa vipi makala niliyoandika hapa haikukutosheleza? Nieleze kinaugaubaga
Asante,kwa ushauri mzuri,nitaufanyia kazi,,be blessed.
Kaka hongera sana kwa makala zako nzuri zenye kuelimisha, kuanzia leo nitakufuatilia nielimike zaidi. Swali ni aina gani ya mazoezi yanayopunguza kitambi kwa haraka zaidi?
Mazoezi ya aina mbili. Yale yanayokufanya ujenge mwili, uukuze uwe imara, kwa kuinua vyuma au zana nyingine. Au kujijenga kwa kupumua kama Yoga, Tai Chi nk. Mazoezi ya aina ya pili ni yale unayofanya kwa haraka ili uheme na kutokwa jasho. Yanaitwa “cardio-vuscular” ikiwa na maana kukimbiza au kuchangamsha moyo. Haya ya aina ya pili ndiyo unayotakiwa kufanya kupunguza unene. Pia hujenga uvumilivu kama wa kutokuchoka (stamina), kutokuwa mvivu nk.
Ukweli bwana Bakari watakiwa kuchanganya. Mathalan katika juma. Unafanya leo ya haraka. Kesho unapumzika kwa kufanya yale laini kama Yoga na kuvuta pumzi. Kesho kutwa una pumzika na kuzingatia ULAJI. Mtondogoo unakwenda tena ya haraka. Unapumzika kesho yake halafu unafanya yale laini nk. Unatakiwa uwe unachanganya na huku ukizingatia kupumzika na ulaji. Kunywa maji, matunda, nk
haya mazoezi ya haraka yanaweza kuwa pia kuogelea, kukimbia, kutembea (dakika 20-30) kila siku kwa haraka kisha unajinyoosha kwa “stretching” nk
Lakini mazoezi lazima yaende pia na ULAJI…Huwezi kuwa unafanya mazoezi halafu unaendelea kula nyama na wanga kila siku. Lazima ule matunda na kunywa maji kwa wingi. Tafadhali soma makala zangu hapa hapa katika Blogu kuhusu namna ya kula matunda. Siyo kula matunda na chakula bali kuyala peke yake. Na kuwa na mpangilio wake. Kwa mfano usichanganye matunda matamu (kama mapapai, maembe, ndizi mbivu nk) na matunda chachu (Machungwa, mananasi nk) …uyale nyakati tofauti. Matikiti maji na maparachichi yanatakiwa kuliwa peke yake bila tunda jingine. Hii ni shauri umeng’enywaji wake ni tofauti na matunda mengine. Soma makala ndani ya Blog hii hii.
eh bwana kaka nimejifunza mengi,na pia mungu akupe nguvu ya kuwa na wigo mpana juu ya masuala haya ya afya hususani kwa watanzania. japo nina rai juu ya aliyesema kufanya kazi ngumu syo mazoezi kwamfano mtu amelima eneo kubwa na pia jasho limemtoka kwa wing alafu mtu huyohyo atoke akafanye mazoezi mengine je nisaw?
makala safi sana hii imenielimisha saana
Thanks for your education
barikiwa saana mpendwa, ama kweli nimeelimika sana! lakini napenda kukutumia e-mail address yangu ili unisaidie kuniandikia ratiba ya kupunguza mwili vikiwemo aina ya vyakula ninavyotakiwa kutumia kwa wiki nzima, mazoezi kwa wiki nzima, maana hata mimi nina uzito wa kilo 90 na umri wangu ni miaka 26. kwa hvyo naona ni tatizo. Ahsante!
Ah wewe niandikie katika Email yangu. Maana sitakuwa na muda wa kukutafuta.
Email yangu ni gmacha52@gmail.com
nashukuru sana kwa ufunuo ulotupa juu ya masuala ya afya na vyakula
mimi nina shida moja ambayo imenikumba takriban siku kadhaa sasa..
kooni kuna kama kitu fulani kinanikereketa hivi na kuna muda nikimeza mate panauma na kuna muda kama panakauka hivi na ninapomeza mate kama kuna kitu kinalia hivi……
sasa sijui tatizo linaweza kuwa ni nn?
Saa nyingine mtu anapouliza jambo unashindwa kuelewa utamjibuje maana haelezi anavyoishi. Je, hii kauka koo ilianzaje? Je una umri gani? Je huwa unakunywa maji ? Je ukimeza chakula au maji unasikia kama yanarudi mdomoni? Ingekuwa vyema ueleze vyema zaidi hali. Umri nk.
Tuwasiliane kwa Bpepe : gmacha52@gmail.com
Thanx for your good articles,i learn something
Nimeipenda sana makala yako hii,nimejifunza sana mambo mengi juu ya Afya.
Hakika nime pata hitaji langu
kaka Macha ni vyema ukaandaa kitabu juu ya ulaji kwa Watanzania kitasaidia sana. hongera kazi nzuri
Si wazo baya Dodi
asante kwa ushauri mzuri, nitafanya hivyo ulivyoelezea pia nitakujulisha mafanikio yangu
ningependa unisaidie tatizo la kutoka jasho mara kwa mara je, husababishwa na nin?
Ninavyoelewa kutokana na uganga wa Kichina tatizo lolote la maji mwilini, jasho, mkojo, machozi nk hutokana na figo.
Labda ungechunguza hasa figo zikoje. Lakini unaweza kupimwa na mganga aliyesomea sayansi ya Kizungu akaona hakuna kitu. Mchina huangalia mzunguko mzima wa maji mwilini ukoje. Hivyo tafiti zaidi kuhusu suala la kazi ya figo. Kazi yake mojawapo kuchuja umajimaji. Ya pili kwa mitaarafu ya Wachina ni kuweka uwiano kati ya ubaridi na joto, uzito na udhaifu, ugumu na ulaini, nk.
Je kuna jambo unalofanya kuzidi kiasi? Je kuna kitu unakula au kunywa au kuzidi kiasi? Jiulize maswali hayo. Huu ni mwanzo.
Mimi nataka kupunguza tumbo,lakini nina operation.Je,ni mazoezi gani yatakuwa salama kwangu na kuniepusha na madhara yanayoweza kujitokeza.
Godwin.
Haya maelezo hayatoshi Godwin. Opereshni gani? Unene na kitambi ni dalili ya tatizo.
INgekuwa miye ningeangalia kula zaidi matunda na mboga mbichi za majani – kwa wingi. Kunywa maji dakika 20 hadi 30 kabla ya kula. Kujaribu kufanya mazoezi ya kuhema na kupumua haraka mara mbili tatu kwa jumla nk
Bro nakushukuru sana kwa maelezo yako .napenda tu kuuliza
ati nasikia kuwa ukinywa maji ya baridi yanateremsha kitambi je ni kweli?
Kunywa maji kijumla husaidia kupunguza unene. Lakini sio na mlo. Kunywa maji nusu saa hivi kabla ya kula.
Pili kwa mtazamo wangu, si vizuri kunywa maji baridi maana ndani ya mwili kuna joto. Miye hunywa maji moto siku zote.
napenda kusema shukrani,kwamakala enu yenye faida nyingi kwa wanadamu haswa vijana mana kutokana napilika nyingi zavijana anazozipitia katika harakati zake za maisha(makazini,ama mavyuoni,shuleni nk) vijana wengi tumekua tukipata wakati mgumu katika kupanga milo bora na sio bora mlo nawengine wetu kuishia kua na maumbo mabaya(haswa kwa wanawake kutoka vitambi nakunenepa sana) vitu vinavotuletea msongo wa mawazo nakutufanya tuingie katika mambo yasiyofaa maoni angu ni makala ako izidi kupanuliwa zaidi haswa iangaziwe kwaupana zaidi masuala ya saikoloji kwa wale walioasilika na matatizo ya unene(maana kunawatu wanajitapisha maisha yao yote kukwepa unene,wengine kupungukiwa damu kukosa nguvu nakuwafanya wenye wasi wasi.Asante.
Nashukuru kwa fikra zako Latifa…ntajitahidi kuandika kupanua zaidi.
Nmependa sana elimu yenu nitaifanyia kazi
Nashukuru kwa Elimu yako
Reblogged this on Muddyb Mwanaharakati and commented:
Mambo ya afya!