VIJANA wengi leo nyumbani Bongo wanapatwa na maradhi ambayo zamani yalikuwa ya wazee au watu wa makamo. Maradhi haya ni kama kisukari na mstuko wa moyo.
Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi …chunguza zaidi.
Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa.
- Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi
- Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic
Jambo la kuangalia ni je?
- Unashikwa kichomi ukiwa unatembea?
- Umeinama au umelala
- Ukishakula chakula
Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo.
Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka.
Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo.
Tatizo jingine ni ulaji wa chakula chenye chumvi nyingi sana. Chumvi inakorofisha pia mzunguko wa damu mwilini.
Hasa kama hunywi maji.
Soma zaidi suala hili hapa:
https://kitoto.wordpress.com/2010/04/13/njia-kumi-kusaidia-kupunguza-unene/
Kama unapatwa kichomi ukiwa umelala au umeinama ina maana kuna tatizo pia la mzunguko wa damu ndani ya moyo au kwenda moyoni. Labda una tatizo la unene (je unafanya mazoezi ya kutosha?) kama unafanya mazoezi, je unafanya mazoezi ya aina gani?
Kuna mazoezi ya aina mbili.
Mazoezi ya nguvu na haraka (cardio vascular); kama kukimbia, mpira, ngumi, kuinua vyuma nk.
Au mazoezi laini yanayofanywa kwa kukihimili (isometric) mathalan ukiweka mkono upande mmoja wa kichwa huku ukisukuma kichwa kisukumane na mkono, unafanya tizi la kuongeza nguvu ya shingo. Zoezi aina hii linaitwa Isometric.
Aina ya mazoezi ya aina hii ni kama Yoga, Pilates na baadhi ya mitindo mbalimbali ya mapigano yaani masho ati mathalan Tai Chi ya Kichina.
Tizi la Yoga zuri sana maana limetulizana:
Tai Chi
Pilates si tofauti sana na Yoga ni kama ndugu wa karibu. Ila Pilates inafafanua zaidi mambo mengine kama tumbo nene:
AinNI muhimu kuchanganya mazoezi haya mawili. Yaani ukishafanya mazoezi ya nguvu, ya kuhema unatulizana.
Kama una kichomi cha mara kwa mara yaweza kuwa ni dalili za ugonjwa wa moyo, kisukari au mambo mengine. Kuondokana na mambo haya:
- Kamwone mganga wa moyo
- Kama huna ugonjwa wa moyo angalia unavyokula. Je, unakula sana vyakula vya mafuta
- Punguza ulaji wa mafuta au vyakula vizito jaribu kula zaidi samaki ambao huwa na mafuta yasiyoumiza mwili.
- VITUNGU SAUMU VIBICHI vinasaidia sana kukinga moyo, matatizo ya mafuta, lakini tatizo ni harumu mbaya ya mdomo. Hivyo unaweza kuwa unachanganya na mboga nyingine za saladi unapokula mlo kila siku. Kama nyanya, matango, nk.
Mbali na ulaji suala la mapumziko ya kutafakari au kwa kimombo Meditation limefanyiwa utafiti na kuonekana kwamba linasaidia sana maradhi ya moyo, akili na “stress” ya mwili kwa ujumla. Jaribu hizi hapa chini, ukiweza dakika kumi hadi 20; mara mbili kwa siku, kufuatana na muda ulio nao.
1.KUKAA TU
2. KUVUTA PUMZI
http://www.youtube.com/watch?v=-j5Z4E2wkh4
3. KULALA CHALI HUKU UNAVUTA NA KUPUMUA…hii ni aina ya masho ati ya Kirusi ambayo inasisitiza Uvutaji pumzi sahihi.
Inaitwa Systema.
Jisomee zaidi habari kuhusu vyakula vinavyouboresha na kuukinga mwili hapa:
http://him.uk.msn.com/health-and-fitness/articles.aspx?cp-documentid=155013085
Asante kwa bonge la SHULE Mkuu!
Kuna mengi ndio kwanza nimestukia kutoka kwenye hii post yako.
Kweli
kiujumla unanifurahisha sana the way unavyoheshimu na kufuata ulaji na kanuni bora za afya kama mwanadamu.excellent!!!
nimefaidika na somo lako,mume wangu ana tatizo la kichomi upande wa kulia chini ya mbavu ya pili kutoka juu,hili tatizo linamtokea mara kwa mara,amejaribu kupima x-ray kuona kama ana vidonda vya tumbo au gesi pia hamna tatizo hilo,daktari amempima kipimo cha damu hajaona tatizo,aliandikiwa dawa za ges but whazikumsaidia,ila mume wangu ana ugonjwa wa pumu jee ni sababu zipi zinaweza kusababisha tatizo hilo?
Unajua Maryam tumbo ni kama stoo au ghala. Tunaweka na kulijaza na vyakula kila mara. Linatakiwa lichunguzwe sana. Kwanza huwa unakula nini na vipi? je Unabugia ? Je unakula chakula na maji au vinywaji vingi?
Kichomi ni kitu kinachoweza kuwa tatizo la moyo au pia wingi wa “acid” katika tumbo. Linaweza kuwa kufanya kazi au mazoezi kuzidi.
Pumu huathiri mapafu na moja ya njia za kuikabili ni kufanya mazoezi yanayosaidia pumzi kama kuogelea, kukimbia mbio za jogging; lakini si kila siku; labda mara mbili kwa juma.
Yoga pia inasaidia. Hebu chunguza unapoishi kama kuna sehemu za kufanya Yoga, hasa kama ni mji mkubwa. Unaweza pia kuwaona waganga wa Kichina ambao wana utaalamu wa “Accupuncture” (sindano zinazoangalia njia za umeme mwilini) ambao husaidia sana pumu na maradhi ya mapafu.
Asante sana kwa bonge la darasa!
Naitwa mtweve tatizo langu tumbo linajaa ges na kuzunguka kitovu linauma kwa kuchomachoma halafu linakuwa LA moto naombeni ushauri wenu
Tumbo kujaa gesi latakiwa kumwona mganga. Upimwe vizuri. Ila kwa mtazamo wangu je unakula vyakula vya aina gani. je unakula sana vyakula vya mafuta. Vinywaji vyenye gesi? je unafanya mazoezi ya viungo? Je una kitambi? Huenda una vidonda tumboni (“ulcer”)…
kichomi kwa kiingereza inaitwa nini
Kichomi ni “cramp” au “sharp burn” au “sharp pain in the chest area”…wapo wanaosema ni “pneumonia” lakini sidhani.
Nimependa
MIMI VICHOMI HUWA KINA NISUMBUA NA HAPACHINI YA KITOVU, UKWELI MIMI HUWA NINA TUMIA SANA DAWA ZAKUTULZA MAUMIVU JINO HUWA LINA NIUMA. LEO NILIMUONA DAKITAR AKANIAMBIA ET NIASID HATA SIKUPIMA NIMETUMIA DAWA NANINASIKIA PO JENISAWA AMA MPAKA NIPIME NDIYO VIZUR? NIKO KENYA
Aisee Asidi ziko za aina nyingi. Je mganga alikueleza ni aina gani? Kuna ile inayosababisha kiungulia, yaani kujisikia “kinamna” au tuseme kuchoma katikati ya tumbo na kifua. Hiyo ni dalili za mwanzo za matatizo ya tumbo; yaani chakula kutoingia tumboni, kutomeng’enywa sawasawa. Hii huweza kusababishwa na mambo mbalimbali lakini yote yanahusiana na namna unavyokula, nini unakula, nk. Moja ya dosari ni nyongo kutofanya shughuli yake vizuri. Je unakula usiku sana? Kawaida unatakiwa ule mlo wa jioni kabla ya saa mbili usiku. Na ukisakula ukae saa tatu kabla ya kwenda kulala. Je ukishakula chakula kingi mara moja unakwenda kulala? Unatakiwa ukishakula usikae tu chini, fanya shughuli, tembea tembea nk.
Asidi ya pili ni ile ya vidonda, ambapo vipo vya aina mbili: inayotokona na utata wa maisha na hisia. Ya pili inayotokana na ulaji. Yaani mtu huli sawasawa- ama unachukua muda mrefu kula na ukila unajaza tumbo(wale wanaokula mlo mmoja mkubwa kwa siku) au unakula vyakula vyenye “viungo” sana mathalan : pilipili, chumvi, binzari, nk kila siku – halafu hunywi maji kwa wingi. Au unakunywa hayo maji na chakula badala ya kuyanywa nyakati tofauti na milo? Maji yanatakiwa yanywewe dakika 20 kabla ya chakula, au nusu saa hadi saa nzima kuendelea baada ya chakula- si na chakula. Hii ni mifano michache. Hebu muulize kwanza mganga ni asidi ya aina gani unayo.
Nitumie barua pepe (kilimanjaro1967@hotmail.com) au jisomee mwenyewe hapa:
http://health.howstuffworks.com/wellness/natural-medicine/home-remedies/home-remedies-for-heartburn.htm
Ili kupata uhakika ni vizuri ukapima kwanza ili ujue tatizo linalokusumbua hii itakusaidia kujua ni dawa gani utumie kutibu ugonjwa wako,jacob wa dar es salaam tanzania
Salaam!
Kweli mnafundisha.
Elimu hii ni nzuri kwani inatusaidia jinsi ya kuishi na kuepuka magonjwa hatari kama ya moyo na n.k
Mimi nina miaka 19 nafanya mazoezi na kazi za kawaida.sina unene ila najisikia kama kichomi kwenye upande wa moyo hasa nikikimbia sana au kubeba kitu kizito sana.naomba unisaidie
Jose….Wataalamu hushauri kabla a kufanya mazoezi yeyote upimwe na mganga kwanza kuhakikisha mwili uko sawa.
Mara nyingi kama hujazoea kufanya mazoezi unapoanza hujisikii vizuri. Unatakiwa uanze pole pole, kwanza uupashe moto mwili. Na je nikuulize huwa unafanya mazoezi hayo saa ngapi, muda gani, mara ngapi kwa juma?
Mimi nina miaka 19 nafanya mazoezi na kazi za kawaida.sina unene ila najisikia kama kichomi kwenye upande wa moyo hasa nikikimbia sana au kubeba kitu kizito sana.naomba unisaidie..
Ahsante doctor
Mimi doctor nasumbuliwa na moyo yaani huu moyo unakaa kama vile unatambaliwa na mdudu yaani kama kuna wadudu wanapita huku wakini tekenya ile sehemu ya juu ya moyo.
Kama nafanya shughul zang wala hainijii lakin kama nimepumzika kwa kulala bac nahic ili jambo linanitokea.naomba ufumbuzi wako doctor.
Aisee Said Yahya…mimi si dokta. Mimi ni mwandishi tu mwenye utambuzi wa mambo fulan fulani kutokana na ar yangu ya kupenda michezo na afya.
Ungewasiliana na mganga akupime vizuri
Elimu hii ni nzuri kwani inatusaidia jinsi ya kuishi na kuepuka magonjwa hatari kama ya moyo na n.k
Helpful,thanx
Ahsante kwa ushauri, kabla ya kuandika maneno haya nilishambuliwa na Kichomi kikali. Baada ya kuzunguka mtandaoni nikakutana na maandishi yako. Sasa nimeelewa vizuri
je ukiwa na kichomi miguun na mikonon mithili ya shoti ya umeme chenye kujirejearejea
Je umewahi kuonana na Daktari? Maana shoti za miguuni na mikononi mara nyingine hutokea kama mtu umekaa sana muda mrefu na mzunguko wa damu umeathirika. Mazoezi kama kuogelea, kukimbia husaidia…. Lakini kama zinatokea tu ghafla bin vuu bila sababu, kapimwe (damu, figo, nk)
MM NNA KICHOMI WAKATI KULIA USAWA WA MOYO WAKATI UPANDE WA KUSHOTO.alafu tumbo langu linajaaga gesi,pombe sinywi ila pilipili na kulaga mfululizo wakati.je?matatizo haya yanaweza kuwa ni moyo?by deo malamla mwakyegula
Ningeomba anuani pepe yako (Email) nikuandikie kirefu zaidi. Unajua hili suala la kichomi inategemea una umri gani, unafanya mazoezi? Mnene au mwembamba…shauri mbali na umbo yategemea kama mzunguko wako wa damu na maji mwilini ukoje.
Ushauri wangu ni huu:
1. Nenda kwa mganga kapimwe moyo. Maana maumivu ya upande wa kushoto (chini ya kikwapa/ bega) huhusiana na moyo. Kama presha na moyo uko sawa basi yatakuwa mambo mengine ya mzunguko. Unajua watu wasiofanya mazoezi huwa na matatizo ya mzunguko wa damu na musuli inajibana bana.
2. Umezungumzia gesi, hili linaweza pia kuwa tatizo la ulaji. Je unakula vyakula vya aina gani. Ndiyo maana ni muhimu kupata zaidi habari. Je unakunywa maji, na kama unakunywa maji unayanywaje? Je unakunywa na chakula au kabla au namna gani…
3. Pili pili kwa wingi si vizuri maana inaipakazi damu na hasa figo na ini. Chochote kinachozidi katika mzunguko wa damu – kiwe pombe, sigara, tangawizi, kahawa, mirungi, pilipili, – hivi ni vitu vinavyoweza kuwa na athari katika umaji maji mzima wa ndani ya mwili. Hivyo yabidi kuweka uwiano. Kwa mfano kunywa zaidi maji, kula vyakula au vitu vinavyowiana na hivyo. Unaweza kula matunda mathalan yakatuliza huo uchachu, au ukafanya mazoezi na kunywa maziwa yakatuliza hayo. Lakini haya mambo yote najisemea tu au kujiandikia tu bila kujua hasa habari zako zaidi. Nijibu maswali mawili matatu niliyokuuliza juu halafu tuchimbe zaidi. Anuani yangu ni kilimanjaro1967@hotmail.com
naomba ushauri,mimi pia nasumbuliwa na vichomi tumboni pande zote kulia na kushoto hii ni wiki ya pili napatwa na hali hii,ila nina tatizo la vdonda tumbo kwa mda mrefu yapata miaka kumi sasa.je nina tatizo gan?
Tatizo lolote la vidonda tumboni latakiwa kutazamwa na Daktari. Nikikueleza nini kufanya bila wewe kuchunguzwa kwanza itakuwa makosa. Nnavyojua tatizo la vidonda tumboni ama husababishwa na ulaji au uvutaji sigara (vyakula vinavyoharibu kuta za tumbo), kutokunywa maji, kula sana chumvi nyingi, kutofanya mazoezi ; pili, hisia na wasiwasi zaweza pia kuchangia. Aina hii ya pili huwakabili watu wenye mawazo mengi na bila kusuluhisha tatizo, huwezi kulitibu.
Ila kama nilivyokusisitiza kapime kwanza kw amganga. Mimi si mganga
Mm Nina kichomi kwenye ziwa upande wa kushoto mazowezi nafanya yoga nafanya ila hutokea Kama kuchomwa Sio mdaa wte na wala sio mdaa ninaofanya mazowezi , nini tatizo gani
Je umekwenda kuangalia hospitali? Waganga wanasemaje?
Je unafanya mazoezi kiasi gani?
1. Je unazidisha muda wa mazoezi? Dakika 40-45 mara tatu kwa juma zinatosha mazoezi. Kwa kuweka mapumziko kati – siku 1-2 kwa juma.
2. Je, umefundishwa sawasawa namna ya kuyafanya haya mazoezi?
3. Je umepima moyo kabla ya kuanza mazoezi?
4. Hiyo Yoga umefundishwa sawasawa au unajifanyia tu
Nafanya mbona yoga nilifundishwa India hasa
Je kichomi kinahusiana na mimba?
Mimba ina masuala mengi ambayo mganga au mkunga husika anaweza kukuelekeza. Kama unapata kichomi au maumivu yeyote wakati una mimba sharti umuulize mganga anayekutazama wakati wa uja uzito.
Nimefurahia sanaa coz nimepata jibu la tatizo
Mimi ni nakichomi sasa kwa mda wa muezi moja na nusu, ina chomea kwenye mngogo katikati wa uti wa mgongo na mwisho wa mkono huchoma ni kihema. sio mara ya kwanza na nime kua na limonia attack mara nyingi. kwanza nikiwa mahali ya baridi ndio inaanza. ama niki oga maji ya baridi ni fanye nini na kwa madakitari si hishi kwenda hata sasa na tumia dawa Augmentin 625mg.
Kama ni jambo linalozunguka mwili mzima yabidi kujua kwanza waganga wanasema nini. Pili, kama baridi ndiyo inasababisha basi yabidi uchunguze kwanini baridi haikupendi. Je una matatizo katika mapafu? Labda una mushkeli katika mapafu basi. Au labda una kitu kinachoitwa “rheumatism” ambacho ni matatizo ya mifupa na viungo kutokana na hali fulani. Dawa ya Augmentin hutumika kwa maradhi ya vidonda ni “antiobatic”…
Ningekushauri ujaribu kufanya USINGAJI. Lakini usifanye usingaji huo na wasingaji wa mitaani. Jaribu wale waliofuzu walioshapitia mitihani na kuwa na vyeti vya bima ya maisha.
Hujanieleza kwanini kichomi kilianza. Je uliumia? Je unaishi mazingira ya aina gani? Jaribu kuniandikia Bpepe.
Unipe maelezo zaidi labda nikuelekeze vitu vya kusoma na kutafiti.
kilimanjaro1967@hotmail.com
jambo bwana,mi nina sumbuliwa na tatizo la kuhumiwa chini ya mbavu mwandani,sijuwi kama ni kichomi ao,uwa unikosesho raa sana,unaweza kunisaidia?nifanye je ili tatizo ili liishe,na stomach nayo inanisumbuwa,nisahidie pls.
Maumivu yeyote kwenye sehemu ya kiwiliwili (tumbo, mbavu, nk) yanatakiwa kuangaliwa na daktari.
Ila kwa maoni yangu yabidi upimwe kuangalia moyo, mapafu, …je ujiulize wewe mnene? Je huwa unafanya mazoezi ya “stretching” ?
je unavutaje hewa? je wewe ni mvuta sigara? Je kwenu kuna historia ya maradhi ya aina gani?
Watanzania wengi hatuna desturi zifuatazo hivyo tunakumbwa na mambo ya ajabu ajabu
1. Kuangalia tunavyokula
2. Kutofanya mazoezi ya viungo
3. Kutokunywa maji (bilauri 6-8 kwa siku)
4. Kutokwenda kwa mganga kupimwa hata kama huumwi, mara moja kwa mwaka. Kuangalia moyo, mapafu, damu, nk
Ninashukuru Sana Admin Kwa Kuweka Maelezo Mazuri Ahsante Sana!
habari,jamani mimi ninaumwa kweli! maradhi mengi yananisumbua yani mpaka nashindwa kuelewa kipi ni kipi. kwa kuanza kabisa kichwa kinaniuma sana. kisogoni. kuna mda nasikia hadi kuanguka au kuzimia nimeshenda hospital karibia zote dodoma naishia kupewa dawa lakini tatizo haliishi. nlishapima presha,damu na sukari hamna tatizo. nimewahi kujigonga vibaya sana kisogoni sa sijui iyo inaweza kuwa sababu? pili,nina maumivu makali sana upande wa kulia kwa chini huu mwaka wa tano sasa, nshapima vipimo vingi sana naambiwa tatizo hakuna, tatu, kifua nacho kinauma sana had mgongoni,taya, shingo,mkono wa kushoto na mguu, pia mkono wa kulia unaishiwa nguvu kabsa na misuli ya mguu wa kushoto inauma na kukaza mpaka nashindwa kukanyaga. sijui tatizo nini?
Duuu. Bahati mbaya huu si ukumbi wa daktari. Kwahiyo hatuwezi kutoa maoni ukasema kweli hii ndiyo dawa. Tunachoweza kusema ni kuchangia maswali ya wewe kujiuliza.
1. Je una umri gani na haya mambo yalianzaje? Kama unasema ulianguka ukagonga kisogo. Je kichwa kilipimwa ulipoanguka? Maana nilivyoelewa mimi kuna tatizo la mzunguko mzima wa mwili, mifupa, mishipa na mishipa ya fahamu.
2. Ningependekeza kuwaona wataalamu wanaoangalia afya ya jumla … hawa ni watu kama Psychotherapist yaani mtu anayeangalia mwili ulivyo. Si kwa ndani bali musuli, mishipa na ngozi. Ingekuwa mimi ningeulizia katika vyuo vikuu vya Uganga au ningeangalia sehemu gani Tanzania ina psychotherapist. Au mtu anayeangalia maradhi yanayotokana na ajali za mwili au hata “trauma”…
3. Fanya utafiti katika mitandao. Ndivyo watu wengi wanavyofanya. Bofya You tube,Google na kadhalika uorodheshe aina ya mambo yanayokusumbua. Mathalan nimebofya neno “head injury trauma”…nikakuta misururu ya maelezo.
4. Jaribu kutafuta waganga wa Accupuncture. Nasikia Dodoma wapo. Wachina na Wajapani. Ubaya wapo wanaotapeli, hivyo itakuwa vigumu kujua yupi wa kweli au uongo. Ila ni vizuri kuulizia na kufanya tiba hiyo maana inatathmini mwili mzima.
5. Je unafanya mazoezi ya viungo? Maana watu msiofanya mazoezi mkiumia kidogo huwa mwili mzima unaharibika. Baadhi ya mazoezi unayoweza kuangalia ni kama Yoga na hata Usingaji.
Sijui kama haya mawazo yanasaidia. Ukweli tatizo lako linahitaji mtaalamu hakika. Hizi ni fikra tu za juu juu.
MAMBO?ILA SAMAHAN KAMA NITAKUWA NJE YA UTARATIBU WAKO.Mm ni mfanya mazoezi ya taichi na maditation ila kama ujuavyo bongo yetu hakuna mwamko nahitaji kuwasaidia watu kwa kufanya mazoez hayo je kuna kikundi chochote unafaham kinadeal na mazoez ya taichi,hata kama wewe unawatu mnaofanya nao mazoez ya tiba nifahamishe ndugu 0753155171
Kweli kabisa maneno yako, Athumani.
Tuwasiliane kwa Bpepe Athumani. Niandikie
kilimanjaro1967@hotmail.com
asante sanaa maana baada kuskia maumivu kwa muda mrefu na kugoogle hatimae nimepata jibu na nimekua na amani
Nina rafiki yangu huwa anasumbuliwa na moyo, kuna wakati anajisikia tu moyo unakwenda mbio na anakuwa anashtuka hadi inafikia wakati hapati usingizi wakati wa usiku, amejaribu kwenda hospital lakini tatizo bado, je atakuwa anasumbuliwa na nini?
Kama amekwenda hospitali na waganga hawakumsaidia itabidi tu atafiti mwenyewe.
Tatizo hili ninavyojua linaitwa Arrhythmia…
Hebu some zaidi hapa
http://www.nhs.uk/conditions/arrhythmia/Pages/arrhythmia.aspx
Kichomi changu ni chini ya moyo upande wa kulia katikati ya mbavu naomba msaada kutoka kwako…………Gabrielpaul625@gmail.com
haya mambo ya vichomi yatakiwa kuangaliwa na madaktari…ukibabaisha huku mitandaoni haitoshi.
Labda jisomee zaidi…lakini kamwone mganga. Huwa dalili za kitu fulani hasa kama ikizidi sana…
Maana yake
https://en.wikipedia.org/wiki/Heartburn
Dalili za jambo gani?
http://www.nhs.uk/Conditions/Gastroesophageal-reflux-disease/Pages/Introduction.aspx
Nina matatizo ya vichomi kwene mapafu, ways down nifanyeje tabibu
Kapimwe maana kichomi ni dalili ya jambo fulani…
ASANTE SANA KWA USHAURI
Nafurahi sana maana nimejifunza mengi kuptia kwako Dr.
Ahsante sana. Lakini. Mi sio dokta ni mtafiti tu nnayejali afya.