Arusi za Waafrika Majuu huwa zina ugumu na urahisi wake.
Ugumu?
Mwafrika kuwa mbali na jamii na jamaa zake; akibahatika kupata wahudhuriaji wachache basi humshukuru Mungu. Ugenini ni ugenini tu…
Urahisi?
Ile furaha isiyopatikana kirahisi kutokana na kuishi ughaibuni kama mgeni, huvimba, ikanepa na kuringa : raha ya kufanya kitendo maalum.
Karibuni nimehudhuria arusi mbili kem kem. Mosi, ya dada [...]
Archive for the ‘Blogroll’ Category
ARUSI MAJUU…
Posted in Uncategorized, tagged Arusi, Kenya, London, Maisha, Tom Chiwalala, Ughaibuni, Ujerumani on September 19, 2009 | 1 Comment »
MPYA ZA MUZIKI UGHAIBUNI
Posted in Uncategorized, tagged Nasibu Mwanukuzi, Norway, Olso, Ras Nas, Reggae, Swahili Music, Tanzania on September 16, 2009 | Leave a Comment »
RAS NAS ZIARANI NORWAY 2009
Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya rege na muziki wa dansi mwenye makao Oslo, Norway, Ras Nas ( Nasibu Mwanukuzi), anapanga safu kali kwa ajili ya ziara ya miji sita Norway. Ziara hiyo itakayoanza Kongsberg tarehe 23 Oktoba itamalizikia jijini Trondheim 7 Desemba.
Kikosi cha Ras Nas kinachanganya wanamuziki toka Congo Brazzaville, Ivory [...]
MJADALA WA MJENGWA KUHUSU “UTANZANIA”
Posted in Uncategorized, tagged Bongoland, Identity, Kiingereza, Kiswahili, Kujitambua, Kujitegemea, Kwanza Jamii, Language, Lugha, Maggid Mjengwa, Tanzania, Utamaduni, Wee Nani on September 16, 2009 | Leave a Comment »
Mjadala aliopopoa Maggid ” Mwenyekiti” Mjengwa (pichani, kulia, alipohudhuria semina zangu, Dar, Mei) blogu ya Kwanza Jamii umezua maoni kem kem. Ni mjadala muhimu kwa sababu kadhaa:
1-Zamani Mwalimu Nyerere alisisitiza sana juu ya utaifa ndiyo maana akashauri sote tuongee Kiswahili. Hii imechangia sana kutokuwa na kero za ukabila Tanzania kama zilivyo nchi nyingi bara Afrika. [...]
Wimbo wa “Dar es Salaam” unaotingisha Majuu (Skandinavia)
Posted in Uncategorized, tagged Tanzania, Dar es Salaam, Swahili, Bongoland, Ras Nas, Nasibu Mwanukuzi, East African musicians, Norway, Oslo, Dagsavisen, Sayari, Music, Scandinavia, Kongoi Productions on August 28, 2009 | Leave a Comment »
Nasibu Mwanukuzi au anavyojulikana kwa jina la kisanii, Ras Nas…katoka na kibao ambacho pia ni jina la Albam yake ya pili kinachoutukuza na kuughani mji wa Dar es Salaam karibuni.
Moja ya magazeti makubwa nchini humo: Dagsavisen liliipa albam hiyo nyota tano. Nyota tano si mchezo kwa mwanamuziki wa Kiafrika anayetumbuiza Uzunguni.
Niliwahi kufanya kazi na Nasibu Mwanukuzi [...]
SEMINA MBALIMBALI DAR ES SALAAM, MEI 2009
Posted in Uncategorized, tagged Afya, British Council, Elimu, Freddy Macha, Health and Fitness, Lucky magazine, Mazoezi, Mwandege Boys Sec School, Nyumba Ya Sanaa, Soma Cafe, Tanzania, Tanzania Youth Alliance-Tayoa, Warsha, Yoga on June 5, 2009 | 2 Comments »
Zoezi maalum la kusaidia mabega kutokana na kazi mbalimbali zinazoathiri migongo, shingo na kichwa. Kuning’iniza bega moja ukizungusha mkono pande zote, huku mkono mwingine umeshika kiti au meza.
Semina zilitayarishwa na jarida la LUCKY linaloendeshwa kwa ushirikiano wa wananchi wanaojitolea mhanga kuelemisha na kuendeleza jamii ya Tanzania. Waliosimamia kazi hii ni Innocent Swai na mhariri wake [...]
BONGO YA KUUGUZA NA KUKUTIBU…
Posted in Uncategorized, tagged Bongoland, Dar es Salaam, Issa Michuzi, Lucky magazine, Nyumba Ya Sanaa, Tanzania, Tiba on June 3, 2009 | Leave a Comment »
Karibuni nimeingia tena Bongo baada ya miaka miwili. Ama kweli kwa tunaoishi ughaibuni kurudi nyumbani ni kama kwenda hospitali. Kabla ya tiba lakini, shurti kuujua ugonjwa.
Tiba ya kwanza utani, masihara na vicheko. Hapa tuko Nyumba ya Sanaa (iliyofunguliwa na Mwalimu Nyerere mwaka 1983); leo imegeuzwa Jumba La Kila Kitu : baa, kamari, michezo, hoteli, mahali pa watalii kununua vito vya Tanzania, makutano kwa [...]
MJUE MHAMASISHAJI- Innocent Swai na jarida la LUCKY
Posted in Uncategorized, tagged Dar es Salaam, Education, Elimu, Innocent Swai, Kiswahili, Lucky magazine, Maendeleo, Tanzania on April 30, 2009 | 2 Comments »
“ELIMU HAINA MWISHO…”
Methali ya Kiswahili
Nchi yetu ina utata.
Mheshimiwa Rais kachorwa vibaya mitandaoni; miezi kadhaa iliyopita akazomewa ilhali kachaguliwa kwa asilimia 80 ya kura; Rais wa zamani, bwana Mwinyi akapigwa kofi hadharani; ajali za mabasi zimezidi,uvutaji bangi (hasa miongoni mwa vijana) umefikia asilimia 90 sehemu fulani fulani; viongozi mafisadi mahakamani; utovu wa nidhamu unaiandama nchi [...]