Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Fasihi’

Said Ahmed Mohammed keshatoa zaidi ya vitabu  30 – Riwaya 11 (ikiwepo” Asali Chungu” kigongo chake cha kwanza kilichomwagika uwanjani mwaka 1976), Tamthiliya 7, mikusanyiko minne ya Ushairi na mikusanyiko Saba ya Hadithi fupi ambayo moja wapo ni “Kiti cha Moyoni” alichochangia na Ken Walibora na “Damu Nyeusi” (pia  na Ken Walibora) kikatoka 2007. Mbali na vitabu, Profesa Said ambaye ni mhadhiri wa lugha za Kiafrika chuo kikuu cha Bayreuth, Ujerumani(toka 1997) na keshachapa vitabu vingi vya watoto wa shule za msingi ambavyo lengo lake kufundisha, kutukuza na kujenga lugha na fasihi ya Kiswahili.

Baadhi ya vitabu vyake Profesa Said Ahmed Mohammed – vyote vimechapishwa Kenya.
(more…)

Read Full Post »

Mahojiano na mtaalamu, mtafiti na mwandishi wa Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!  Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia

Dk. Harith Ghassany ni mwandishi wa kitabu kinachoongelewa Tanzania nzima sasa hivi na huenda kikavuka mipaka na kuingia nchi nane zinazopakana na Jamhuri ya Muungano. Kitabu hiki chenye kurasa 500, kinazungumzia namna gani Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yalipikwa Dar es Salaam, Algeria  na mashamba ya mkonge ya Tanga na kupakuliwa Zanzibar. (more…)

Read Full Post »

TAREHE 29 OKTOBA, 2010….

Kuunganisha  chuo cha  SOAS na jumuiya ya Wazungumzaji  KISWAHILI Uingereza…

‘Milima haikutani, bali wanadamu hukutana’

Sherehe itafanywa  wapi?

Chumba cha  G50,   SOAS, Russell Square,

Thornhaugh Str.

London WC1H OXG

Saa moja jioni – MBili na nusu usiku. Kiingilio BURE. Karibuni

FAROUK TOPAN, mhadhiri wa KIswahili atafungua dimba la  SWAHILI SOCIETY. Uzinduzi utatangaza rasmi tovuti ya Kiswahili:

www.swahilisociety.com

SHEIKH MBARAK  ataongelea kuhusu ” Maisha ya Kiswahili  Nje ya Afrika, mjini London.”

FREDDY MACHA atawasilisha mada kuhusu ‘ Mzizimo wa Jumuiya ya Kiswahili Mtandaoni”‘

SOKO,  wauzaji wa mavazi ya Kitanzania , wataonyesha walicho nacho.

Mgawaha wa  KILIMANJARO utauza Chakula cha  Kiswahili

Mwishowe bendi ya  KITOTO,  itatumbuiza   ukumbi wa JCR  kuanzia saa tatu usiku.

Mtangazaji na mwanahabari, Ayoub Mzee  toka Swahili Diaries SKY news, atawakilisha habari hizi!

KARIBUNI!!!

Habari zaidi ongea na Jason Tuff  (pichani chini) akiwa Mdawi, Kilimanjaro, alikokuwa akifanya mazoezi ya Kiswahili…


Jason ni mmoja wa Waingereza wanaopigania hadhi ya Kiswahili nje ya Bongo na mchangiaji wa klabu hii mpya ya Waswahili SOAS.

Simu…. +44-7816-642296

Barua pepe : 212894@soas.ac.uk

Read Full Post »

Picha mbili toka Shule iliyotujenga kitabia ya Mzumbe,  mwaka 1973-74.

Ya kwanza  jioni moja kabla ya jua kutua mwaka 1974.  Kilikuwa kikundi cha mabondia. Kawaida shule za kulala za sekondari huwa na uchaguzi ambao enzi hizo tuliziita kwa Kizungu “hobby” ina maana burudani baada ya kazi au masomo.  Husaidia wewe kijana kusahau masomo magumu, kujifunza kitu chochote kinachokuongezea nidhamu na bidii ya elimu na kujiendeleza. Kitaifa miaka ya Sabini mwito uliopigiwa kelele na   TANU chini ya  Mwalimu Nyerere ulikuwa Elimu ya Ujamaa na Kujitegemea. ..

Toka kushoto aliyenyoosha ngumi ni kijana aliyekuja kuwa msomi, mwanafikra, mwandishi wa vitabu (mathalan, Makuadi wa Soko Huria, E & D Limited, 2002) na mhadhiri maarufu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Chachage S. Chachage.

Enzi hizo tulimwita Seti. Alikuwa mchangamfu na alipendwa hadi alipokuja kuwa mtaalamu maarufu wa mambo ya elimu jamii nchini. Leo anakumbukwa kwa jina la Profesa Chachage. Alifariki mwaka 2006. (more…)

Read Full Post »

 

Sinema mpya ya Bongoland -2 iliyotengenezwa na Kibira Films imefananishwa na kazi za marehemu Sembene Ousmane(pichani juu). Je wangapi wanamkumbuka mzee huyu aliyefariki mwaka jana akiwa na miaka 84? Nikiwa shule sekondari tulimsoma. Aliheshimika kama mwandishi aliyetukuza maslahi ya wachapakazi, makuli, wavuvi, wafanya kazi na wakulima. Alipinga ukoloni, ingawa alishapigana vita vikuu vya pili, kama askari manamba wa Ufaransa. Alitonesha donda ndugu la viongozi walafi , wafisadi, muflis na wazembe wa Kiafrika. Mzee aliyeishi na anayefaa kuigwa na kusomwa na kukuelemisha.
Vitafute vitabu vyake maktaba …
Soma mathalan, “Gods Bits of Wood” kitabu cha kipekee.
Kitabu barabara. Alipata tuzo nyingi sana.
Baada ya kuchapa maandishi, akagundua kumbe walalahoi wengi Afrika si wasomi wa vitabu. Akaamua sasa atengeneze sinema. Moja ya sinema zake maarufu ni “Xala” (tamka Shala) inayozungumzia Afrika leo na uzandiki wake. Ousmane Senegal (mzawa wa Senegal) alikuwa mwasisi wa sinema na vitabu vyenye ujumbe mkali wa kimaendeleo  Afrika miaka 40 iliyopita.

Ikiwa sinema mpya ya Kibira Films, imelinganishwa na kazi za Ousmane Sembene, basi Watanzania tunao wasanii na wataalamu wanaokanyaga, wakitembea kuelekea kuzuri.

Read Full Post »

Kila siku Wabongo mbalimbali wanaingia mitamboni. Lakini waandishi wa kizazi  cha kale, cha kijadi, wataalamu waliotopea katika kalamu, fasihi, mawazo na falsafa, ni wachache wanaojivuta na Mablogu. Mmoja wa Wataalamu na Wasomi wa Tanzania wanaofundisha na wanaostahili kusikilizwa ni Ndugu  Joseph Mbele anayefundisha katika vyuo mbalimbali vya Marekani. Ninamfahamu na kumsoma Joseph Mbele toka akisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka ya  Sabini. Ni mwandishi na mjuzi stadi wa fasihi ya Afrika na hasa ya Kitanzania.

 Hebu yacheki mawazo yake na sikosei kusema kutakuwa na moja au mawili ya kujifunza toka kwake.

http://josephmbele.blogspot.com/

Read Full Post »

adam-shafi.jpg

Nimepokea simu. Simu ya maana. Adam Shafi yuko Majuu. Kaja kikazi Uholanzi. Yeye mtaalamu wa lugha ya Kiswahili. Baada ya kumaliza kapitia Uingereza katika mji mmoja wenye wakazi wengi wa Kitanzania, yaani Milton Keynes. Ni wastani wa saa moja kwa treni toka London.  Mrefu, mchangamfu, mzungumzaji aliyesheheni “mastore” kibao. Nishakutana na waandishi wa kila sampuli. Wanaojificha: wakimya, wasioongea sana, wapole wanaokaa chumbani kati kati ya watu ukadhani hawapo. Wanaopiga kelele, wakijafaragua; ama wenye aibu…
Shafi ni mtu wa kawaida kabisa, naweza kuiita hulka, tabia na namna yake “Mfurahia Maisha” : kachangamkia  uhai, haswa. Kaishi, anaishi…hamalizi. Kila mara atasema ana mikakati ya kufanya jambo fulani, kuandika kitabu kingine kipya, kuendeleza fasihi na Kiswahili….
(more…)

Read Full Post »

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 355 other followers