Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Gloria Nanvuma’

Picha na Urban Pulse Creative Media
Video za simu na Malkia Kassu

Jumapili Machi 30, 2014; ulifanyika mkutano wa Watanzania kuangalia masuala ya bima ya maisha, na pia kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete kuwahutubia wananchi.
Kitoto ngoma live- 2014- pic by Frank BZ
Wana Kitoto…tukitandika Ngoma iitwayo “Djembe”…AFRIKA OYEEE!

Wakati huu watayarishaji (kinyume na miaka mingine) walijitahidi kuweka sanaa za maonyesho za Wazalendo wakazi, Uingereza. Uimbaji wa Francis Chengula (Mtunzi wa wimbo “Nakupenda Tanzania”) na shairi la Ustaadh Khamis Juma- mbele ya Rais viliburudisha ukumbi wa Sattavis Patidar Centre, Wembley, kaskazini magharibi ya London.
Wengine tulikuwa sisi wapigaji ngoma wa Kitoto Band. Tunapenda kujivunia ngoma asili za kikwetu maana zinasahaulika. NGOMA ndiyo uti wa mgongo na roho ya muziki wote wa kisasa (pop music) duniani leo…!

Ngoma zilidundwa na Gwang (mzawa wa Grenada), Paolo Forcelatti (Italia) na mdau wa Kitoto hapa katika blog. Wachezaji wawili walikuwa Herieth Ngatunga (Tanzania) na Gloria Nanvuma (Uganda).

(more…)

Read Full Post »