Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Afrika Jambo’

 

Ukumbi wa The Eastern District Social Club, Northampton haujulikani kwa wengi. Hata hivyo eneo hili nje kidogo ya mji, ulijikuta ukikaanga Maandazi , Vitumbua na Nyama Choma punde Wasanii mseto wa Kitanzania walipozindua WASATU – jumuiya ya kuwakutanisha na kuwaunganisha. Ilikuwa Jumamosi 1 April, 2017.
Wimbo maarufu wa Les Wa Nyika, SINA MAKOSA, uliotungwa na Omari Shaaban, kuimbwa na Issa Juma na kupambwa gitaa maridadi la John Ngereza, ulikuwa kati ya vibao mbalimbali vya Kiswahili vilivyotukumbusha tukokako, na tu wapi, duniani. Umoja ni nguvu. Kiswahili oyee! Tanzania Oyee! Afrika Mashariki na Kati oyee!

Advertisements

Read Full Post »

Soma Cafe- Africa Day 2013
Fikra za Umoja wa Waafika zilianza kuzungumziwa na kuchipuka kupitia Marcus Garvey- mwanarahakati wa Kijamaika aliyewasisimua viogozi wa mwanzo wa bara, miaka ya 1920 na 1930 . Garvey huzungumziwa sana katika Muziki wa reggae wa akina Bob Marley, Peter Tosh na Bunny Wailer. Alifariki na kuzikwa London mwaka 1940.
Marcus Garvey
Marcus Garvey
Lengo lake mwandishi na mpiganaji huyu lilikua kuwaunganisha weusi wote duniani na kutupa moyo wa kujipenda na kutoogopa asilia yetu.
(more…)

Read Full Post »

Fab Moses  na gitaa  nyumbani kwake anapotunga nyimbo mbalimbali za Kiswahili, London. (picha na Freddy Macha, 2009)

Fundi  na mfanya biashara wa Kiganda, John Kizito mwenye kampuni ya kutengeneza magari, Bingol Engineering Company, (kusini mwa London) ni kati ya mashabiki wa  mwanamuziki Mtanzania anayewika hapa Uingereza karibuni.

“Fab Moses ananikumbusha wananamuziki wa Kiswahili wa zamani. Hapigi makelele wala hachanganyi matusi na maneno ya Kiingereza. Tena kajaaliwa sauti nzuri sana.”

Huyu Kizito ndiye babake aliyekuwa mrembo wa Uganda mwaka jana yaani Maria Namiiro.

http://www.ugpulse.com/articles/daily/Beauty.asp?about=Maria+Namiiro+is+Miss+Uganda+UK+2009&id=1102

Sifa alizozitosa John Kizito hazikuishia maneno matupu.  Maana mkono mtupu haulambwi. Alichangia gharama za CD ya kwanza ya Mbongo mwenzetu mwenye sauti inayokumbusha akina Marijani, Simba wa Nyika,  Sikinde, Mbaraka Mwinshehe na Tabora Jazz, wana Segere Matata.

Shoo ya kwanza ya Fab Moses  ilifanyika Ijumaa iliyopita, mjini Brighton, ukumbi wa Salsa Lounge ukingoni mwa bahari ya English Channel, hapa Uingereza.

Dhana yake iliyonyooka ni moja.

Inaitwa Nengua: mtindo wa kucheza (kukata kiuno na kujilegeza), CD na hata bendi.

Nengua ilikuwa na wanamuziki wakubwa stadi mbalimbali toka Kenya, Uganda na Tanzania. Toka Kenya, Ben Adolwa (mpiga Sax) kawahi kupiga na mtunzi maarufu wa wimbo wa “Malaika” (marehemu Fadhil William) na Billy Mwangura mpiga besi, mzawa wa Mombasa. Kongo wapo Mille Baguette (kawahi kufanya kazi na zee la jazz toka Cameroon, Manu Di Bango), Ladi Mbala na mpiga gitaa anayestawisha klabu za Waafrika London, Burkina Faso.

Toka Bongo wana Nengua wengine ni Jenny Kimali Harris (sauti ya kuitikia ) na Saidi Kanda (aliyetwaa tuzo la kimataifa la WOMAD la mpiga ngoma wa mwaka 1989). Kanda ambaye anavipaji lukuki : kuimba, gitaa, vyombo vya ala za kijadi mathalan zeze na marimba ni pia fundi mitambo. Alichangia sana katika kuitoa CD hii ya Nengua.

Tazama vitu vyake Mbongo mwenzetu anayetutia sifa Waafrika:

http://saidikanda.com/

Fab Moses ambaye hujulikana zaidi kama mcheza sarakasi na ngoma za kiasili kawahi kutoa CD nyingine akiwa na wanamuziki wa mseto wa bendi ya No Tchuna Cha (siku hizi Afrika Jambo) inayooongozwa na gwiji Kawele Mutimanwa na mwanamuziki wa zamani wa Simba wa Nyika, Rama Sax, toka Tanga, mwaka 1999.

Mwangalie Fab Moses akiimba hapa:

http://vids.myspace.com/index.cfm?fuseaction=vids.individual&videoid=42998197

Je unaitaka CD ya Nengua?

Ongea na Kizito +44-7939-112536

Au  Fab Moses : +44-7950-604530

Read Full Post »

 

fab-moses-pic by f macha

Si wanamuziki wengi wanaoishi ughaibuni toka Bongo.  Miaka mingi hata hivyo  amekuwepo mtunzi na mwimbaji, Fab Moses ,  CD na shoo yake inayoitwa NENGUA.

Mtazame katika tovuti  ya My Space:

http://vids.myspace.com/index.cfm?fuseaction=vids.individual&VideoID=42998197

Mbali na nyimbo zake mathalani: “Ngunguri Ngangari” na “Nyerere” , Fab Moses huonekana katika majukwaa kadhaa ya London akitungua nyimbo mbalimbali za Kiswahili na bendi mashuhuri ya Afrika Jambo.  Bendi hii inasimamiwa na magwiji Kawele “Finger Printer”Mutimanwa, mpiga gitaa mashuhuri wa Kikongo, Uingereza na Ramadhani Athumani Mtunguja (“Rama Sax”) mpiga saxafoni mzawa wa Tanga aliyekuwa zamani na Simba wa Nyika na Les Wanyika na kushikiri katika kibao maarufu Sina Makosa kilichotolewa Nairobi mwaka, 1978. Afrika  Jambo hutumbuiza klabu kadhaa mashariki ya London zikiwemo (East Side Bar, Ilford) Kila Jumapili na Railway Tavern klabu ya Waganda, Forest Gate.

Waliomsikia Fab Moses huvutiwa na uzuri wa sauti yake inayokumbusha vibao mbalimbali vya nyumbani kama nyimbo za Shabani Marijani (Georgina), Simba wa Nyika, Mlimani Park, nk. Moja ya Sifa anazopewa Fab Moses ni sauti inayolandana sana na ya mwanasokomoko, hayati Marijani.

Mwanamuziki Fab Moses ni vile vile mwanasarakasi wa siku nyingi aliyeshafanya kazi na vikundi kadhaa nyumbani ikiwepo Muungano (cha Mzee Nobert Chenga) na Black Eagles. Kwa takribani miaka minane sasa anaongoza kikundi chake cha sarakasi na michezo jukwaani kinachoitwa Highflyers. Walioshamshuhudia (nikiwemo) wanakubali Fab Moses ni  mwalimu na kocha mzuri sana wa Sarakasi. Chini ya utaalamu wake mtu yeyote (watoto kwa wazima) anaweza kufundishwa kujinyonga nyonga na kuwa mwanasarakasi. Hilo latokana na uvumulivu na ufundi wake, Mtanzania huyu mwenye vipaji vingi…

fab-moses-singing

Habari zaidi za NENGUA, kikundi cha Sarakasi (Highflyers) au Afrika Jambo; mpigie Fab Moses -+44-7950-604530

Barua pepe: fabrahs@yahoo.co.uk

Picha na Freddy Macha

Read Full Post »