Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘David Brewin’

PICHA ZOTE ZIMEPIGWA NA URBAN PULSE

Balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania, Mheshimiwa Dianna Melrose ameeleza furaha yake kuteuliwa kufanya kazi nchini kwetu na kukiri kwamba anauchangamkia wadhifa huo atakaouanza karibuni.
Balozi Melrose alikuwa akiongea katika sherehe ya chakula cha jioni iliyofanywa kwa heshima yake nyumbani kwa Balozi wetu wa Uingereza mheshimiwa Peter Kallaghe na mkewe Joyce Kallaghe jijini London Alhamisi iliyopita.
4-Mh Balozi Dianna Melrose akitia saini  kitabu cha wageni. Kushoto ni Mama Balozi Kallaghe
Balozi Dianna Melrose akitia saini kitabu cha wageni. Kushoto ni Mama Balozi Joyce Kallaghe

“Nimebahatika sana.” Alikiri Mama Melrose. “ Watanzania ambao nimekutana nao wana hulka ya kirafiki na uungwana sana. Ni watu wenye tabia njema na ninahisi nitafurahia sana maisha yangu kwenu. Nitafurahia kwa sababu wenzangu walioshaishi Tanzania muda mrefu wamebakia na mapenzi makubwa ambayo sijayaona kwa Waingereza walioishi nchi nyingine. Wamebakia na kumbukumbu nzuri na mahusiano ya muda mrefu na Tanzania.”

3-Mh Balozi Dianna Melrose akisema machache
Mheshimiwa Balozi Dianna Melrose akiongelea machache. Kushoto kwake ni Balozi wetu Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe

(more…)

Read Full Post »