Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Fab Moses’

PICHA NA HABARI 

Za Freddy Macha

3-bango la WASATU

Jumuiya ya Wasanii Watanzania Uingereza (WASATU)  ilichemsha supu, ukumbi wa Heartlands , Birmingham, Uingereza Jumamosi iliyopita. Makutano haya yalikuwa pia sehemu ya mchango mahususi kusaidia wasichana wanaopewa mimba kabla ya kuwa watu wazima, vijijini,  Arusha. Fedha zilikusanywa na mjasiria mali mkazi wa Birmingham, Mtanzania Sia Travel. Sia alijaa mlangoni akihakikisha kila senti iiliyolipwa na wahudhuriaji watashiba chakula ,  sanaa  usiku kucha na kuwafariji vigoli wetu, Tengeru.
(more…)

Advertisements

Read Full Post »

 

Sarakasi ni kati ya sanaa hatari na za kusisimua sana. Kwa sasa Ulaya wapo vijana na watu wa makamo mbalimbali waliohamia toka Afrika Mashariki (hasa Kenya na Tanzania) wakitumbuiza kadamnasi kwa sarakasi, Uingereza, Ureno,  Ujerumani na Hispania.

Nchini Hispania kuna visiwa vya Grand Canary ambapo Watanzania wachache huruka ruka kuvutia maelfu ya watalii.

Moja yake ni Lanzarote. Hapa  Mtanzania Mohammed Idi Mohamed aliyehamia  baada ya kuishi Ujerumani kwa kipindi. Mohdy, Muddy au Modi (wanavyomjua wengi) aliwahi pia kufanya kazi Tanzania, Ureno na Uingereza.

Alifariki Jumatatu 18 Septemba, 2017, asubuhi. (more…)

Read Full Post »

 

Ukumbi wa The Eastern District Social Club, Northampton haujulikani kwa wengi. Hata hivyo eneo hili nje kidogo ya mji, ulijikuta ukikaanga Maandazi , Vitumbua na Nyama Choma punde Wasanii mseto wa Kitanzania walipozindua WASATU – jumuiya ya kuwakutanisha na kuwaunganisha. Ilikuwa Jumamosi 1 April, 2017.
Wimbo maarufu wa Les Wa Nyika, SINA MAKOSA, uliotungwa na Omari Shaaban, kuimbwa na Issa Juma na kupambwa gitaa maridadi la John Ngereza, ulikuwa kati ya vibao mbalimbali vya Kiswahili vilivyotukumbusha tukokako, na tu wapi, duniani. Umoja ni nguvu. Kiswahili oyee! Tanzania Oyee! Afrika Mashariki na Kati oyee!

Read Full Post »

fab-moses-a-r-migiro-na-saidi-kanda-pic-by-f-macha-2016

Mcheza  Sarakasi na mwanamuziki Fab Moses na mwenzake mwana muziki nguli Saidi Kanda wakiwa na Mheshimiwa Balozi, Asha Rose Migiro baada ya kikao cha Jumatano iliyopita London.

Wasanii wanane waligonga milango ya Bond Street. Ikafunguliwa. Wakakaribishwa. Msaidizi wake mheshimiwa akawataka kukaa. Kaeni. Bw Allen Kuzilwa huyo.. Juu  ghorofa ya kwanza. (more…)

Read Full Post »

This slideshow requires JavaScript.

Maadhimisho ya miaka 40 ya urafiki kati ya Uingereza na Tanzania (BTS) yalifanyika mjini Reading, Jumapili 8 Novemba 2015. Wanamuziki watatu wa Kitanzania walialikwa kutumbuiza kwa mseto wa midundo ya kijadi na kisasa : Chakacha, Ilimba, Rumba na ngoma maarufu ya mkoa wa pwani iitwayo BUTI.
(more…)

Read Full Post »

Kitoto ni ngoma ya Kusini, Tanzania. Kitoto kwangu ni mashangilizi ya ngoma na utamaduni wa Mwafrika.
Hizi ni baadhi ya shughuli ambazo mwana Kitoto hufanya ughaibuni. Usiku na mchana. Ninazionea fahari…

Miaka mingi wengi wameniuliza watakujaje Majuu. Njia nzuri na rahisi sana ni kufanya mambo ya kwetu. Ngoma ni kitu kinachopendwa na wageni maana ni uhalisia na asili ya Mwafrika.

Juu hapa wanaonekana wanamuziki wawili wa Kitanzania wanaoishi Uingereza. Saidi Kanda na Fab Moses. Fab Moses hucheza sarakasi, huimba na kucheza ngoma. Mpiga ngoma maarufu aliyekuwa zamani na Remmy Ongala, Saidi Kanda kashika marimba. Marimba ya Kitanzania ndiyo. Vitu vyetu hivyo.

Kitoto tunapiga mashairi, ngoma na kuicheza. Hapa ni usiku wa kusaidia fedha za kupunguza ukeketaji Tanzania, London, 2014. Ngoma oyee!

(more…)

Read Full Post »

Fab Moses  na gitaa  nyumbani kwake anapotunga nyimbo mbalimbali za Kiswahili, London. (picha na Freddy Macha, 2009)

Fundi  na mfanya biashara wa Kiganda, John Kizito mwenye kampuni ya kutengeneza magari, Bingol Engineering Company, (kusini mwa London) ni kati ya mashabiki wa  mwanamuziki Mtanzania anayewika hapa Uingereza karibuni.

“Fab Moses ananikumbusha wananamuziki wa Kiswahili wa zamani. Hapigi makelele wala hachanganyi matusi na maneno ya Kiingereza. Tena kajaaliwa sauti nzuri sana.”

Huyu Kizito ndiye babake aliyekuwa mrembo wa Uganda mwaka jana yaani Maria Namiiro.

http://www.ugpulse.com/articles/daily/Beauty.asp?about=Maria+Namiiro+is+Miss+Uganda+UK+2009&id=1102

Sifa alizozitosa John Kizito hazikuishia maneno matupu.  Maana mkono mtupu haulambwi. Alichangia gharama za CD ya kwanza ya Mbongo mwenzetu mwenye sauti inayokumbusha akina Marijani, Simba wa Nyika,  Sikinde, Mbaraka Mwinshehe na Tabora Jazz, wana Segere Matata.

Shoo ya kwanza ya Fab Moses  ilifanyika Ijumaa iliyopita, mjini Brighton, ukumbi wa Salsa Lounge ukingoni mwa bahari ya English Channel, hapa Uingereza.

Dhana yake iliyonyooka ni moja.

Inaitwa Nengua: mtindo wa kucheza (kukata kiuno na kujilegeza), CD na hata bendi.

Nengua ilikuwa na wanamuziki wakubwa stadi mbalimbali toka Kenya, Uganda na Tanzania. Toka Kenya, Ben Adolwa (mpiga Sax) kawahi kupiga na mtunzi maarufu wa wimbo wa “Malaika” (marehemu Fadhil William) na Billy Mwangura mpiga besi, mzawa wa Mombasa. Kongo wapo Mille Baguette (kawahi kufanya kazi na zee la jazz toka Cameroon, Manu Di Bango), Ladi Mbala na mpiga gitaa anayestawisha klabu za Waafrika London, Burkina Faso.

Toka Bongo wana Nengua wengine ni Jenny Kimali Harris (sauti ya kuitikia ) na Saidi Kanda (aliyetwaa tuzo la kimataifa la WOMAD la mpiga ngoma wa mwaka 1989). Kanda ambaye anavipaji lukuki : kuimba, gitaa, vyombo vya ala za kijadi mathalan zeze na marimba ni pia fundi mitambo. Alichangia sana katika kuitoa CD hii ya Nengua.

Tazama vitu vyake Mbongo mwenzetu anayetutia sifa Waafrika:

http://saidikanda.com/

Fab Moses ambaye hujulikana zaidi kama mcheza sarakasi na ngoma za kiasili kawahi kutoa CD nyingine akiwa na wanamuziki wa mseto wa bendi ya No Tchuna Cha (siku hizi Afrika Jambo) inayooongozwa na gwiji Kawele Mutimanwa na mwanamuziki wa zamani wa Simba wa Nyika, Rama Sax, toka Tanga, mwaka 1999.

Mwangalie Fab Moses akiimba hapa:

http://vids.myspace.com/index.cfm?fuseaction=vids.individual&videoid=42998197

Je unaitaka CD ya Nengua?

Ongea na Kizito +44-7939-112536

Au  Fab Moses : +44-7950-604530

Read Full Post »

Older Posts »