Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Freddy Macha Interviews’

Janet Chapman ni kati ya Waingereza wanaojitolea (bila mshahara au malipo ),  miaka mingi kujaribu kusaidia Afrika, hususan Tanzania. Akiwa mwanachama wa Shirika la Misaada ya Maendeleo Tanzania (TDT) na Jumuiya ya Waingereza na Watanzania (BTS) karibuni amejihusisha na suala la kutokomeza Ukeketaji. Katika mahojiano na “Kwa Simu Toka London” Mei 11, 2017 anafafanua mradi mpya wa kujenga ramani vijijini Tanzania, yaani “Mapping”. Je maana  na faida yake ni ipi?   Kufaidi zaidi mahojiano bofya CC  dirisha la You Tube upate maelezo yaliyoandikwa kitaaluma kuelewa kinachosemwa.

Advertisements

Read Full Post »

Riwaya zako tatu zimepishana miaka 36. Je kwanini, muda mrefu toka Utengano hadi Nyuso? Asali Chungu (1977), Utengano(1980) na Nyuso za Mwanamke (2010), Mhanga Nafsi Yangu (2012).
Vile vile dhamira kuu inamwangalia mwanamke kwa macho na hisia za kumtetea. Mwandishi mwingine Mwafrika anayesimama upande wa kina mama (hasa vitabu vyake vya mwanzo) ni Msomali – Nuruddin Farah. Je, kwanini wanaume muwatetee wanawake? Kwani hawawezi kuandika wenyewe?

Nyuso za Mwanamke
Mwandishi Said Ahmed Mohammmed
Kuandika riwaya au kazi yoyote ya fasihi kunahitaji wakati, utulivu na wiitisho wa ndani wa nafsi ya mwandishi. Huwezi tu kujilazimisha kufululiza. Kisha nadhani vita vya wanawake ni vita vya wanaume pia kama ilivyo kwamba vita vya wanaume ni vita vya wanawake. Kwa hali hii hakuna suala la kwa nini? Kwa bahati mbaya waandishi wanaume wachache tu ndio wenye msimamo wa ukombozi wa wanawake katika fasihi ya Kiswahili. Ama suala la wanawake kutoandika wenyewe wapo wachache katika fasihi ya Kiswahili wanaoandika hata kwamba hawajitetei. Jambo hili linashikamana na historia ya wanawake katika jamii zetu. Wanawake popote pale wamekuwa katika historia ya ukandamizwaji, je kwa nini tusiwatetee?.
(more…)

Read Full Post »