Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Janet Chapman’

Janet Chapman ni kati ya Waingereza wanaojitolea (bila mshahara au malipo ),  miaka mingi kujaribu kusaidia Afrika, hususan Tanzania. Akiwa mwanachama wa Shirika la Misaada ya Maendeleo Tanzania (TDT) na Jumuiya ya Waingereza na Watanzania (BTS) karibuni amejihusisha na suala la kutokomeza Ukeketaji. Katika mahojiano na “Kwa Simu Toka London” Mei 11, 2017 anafafanua mradi mpya wa kujenga ramani vijijini Tanzania, yaani “Mapping”. Je maana  na faida yake ni ipi?   Kufaidi zaidi mahojiano bofya CC  dirisha la You Tube upate maelezo yaliyoandikwa kitaaluma kuelewa kinachosemwa.

Advertisements

Read Full Post »

Picha na Habari za Freddy Macha, London

1-balozi-migiro-akihutubia-jumuiya-ya-watanzania-na-waingereza-pic-by-f-macha

 Balozi wetu Uingereza, mheshimiwa Dk Asha Rose Migiro alihutubia  jumuiya ya Watanzania na Waingereza (British Tanzania Society- BTS)  Jumamosi iliyopita. Hotuba hiyo iliyofanyika ukumbi wa Central Hall Westminster, London ni mara ya pili kwa balozi huyu mgeni kukutana na BTS. Mwezi Julai alikaribishwa rasmi akiwa na Balozi mpya Uingereza Tanzania Bi Sarah Cooke na aliyestaafu, Bi Diana Melrose.

8-bango-la-bts-pic-by-f-macha-2016

Mada hiyo iliyoitwa “Maendeleo ya Sasa Tanzania”  Ilikuwa sehemu ya mkutano wa 41 wa mwaka wa BTS na kuhudhuriwa na Watanzania na Waingereza wakazi hapa. (more…)

Read Full Post »

Picha  na habari za   Freddy Macha, London

Barabara ya Bond jijini London- pic by F Macha 2016

 Mwezi Julai Uingereza umekuwa wa vishindo vya kihistoria. Baba yao ni kujitoa Uingereza nje ya Jumuiya ya Ulaya (EU) na kuteuliwa Waziri Mkuu mpya mwanamke, Theresa May.

Kwa Watanzania, Uingereza mabadiliko ya mabalozi yalisikika.   Jumuiya ya Watanzania na Waingereza (British Tanzania Society) ilimkaribisha rasmi Dk Asha Rose Migiro na mwenzake mpya Tanzania, Bi Sarah Cooke. Bi Cooke aliyekuwa zamani Bangladesh alichukua nafasi ya Bi Dianna Melrose aliyesema aliwapenda sana Watanzania na lugha ya Kiswahili. (more…)

Read Full Post »

This slideshow requires JavaScript.

Maadhimisho ya miaka 40 ya urafiki kati ya Uingereza na Tanzania (BTS) yalifanyika mjini Reading, Jumapili 8 Novemba 2015. Wanamuziki watatu wa Kitanzania walialikwa kutumbuiza kwa mseto wa midundo ya kijadi na kisasa : Chakacha, Ilimba, Rumba na ngoma maarufu ya mkoa wa pwani iitwayo BUTI.
(more…)

Read Full Post »

TANZANIA- FGM
Ijumaa tarehe 30 Mei, London.
Ukumbi wa hoteli iliyoko kitongoji cha Hackney, kaskazini ya London ulishuhudia usiku wa muziki, chakula na vinywaji.
the-russet-front

Kila aliyeingia hapa alifahamu alichokijia. Hakukuwa na hotuba wala kelele nyingi. Mabango yaliyopitishwa miezi kadhaa yaliibeba bendera ya Tanzania na wito wa “NYIMBO KWA DADA ZETU”…matangazo yalienezwa sehemu mbalimbali London na mtandaoni. Wapenzi wa Tanzania weupe kwa weusi waliitikia wito.
FGM flyer London 2014
(more…)

Read Full Post »