Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Mariam Kilumanga’

Picha na Habari za Freddy Macha

 

Kila mwaka wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Ubalozi wa Tanzania huchagua usiku mmoja ambapo wananchi wa madhehebu yote hualikwa kufuturu.  Jumamosi 10 Juni, 2017 shughuli hii haikufanywa Ubalozini, wala haikuwa ya bure. Washiriki tulitakiwa kuchangia pauni 10 (kama shilingi 25,000) kutopoteza kodi za wananchi nje. Si kiasi kikubwa na kina mama nao walijitolea kupika na mikeka kukalia.

Pili,  mkutano wa takriban saa 3 na nusu uliwakutanisha Watanzania na Balozi Asha Rose Migiro kutathmini mada mbali mbali muhimu kabla ya kula. Desturi hii  ni ya kipekee kwa Watanzania na sijawahi kusikia ikifanywa na mataifa mengine. Zingatia pia kuwa kikao kilifanywa kanisa la Monravia, Hornsey kaskazini ya London.

(more…)

Advertisements

Read Full Post »

1- Nembo ya muda ya Jumuiya - pic by F Macha 2016 Nembo iliyopendekezwa…

Jumamosi Mchana 7 Aprili ilikuwa siku ya jua kali Uingereza.  Wananchi wengi walijazana bustanini au sehemu za starehe wakiota jua na kula barafu za sukari yaani “Ice Cream.” Magari yalipiga honi, wenyeji waliheushwa na ujoto ujoto huu adimu mazingira ya Ulaya. Ndani ya ofisi ya Ubalozi wa Tanzania London, kundi la Watanzania wanane lilikaa mchana wote likijadili (kwa ari na mori) maslahi ya wananchi wenzao Uingereza. (more…)

Read Full Post »

Alhamisi jioni, Wazalendo na marafiki zao walishiriki misa kuiombea Tanzania ndani ya kanisa mashuhuri la Westminster Abbey kuadhimisha miaka 50 ya muuungano.
Westminster Abbey-pic by F Macha 2014

Misa hizi hutayarishwa kila mwaka kwa heshima ya nchi za Jumuiya ya Madola. Mgeni rasmi alikuwa Balozi wetu Uingereza Mheshimiwa Peter Kallaghe( pichani chini akisalimiana na baadhi ya walioshiriki), maofisa ubalozini na wawakilishi wa Jumuiya ya Uingereza na Tanzania (British-Tanzania Society).
Balozi Kallaghe na Watanzania Wahindi Westminster- pic by Rashid Dilunga 2014
(more…)

Read Full Post »

LOGO -fashion Sept 7- by Sara Abood
Mchoro wa shughuli uliobuniwa na Sara Abood.

Wabunifu mavazi wanne toka Tanzania walioshiriki maonesho ya mavazi Ubalozi wetu London Jumamosi Septemba Saba wamechaguliwa kuingia dimba la kimataifa London Fashion Week, Februari mwakani.
Wasanii hao waliopewa nafasi ya kujitangaza kupitia jitihada za Jumuiya ya Wanawake Uingereza (TAWA) ukishirikiana na Ubalozi ni mseto wa wafanyabiashara wakongwe na vijana wanaoanza fani hii ya urembo.
Mama Joyce Kallaghe-pic by Felipe Camacho
Mama Joyce Kallaghe, ni mtangazaji mzuri wa mavazi ya Kitanzania ughaibuni. Picha na Felipe Camacho.

Akifungua shughuli hii, mkewe Balozi, Mama Joyce Kallaghe alikumbusha hii ni nafasi nzuri kwetu.
“ London Fashion Week” ni tafrija maarufu inayofanyika sambamba Paris, New York, Milan mwezi Februari na Septemba kila mwaka toka 1984. Mbali na msaada wa TAWA na Ubalozi, mwekezaji mkuu wa shughuli hii ni British Council- shirika linaloendeleza vipaji nchi zaidi ya 100 duniani kwa miaka 75 sasa.
Mada ya maonesho iliitwa “Fahari Passion 2013” na mchoro wake uliobuniwa na Bi. Sara Abood unaonyesha uso wa mwanamke na rangi za bendera ya taifa.
Khanga dress tight
Khanga inavyojigamba na kupendeza. Picha na Abubakar Faraji
(more…)

Read Full Post »