Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Mutabaruka’

The Strand London- pic by F Macha 2016

Ndogo Ndogo Mitaani Ulaya

Wazungumzaji , wanafunzi na wapenzi wa Kiswahili  wana-arifiwa safu mpya ya mwandishi Freddy Macha.

Baada ya miaka mingi akitathimini, kutafiti  na kutangaza habari, fasihi na makala, ameanzisha kipindi kipya (cha Video)  mtandaoni.

https://www.youtube.com/channel/UCtVEe3zlUtuF6pTbn_OK8JQ

Ndiyo nini?

“Kwa Simu Toka London” siyo toleo la hali ya juu au kustaajabisha. Macha anatumia weledi na ujuzi wake  kuelezea -kupitia simu ya mkononi- kadhia mitaani, maholi na majumbani,  London, na kwingineko anakotembelea Ughaibuni.  Teknolojia inakayotumika ni ya kawaida tu kwa chombo hiki tulichokizoea siku hizi. (more…)

Advertisements

Read Full Post »

Kinyume na wengi wanavyodhani, si Marasta wote huvuta bangi.
Mshairi maarufu wa Kijamaika, Mutabaruka ni mfano mzuri. Hanywi pombe, havuti sigara, havuti bangi, hali chakula katika mahoteli, hujipikia mwenyewe au kusafiri na mpishi wake. Anaamini katika “uasilia wa mambo” na hivyo huenda peku peku kila mahali. Nimewahi kukutana naye mazingira yenye barafu Ulaya, jua kali la Marekani ya Kusini, kamwe hakati nywele au havai viatu. Nimemwona hapa London katika baridi, mvua na unyevu unyevu, viatu, ndala au buti haviingii miguuni.

Interviewing Mutabaruka, Salvador Bahia 1993-pic by Amita Tiwari

Nikimhoji Mutabaruka (kushoto), mjini Salvador, Brazil, mwaka 1994. Picha na A Macha…

Alizaliwa mwaka Desemba 1952 na jina la ubatizo lilikuwa Alan Hope. Alipopata mwamko wa kujielewa yeyé na nani, kwa fahari ya Uafrika akabadili jina kuwa Mutabaruka. Jina hilo ni la Kinyarwanda, lina maana “mtu anayeshinda nyakati zote…” Si mwoga kutenda au kusema. Si mnafiki hata chembe.
Sikiliza mashairi yake Mutabaruka utapata elimu na hekima kubwa kuhusu kujielewa na kujitambua tunakotoka, hasa sisi Waafrika.
Shairi lake nilalolipenda ni hili lililorekodiwa mwaka 1983….Check it.

Read Full Post »