Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Swahili Music’

 

Ukumbi wa The Eastern District Social Club, Northampton haujulikani kwa wengi. Hata hivyo eneo hili nje kidogo ya mji, ulijikuta ukikaanga Maandazi , Vitumbua na Nyama Choma punde Wasanii mseto wa Kitanzania walipozindua WASATU – jumuiya ya kuwakutanisha na kuwaunganisha. Ilikuwa Jumamosi 1 April, 2017.
Wimbo maarufu wa Les Wa Nyika, SINA MAKOSA, uliotungwa na Omari Shaaban, kuimbwa na Issa Juma na kupambwa gitaa maridadi la John Ngereza, ulikuwa kati ya vibao mbalimbali vya Kiswahili vilivyotukumbusha tukokako, na tu wapi, duniani. Umoja ni nguvu. Kiswahili oyee! Tanzania Oyee! Afrika Mashariki na Kati oyee!

Advertisements

Read Full Post »

Flyer by Evelina Moceviciute 2015
Mwanamuziki mkazi London, Freddy Macha, anatazamiwa kutumbuiza kwa ngoma na muziki wa gitaa, kwenye tafrija ndogo kutangaza na kuuza picha za watoto wa Kitanzania. Tafrija na maonesho yametayarishwa na wapiga picha watatu wa Kizungu, Amy Read, Evelina Moceviciute na Saraya Cortaville waliofanya kazi za kujitolea Mbeya vijijini mapema mwaka huu. Mauzo ya taswira yatatumika kusaidia maisha na elimu ya watoto hao hao waliopigwa picha. Mradi mzima unaitwa “Ahsante Children”…kutukuza na kutangaza lugha ya Kiswahili, Tanzania na wananchi Afrika Mashariki.
Onesho litafanywa mkahawa wa
The Chapel
St Margaret’s House,
21 Old Ford House,
Bethnal Green,
Hackney, London E2 9PL.
Jumapili 4 Oktoba 2015.
Saa 11 na nusu jioni hadi 3 usiku.

HABARI ZAIDI
http://www.freddymacha.com/
Freddy Drums - Germany May 2012- pic by Luis Tome Passarello
Freddy Macha na ngoma. Picha ya Luis Tome Passarello

Read Full Post »


Tamasha la kimataifa Ubongo Fest kuadhimisha maisha na kazi za mwanamuziki Remmy Ongala litafanyika mjini Dar es Salaam Jumamosi ijayo tarehe kumi, ukumbi wa Leaders, Kinondoni.
Tamasha hilo ambalo linaangukia sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania litahusisha watumbuizaji toka Uingereza, bara Afrika na wanamuziki maarufu nchini mathalan Twanga Pepeta, Msondo Ngoma, Bendi ya Matimila, Jikhoman, Mrisho Mpoto na Banana Zoro.

Aziza Ongala

Akifafanua habari hizo binti yake marehemu, Aziza Ongala, alisema Ubongo Fest inatukuza kazi za baba yake aliyeimba kuhusu umaskini, ulaji rushwa, maisha, imani, madhara ya UKIMWI na fahari ya Utanzania. Ingawa mwanamuziki huyu aliyebatizwa jina la “Dokta” na wanahabari, alizaliwa Kongo aliigeuza Tanzania kuwa nyumbani na familia yake baada ya kuhamia nchini mwaka 1978 akiimbia bendi ya Mzee Makassy.
“Ubongo Fest” alifafanua Aziza imetokana na neno Dokta Remmy alilotumia kufafanua mtindo wake wa “Bongo Beat” aliouimba na kwamba lengo lake ni kutumia tafrija kuwa jukwaa la wasanii wa kimataifa kuonyesha, kuvumbua na kutukuza vipaji mbalimbali vya watunzi nchini. Aziza na mumewe Mjamaika, Miael McGeachy wanaoishi London wanasema tamasha hili ni kipemgele cha Dk. Remmy Ongala Foundation iliyoundwa karibuni Uingereza kuendeleza kazi za Ramazani Mtoro Ongala. Moja ya matazamio yake ni kujenga shule ya wasanii na watoto yatima Tanzania.
“Lengo letu ni kutoa nafasi kwa wasanii wa Kitanzania kujenga mawasiliano ya kimataifa ili kusaidia ujenzi wa uchumi na utamaduni Tanzania. Ubongo Fest itakuwa mwanga mkubwa wa Kitanzania utakaorodheshwa katika sinema na rekodi. Ni mategemeo kujenga kiu ya soko la wageni kuja kwetu kadri tamasha litakapozidi kuimarika na kufahamika duniani,” wanaeleza.

Miael McGeachy mumewe Aziza Ongala akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Watanzania Uingereza, Said Surur(wa tatu kulia) na mdau wa Kitoto, mjini London kabla ya kuelekea Dar es Salaam kutayarisha shughul ya Ubongo Fest na mkewe na familia ya marehemu Ongala. Picha na Urban Pulse

Soma habari zaidi : http://www.dkremmyongalafoundation.com

Read Full Post »

Nilitunga “Paka Mweusi” nikiishi Mwananyamala Kisiwani, Dar es Salaam…

1.
Paka Mweusi
Aligongwa na Gari
Barabarani
Saa za Jioni
Dereva akasema huo ni mkosi..

2.
Paka Mweusi
Alifia darini
Alikuwa akinuka
Nikapanda kumtoa
Nikaambiwa huyo ni jini…

3.
Paka paka jama
Kiumbe mzuri
Amegeuzwa
Kuwa ni shetani

Pale nilipopangisha nyumba ulilala uwanja wa mpira (wa mchanga) kwa nyuma na mbele ilisimama dede, baa kuu maarufu sana mtaa mzima wa Mwananyamala yaani, Wami. Jumba kubwa nililoishi lililokuwa na wapangaji na familia zaidi ya 10…lilikaa mithili wa taya kuu la kutokea “Mwananyamala A” kwenda Mwananyamala Kisiwani. Hapakumalizika vituko, mapenzi, ukahaba, masihara, uporaji, ukabaji, maisha ya watu waliofurahiana, waliozozana, waliotaniana, waliohusudiana, waliokosana; watoto waliocheza ndani ya maji, mchanga na matope; walionipa uelewa mkubwa wa jamii ya Waswahili na makabila mbalimbali jijini, Dar es Salaam. Mara moja moja utawaona watoto wadogo wakimbeba paka aliyeogofya wakamshika mkia kama tiara au pia wakamzungusha hewani, wakamrusha matopeni, mtini au juu ya paa ama ukuta utadhani kifuu cha nazi…

Nilihamia pale 1975 baada ya kumaliza jeshi; nikaanza kazi magazeti ya Uhuru 1976, hadi nilipohama mwaka 1982.

Nikiwa jeshini Mafinga, Iringa, 1975…

1979 nilipotunga kibao hiki ulikuwa mwaka mgumu sana Bongo na Afrika Mashariki. Ndio mwaka majeshi ya Tanzania yalivyosaidiana na wananchi wa Uganda kumtoa kiongozi wao mnyanyasaji na muuaji, Idi Amin Dada; zikaanza foleni za vyakula na bidhaa muhimu.

Mfalme Jean Bedel Bokassa aliyeangushwa 1979 akashtakiwa na watu wake kwa hatia za mauaji na udhalilishaji wa umma..

Kiulimwengu, ulikuwa mwaka wa viongozi wengi wakorofi sana kuangushwa mathalan, Rais Jean Bedel Bokassa wa Jamhuri ya Kati na Fransisco Nguema wa Equatorial Guinea. Ulikuwa pia mwaka ambao kilele cha mapigano ya Uhuru wa Zimbabwe…kilifikia…nikapata habari rafiki yangu mpigania Uhuru, Soul Zuka, kafariki akipigana na wenzake walioongozwa na Robert Mugabe na marehem Joshua Nkomo. Leo sijui Soul Zuka angesemaje angeiona Zimbabwe iliyopawatia uhuru Waafrika mwaka 1980…na aliyoimwagia damu..!

1979…vile vile ndipo wasanii wenzangu kadhaa walipoanza kuongelea kuunda bendi iliyokuja kuitwa Sayari. Mazungumzo yalifikia kilele Septemba 1981 tulipofanya onyesho la kwanza ukumbi wa Utamaduni wa Wajerumani, Goethe Institut…
Baada ya muda “Paka Mweusi” ulikuwa mmoja ya nyimbo nilizoimba na Wanasayari…

Read Full Post »

Video mpya ya mtunzi,  mwanamuziki na mwandishi wa Kitanzania, mkazi wa Oslo kule Norway imetoka.

Wimbo wake Dar es Salaam ama kweli unatukuza jiji kuu la Bongo ambalo maana yake kwa Kiarabu ni bandari (ama mji) wa amani. Wana Morogoro (alikozaliwa Nasibu Mwanukuzi) hupenda kutania Morogoro ni mji kasoro bahari wakiwa na maana sifa kuu ya Dar ni yale maji chumvi, minazi; kifupi kitovu cha Tanzania.

Read Full Post »

RAS NAS  ZIARANI NORWAY 2009

Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya rege na muziki wa dansi mwenye makao  Oslo, Norway, Ras Nas ( Nasibu Mwanukuzi),  anapanga safu kali kwa ajili ya ziara ya miji sita Norway. Ziara hiyo itakayoanza Kongsberg tarehe 23 Oktoba itamalizikia jijini Trondheim 7 Desemba.

RAS NAS TOUR 2009

Kikosi cha Ras Nas kinachanganya wanamuziki toka Congo Brazzaville, Ivory Coast, Norway na Marekani. Wabongo wa Norway habari ndiyo hiyo!
Mwezi wa Desemba Ras Nas na bendi yake watatembelea miji ya Galle na Colombo Sri Lanka kuwasilisha Norway, ( watapita Tanzania pia) katika tamasha la muziki.

Kwa habari zaidi fuatilia http://www.rasnas.kongoi.com.

Read Full Post »

 

fab-moses-pic by f macha

Si wanamuziki wengi wanaoishi ughaibuni toka Bongo.  Miaka mingi hata hivyo  amekuwepo mtunzi na mwimbaji, Fab Moses ,  CD na shoo yake inayoitwa NENGUA.

Mtazame katika tovuti  ya My Space:

http://vids.myspace.com/index.cfm?fuseaction=vids.individual&VideoID=42998197

Mbali na nyimbo zake mathalani: “Ngunguri Ngangari” na “Nyerere” , Fab Moses huonekana katika majukwaa kadhaa ya London akitungua nyimbo mbalimbali za Kiswahili na bendi mashuhuri ya Afrika Jambo.  Bendi hii inasimamiwa na magwiji Kawele “Finger Printer”Mutimanwa, mpiga gitaa mashuhuri wa Kikongo, Uingereza na Ramadhani Athumani Mtunguja (“Rama Sax”) mpiga saxafoni mzawa wa Tanga aliyekuwa zamani na Simba wa Nyika na Les Wanyika na kushikiri katika kibao maarufu Sina Makosa kilichotolewa Nairobi mwaka, 1978. Afrika  Jambo hutumbuiza klabu kadhaa mashariki ya London zikiwemo (East Side Bar, Ilford) Kila Jumapili na Railway Tavern klabu ya Waganda, Forest Gate.

Waliomsikia Fab Moses huvutiwa na uzuri wa sauti yake inayokumbusha vibao mbalimbali vya nyumbani kama nyimbo za Shabani Marijani (Georgina), Simba wa Nyika, Mlimani Park, nk. Moja ya Sifa anazopewa Fab Moses ni sauti inayolandana sana na ya mwanasokomoko, hayati Marijani.

Mwanamuziki Fab Moses ni vile vile mwanasarakasi wa siku nyingi aliyeshafanya kazi na vikundi kadhaa nyumbani ikiwepo Muungano (cha Mzee Nobert Chenga) na Black Eagles. Kwa takribani miaka minane sasa anaongoza kikundi chake cha sarakasi na michezo jukwaani kinachoitwa Highflyers. Walioshamshuhudia (nikiwemo) wanakubali Fab Moses ni  mwalimu na kocha mzuri sana wa Sarakasi. Chini ya utaalamu wake mtu yeyote (watoto kwa wazima) anaweza kufundishwa kujinyonga nyonga na kuwa mwanasarakasi. Hilo latokana na uvumulivu na ufundi wake, Mtanzania huyu mwenye vipaji vingi…

fab-moses-singing

Habari zaidi za NENGUA, kikundi cha Sarakasi (Highflyers) au Afrika Jambo; mpigie Fab Moses -+44-7950-604530

Barua pepe: fabrahs@yahoo.co.uk

Picha na Freddy Macha

Read Full Post »