Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Ubalozi Tanzania London’

Habari na Picha za Freddy Macha

TUMEZOEA kuwaita wenye hali hii “taahira” – neno la asili ya Kiarabu lenye maana “mtu asiye sawa” (wazimu, chizi, bwege, nk). Ila sahihi ni “mtindio ubongo” – kwa Kiingereza “Down Syndrome”….
(more…)

Advertisements

Read Full Post »

Picha na Habari za Freddy Macha

 

Kila mwaka wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Ubalozi wa Tanzania huchagua usiku mmoja ambapo wananchi wa madhehebu yote hualikwa kufuturu.  Jumamosi 10 Juni, 2017 shughuli hii haikufanywa Ubalozini, wala haikuwa ya bure. Washiriki tulitakiwa kuchangia pauni 10 (kama shilingi 25,000) kutopoteza kodi za wananchi nje. Si kiasi kikubwa na kina mama nao walijitolea kupika na mikeka kukalia.

Pili,  mkutano wa takriban saa 3 na nusu uliwakutanisha Watanzania na Balozi Asha Rose Migiro kutathmini mada mbali mbali muhimu kabla ya kula. Desturi hii  ni ya kipekee kwa Watanzania na sijawahi kusikia ikifanywa na mataifa mengine. Zingatia pia kuwa kikao kilifanywa kanisa la Monravia, Hornsey kaskazini ya London.

(more…)

Read Full Post »

ANAYO AZMA YA KUINDELEZA TANZANIA NA KUONDOA UMASKINI BARANI!!!

Ali Sungura-mdhamini, Balozi Kallaghe, Malkia Kassu, Aisha Mohammed, Allen Kuzilwa- London 2013- pic by Ali Surur
Kutoka kushoto ni mdhamini, Bw. Ali Sungura, Balozi wetu Uingereza , Mheshimiwa Peter Kallaghe, Malkia Kassu, sahiba mkuu Aisha Mohammed na Afisa Balozi, Allen Kuzilwa.
Picha na Said Surur

Jumuiya ya Madola ilianzishwa karne ya 19 kushirikisha makoloni ya Uingereza. Mwaka 1949 chini ya himaya ya kifalme, nchi huru zilihusishwa. Toka 1973 mikutano ya wanajumuiya imefanywa kila baada ya miaka miwili chini ya Malkia Elisabeth. Lakini Jumuiya ya Madola si tu siasa na mikutano. Ina mirengo mbalimbali ikiwemo michezo, uchumi, utamaduni, familia, urembo wa mavazi, fikra na tabia.
Mashindano ya kuwatafuta warembo wa kike na wa kiume hufanywa kila mwaka. Taji zinazoshindaniwa ni Mrembo wa Vijana wa Jumuiya ya Madola, Mrembo wa Jumuiya ya Madola ya Kimataifa na Mrembo wa Kimataifa wa Jumuiya hiyo. Malengo ya mashindano haya ni mengi na baadhi ni…
• Kuendeleza maisha ya wananchi duniani
• Kuondoa umaskini, hasa ule unaowahusu watoto na mama zao, familia, michezo, maisha na afya ya wanyama
• Kampeni za maonyesho ya kusaidia maendeleo ya kijumuiya
• Kuendeleza mashirika ya fadhila
Na kadhalika.
The crowned queens of the Commonwealth 2013-pic by Jay Pedram
Mtanzania, Malkia Kassu ( wa tano toka kushoto) akiwa na washindi wenzake – wote wamevalia taji na kubeba vikombe vya ushindi.
Picha na Jay Pedram
(more…)

Read Full Post »

LOGO -fashion Sept 7- by Sara Abood
Mchoro wa shughuli uliobuniwa na Sara Abood.

Wabunifu mavazi wanne toka Tanzania walioshiriki maonesho ya mavazi Ubalozi wetu London Jumamosi Septemba Saba wamechaguliwa kuingia dimba la kimataifa London Fashion Week, Februari mwakani.
Wasanii hao waliopewa nafasi ya kujitangaza kupitia jitihada za Jumuiya ya Wanawake Uingereza (TAWA) ukishirikiana na Ubalozi ni mseto wa wafanyabiashara wakongwe na vijana wanaoanza fani hii ya urembo.
Mama Joyce Kallaghe-pic by Felipe Camacho
Mama Joyce Kallaghe, ni mtangazaji mzuri wa mavazi ya Kitanzania ughaibuni. Picha na Felipe Camacho.

Akifungua shughuli hii, mkewe Balozi, Mama Joyce Kallaghe alikumbusha hii ni nafasi nzuri kwetu.
“ London Fashion Week” ni tafrija maarufu inayofanyika sambamba Paris, New York, Milan mwezi Februari na Septemba kila mwaka toka 1984. Mbali na msaada wa TAWA na Ubalozi, mwekezaji mkuu wa shughuli hii ni British Council- shirika linaloendeleza vipaji nchi zaidi ya 100 duniani kwa miaka 75 sasa.
Mada ya maonesho iliitwa “Fahari Passion 2013” na mchoro wake uliobuniwa na Bi. Sara Abood unaonyesha uso wa mwanamke na rangi za bendera ya taifa.
Khanga dress tight
Khanga inavyojigamba na kupendeza. Picha na Abubakar Faraji
(more…)

Read Full Post »

Wabunifu mitindo watatu walishiriki maonyesho ya mavazi London Fashion Week yaliyotayarishwa na shirika la British Council na kudhaminiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Ubalozi wetu Uingereza.
Tanzania na Nigeria ndiyo nchi pekee za Kiafrika zilizong’arisha “jua” lake kati ya mataifa zaidi ya 25.
Filamu hii fupi iliyokaangwa na Urban Pulse wakishirikiana na Freddy Macha inakupa taswira ya mambo yalivyokua.

Read Full Post »

Maonyesho maarufu ya mavazi  –London Fashion Week–  yaliyoanza rasmi Ijumaa iliyopita mjini London yameiweka ramani ya  Tanzania duniani.

Image     Wageni wa Kijapani wakiwa na Chichia  anayehamasisha fani ya Khanga. Picha na Aaron Miclat.

Shughuli hii muhimu kiuchumi na kisanaa inayoendelea  juma zima  na kuhusisha vituo vya kitamaduni na balozi 27  ina lengo la kutangaza vipaji vya wabunifu mavazi toka  nchi zisizojulikana  uwanja huu mahiri wa kimataifa unaosifika takriban miaka 30 sasa.

Image  

Moja ya vazi la kanga lililobuniwa na Chichia. Picha ya Urban Pulse

“London Fashion Week”  ni moja ya maonyesho manne ulimwenguni yaliyoasisiwa rasmi kutukuza  ubunifu, ufundi na biashara  mwaka 1984.
(more…)

Read Full Post »

Mariam ( wa  chama cha Akina mama Tanzania London- TAWA) ; Elizabeth Kawogo (ambaye hakutaka sura yake ionyeshwe) na mshikaji  wenu; tukiwa pamoja jana London. (Picha imepigwa na dadake Mariam).

Kisa cha kusikitisha na kuudhi sana.

Katika karne hii ambayo tunaambiwa Watanzania tuko huru toka mwaka 1961…bado kuna utumwa. Ilianzia mwaka 2004 Elizabeth Kawogo akifanya kazi ya usafi kwa Mhindi pale Upanga, Dar es Salaam.

Akakaribishwa na mwajiri wake huyo Zainab Alibhai kuja Uingereza. Akawasili Julai 2006. Kuanzia hapo hadi alipotoroka Mei 2007, dada wa watu mzawa wa Njombe aligeuzwa manamba, kijakazi wa wazazi wake Alibhai. Si ukweli kusema Wadosi wote wabaya, wala si vizuri kusema kila Mswahili mzuri. Kila kabila lina wabaya na wazuri. Lakini kisa cha Elizabeth mikononi mwa watu hawa kilikuwa cha mateso. Alifanya kazi kila siku kuanzia saa moja asubuhi hadi alipojitayarisha kulala saa nne za usiku; siku saba kwa juma. Alichoruhusiwa ni kwenda tu kanisani (saa moja tu) Jumapili. Baas.

London hiyo. Majuu isiyokuwa na joto wala jua. Miezi saba ya baridi aliumia akilala sakafuni katika kagodoro kembamba, blanketi na shuka moja. Hakupewa viatu wala nguo za kuzuia baridi. Vyakula vizuri alivyowapikia jamaa zake (chapati, biriani, sambusa, pilau nk) hakuvila; yeye mpikaji aliambiwa ale  makombo.  Siku nyingine akaambiwa ale tu mkate wa juzi ulioshapitisha tarehe (“mkate wa njiwa,” anasema). Afadhali yangeishia hapo.

Mshahara hakulipwa hata senti tano. Waajiri wake eti wanajitetea alikuja kujitolea, mgeni tu wa familia. Je, mgeni huwa anateswa? Desturi gani hiyo?

Nilipomwona sikuamini huyu ni dada mdogo mwenye miaka 25.

Kanyong’nyea, kanyong’onyeshwa, nyang’aro! Hata picha tuliyopiga naye kaomba tumfiche uso. Bado anaogopa; bado ana wasi wasi. Akiongea humsikii. Keshachoka kuelezea mkasa uliompata; kwake ni usaha  ulioshatumbuliwa, ingawa kwetu ni kisa kipya, tunataka kuelewa zaidi, kukisikia, kwake karaha tupu. ANATAKA TU ARUDI NYUMBANI. KESHACHOKA.

Hana raha ingawa tayari yuko huru. Mahakama ilimtetea mjini London na kuwaamuru wajiri wake, Bwana na Bibi Ramzani Dhanji wamlipe paundi 58, 585.00. Ukweli hicho ni kiasi kidogo kwa makadirio ya maisha ya Ulaya lakini walikisia mshahara ambao hakupewa na mwaka wa mateso aliyopitia. Waliomwokoa wanastahili sifa.

Kwanza mawakili waliomtetea bila kudai hata senti: Pro Bono and Access to Justice na Brent Law Community Centre…hawa mawakili walimpigania. Wakasaidiwa na hakimu aliyewashutumu waajiri wake kuwa WAAJIRI WASIWATENDEE WAFANYAKAZI WAO WA NYUMBANI NAMNA WANAVYOWATESA KULE BONGO. UINGEREZA HII…AKASHUTUMU VIKALI.

Vile vile…

Akina mama wa TAWA (Tanzania Women Association, London) wakiongozwa….na  Patricia Mzena (aliyekutana mara ya kwanza kanisani na kumkomboa baada ya Eliza kujuana na Bertha) na Mariam Kilumanga aliyeharakatika KIMYA KIMYA MWAKA MZIMA. Hadi sasa unaposoma haya makala, Eliza yuko kwake Mariamu…

Bila kumsahau, mheshimiwa  Radhia Msuya (aliyekuwa ) Ubalozi wa Tanzania aliyechangia kwa kila hali…maana Elizabeth alishang’anywa pasipoti na waajiri wake na kunyimwa kila haki. Ubalozi wa Tanzania ulisaidia sana kupigania maslahi ya dada huyu.

UBAYA UPO MMOJA LAKINI.

HABARI ZILIZOENEA MJINI NI KUWA WAPO WENGINE WENGI KAMA ELIZABETH. WENGI WALIOLETWA NA WADOSI NA WABONGO WENZAO (WA DAMU NA KABILA) AMBAO HATA PA KUONDOKEA AU KUSHTAKI HAWANA.

JE UNAMFAHAMU MTU KAMA HUYU?

TUSAIDIANE KUWAFICHUA…

TUKO PAMOJA….

Read Full Post »