Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Warsha’

HAKUNA MWENYE BAYA LA KUMSEMA MTANZANIA HUYU ALIYEKUWA MUUNGWANA KUPINDUKIA…

Freddy Mtoi wa kwanza kushoto akiwa na Salim Kikeke, Zuhura Yunus na Freddy Macha. Picha ilipigwa mwaka 2010 na Hassan Mhelela wa BBC…

Hakuna aliyezisikia habari za kifo cha mwanahabari na mtangazaji wa Kiswahili (aliyefanya kazi siku zake za mwisho redio mashuhuri ya BBC London) akaacha kushtuka. Baada ya kushtuka, huzuni tele.
Hakuna nliyemsikia akisema neno baya kuhusu marehemu Freddy Mtoi aliyefariki jana asubuhi hapa Uingereza.
Yeye nami tuliitana “Wajina” – heshima juu.
Freddy Mtoi alikuwa mpole kuzidi, rahisi kutabasamu, msikilizaji mzuri sana mkipiga porojo lakini hasa wakati akikuhoji. Niliwahi kumtania kuwa alinikumbusha “mtindo wa utulivu” (“laid back”, “cool”) aliokuwa nao mtangazaji mashuhuri wa Kiingereza, Michael Parkinson aliyefanya shughul ya utangazaji zaidi ya miaka 40, akastaafu 2007.

Mtangazaji maarufu wa Kiingereza, Michael Parkinson mwenye mtindo mtulivu wa kuhoji ambao sichelei kuulinganisha na wa marehemu Freddy Mtoi. Picha ihsani ya gazeti la Daily Telegraph…

Marehemu Mtoi (kama walivyo watangazaji na wanahabari wapevu) alikuwa na mtindo huo wa akina Parkinson au magwiji wenye subira na ujuzi wa kumsikiliza na kumfanya mhojiwa ajisikie huru kusema na kujieleza; haingilii ingilii ovyo maongezi au kumtisha kwa sauti kali, makeke au kumsonga songa. Mtoi aliongea kwa upole, alituliza wasikilizaji kwa kuwaelezea na kuwaelemisha kuhusu linalotokea. Ni kama mnasogoa huku akielemisha wasikilizaji. Kama wewe mwanafunzi wa habari na utangazaji msikilize akihoji…utajifunza mengi.
Nasema hivi kwa kuwa “Wa Jina” Mtoi alinihoji mara nyingi sana kuhusu mada na matukio mbalimbali.
Mara ya mwisho ilihusu kifo cha mwanamuziki Amy Winehouse aliyefariki mwezi Julai 2011.

Picha hii ilipigwa na Salim Kikeke, mtangazaji maarufu wa BBC, miaka miwili iliyopita wakati wa warsha la wanahabari na wanablog mjini London.
Toka kushoto ni Zuhura Yunus (BBC Swahili), marehemu Freddy Mtoi, mwandishi Freddy Macha na Tarama Nerima, mtangazaji wa Kiswahili toka Kenya.

Kinyume na wengi walio wachoyo wa sifa na hongera, walio rahisi kudonoa wenzao kwa kutafuta tafuta dosari tu, Freddy Mtoi alikuwa tajiri wa kukubali uwezo, ujuzi, maarifa, kipaji cha anayezungumza naye. Mathalan aliupenda na kuusifia sana wimbo wangu wa “Kilimanjaro” akiuliza kwanini haujulikani ipasavyo?
(more…)

Read Full Post »


Warsha la Mei 2009, katika ukumbi wa British Council, Dar es Salaam.
Picha na Innocent Swai

Kwa watakaohudhuria warsha za siku mbili ukumbi wa Fasdo, Tandika, mnaombwa mujisajili na Mkurugenzi Chande na mwenzake Nassib shauri ya masuala ya chakula na vinywaji.

Fasdo: (Faru Arts Development Organisation)
http://www.fasdotz.org
Chande Nabora: Simu 0713-310755
Nasibb: 0713-261011


Timu ya mpira ya vijana wa Fasdo.
Picha na Lilian Nabora

R A T I B A

1.Jumanne 11 Oktoba, 2011…

Asubuhi ( saa tatu kuendelea)
Utangulizi: Kujuana na kusalimiana
Mazoezi ya viungo na kujinyoosha nyoosha
Mada : Afya na umuhimu wa mazoezi

Chakula cha mchana

Mchana (saba/nane)
Kujiendeleza : Umuhimu wa kusoma, kujituma, Fasihi na Lugha ya Kiswahili/ Kiingereza

Maswali na Majibu toka Wahudhuriaji
MUZIKI kwa wote (“jam session”)

Mdau wa Kitoto akicheza na mcheza dansa toka Nigeria, Funmi Adenkule, wakati wa tamasha la muziki wa Kiafrika lililofungwa na bendi maarufu ya Osibisa, London, 2004…
Picha na Louisa Le Marchand…2.

Jumatano 12 Oktoba, 2011…

Asubuhi ( saa tatu kuendelea)
Utangulizi: Kujuana na kusalimiana
Mazoezi ya viungo na kujinyoosha nyoosha (kifupi)
Mada : Muziki na Kuimba
Mazungumzo kuhusu Muziki wa Tanzania unavyoendelea na matazamio

Chakula cha mchana

Mchana
Mada : Kujiendeleza / Maisha Ughaibuni
Uandishi na Fasihi : Umuhimu wake

Maswali na Majibu toka Wahudhuriaji
MUZIKI kwa wote (jam session)

VIFAA
1. Njoo na kijitabu cha kuandika, au chombo cha muziki kama mpigaji
2. Vaa mavazi rahisi kufanyia mazoezi na kanga, mkeka au kitambaa cha kutandika chini…


Mwana Kitoto akitumbuiza muziki wa “Berimbau” kwa kadamnasi na Sabu, mwalimu wa mchezo wa Kibrazili, Capoeira, mjini London, mwaka 2009.
Picha na Louisa Le Marchand…

Read Full Post »

Mdau wa Kitoto natazamia kufanya semina mbalimbali za afya, mazoezi ya viungo, muziki, fasihi, lugha nk katika ukumbi wa Fasdo ulioko Tandika, Dar es Salaam; Jumanne tarehe 11 na Jumatano tarehe 12 Oktoba, 2011.Wote mnakaribishwa…


Moja ya shughuli lukuki zinazofanywa na kituo hiki cha maendeleo ya sanaa na michezo ni utengenezaji wa vitambaa vya Batik, vilivyofanywa na akina mama wa Fasdo.
Picha na Lilian Nabora

Kiingilio bure.
Habari zaidi wasiliana na Chande Nabora, Mkurugenzi wa Fasdo. Simu namba 0713-310-755 au Nasibb 0713-261011.

Darasa la utengenezaji wa sabuni….
Picha na Lilian Nabora na Ticky Tedvan.

Tembelea tovuti yao : http://www.fasdotz.com


Darasa la kuimba.
Picha na Lilian Nabora


Mfano wa warsha za mazoezi na afya ya mwili mdau niliyofanya Nyumba ya Sanaa mwaka 2009.
Picha na Innocent Swai.

Read Full Post »

DSCI0168

Zoezi maalum la kusaidia mabega kutokana na kazi mbalimbali zinazoathiri migongo, shingo na kichwa. Kuning’iniza bega moja ukizungusha mkono pande zote, huku mkono mwingine umeshika kiti au meza. 

Semina zilitayarishwa na jarida la LUCKY linaloendeshwa kwa ushirikiano wa wananchi wanaojitolea mhanga kuelemisha na kuendeleza jamii ya Tanzania.  Waliosimamia kazi hii ni Innocent Swai na mhariri wake Anna Rugaba. Zilifanyika Ukumbi wa British Council, Shule ya Sekondari Mwandege, Pwani; Nyumba ya Sanaa na Soma Cafe, Mikocheni.

 Nilialikwa kuendesha mada nne muhimu:

1-Maisha ya Ughaibuni : utamaduni, elimu, kazi, uzoefu nk.

2-Afya, Chakula na Mazoezi ya mwili na viungo kwa jumla

3-Uandishi, fasihi na umuhimu wa kusoma na vitabu

4-Muziki : utunzi, uimbaji, upangaji na sanaa

5-Kitabu changu “Mpe Maneno Yake”

WKshops Dar -6

Mazoezi ya viungo, Ukumbi wa Vijana wa Tayoa (Tanzania Youth Alliance) Nyumba ya Sanaa.

WKshops Dar -8

DSCI0196

DSCI0171

Zoezi la kunyoosha mwili linalotokana na mfumo wa Yoga unaolinganisha kiwiliwili na mti (Tree Pose). Manufaa yake ni kukupa mwili usiojipinda ili kupunguza maumivu ya mgongo, kiuno na mabega. Pia husaidia akili , moyo na ari.

Baada ya semina Shule ya MwandegeWanafunzi  waliojaa hamasa  Shule ya Sekondari Mwandege, baada ya semina waliyovumilia saa tatu nzima. Mseto wa muziki, fasihi, rapu, mazoezi nk. (Picha na H. Macha)

Washiriki Bri Council mada ya Ughaibuni

Washiriki mada ya Maisha Ughaibuni, ukumbi wa British Council, wakiandika hoja. Maswali na majadiliano yalikuwa mengi. (Picha na Innocent Swai)

Mazoezi ya Kichwa- Mwandege

Mazoezi ya shingo Shule ya sekondari Mwandege yenye vidato vinne (Picha na H. Macha)

Anna Rugaba- Br CouncilAnna Rugaba wa  Lucky Magazine -Ideas for Living – lililotayarisha warsha hizi akisaidia washiriki kutoa maoni na mrejesho nyuma. (Picha na Innocent Swai)

Asha Mtwangi na mwenzake- Soma Cafe 

Washiriki Soma Cafe : Asha Mtwangi  wa Futures Group (www. futuresgroup.com) linalohamasisha vijana, afya na tamthiliya akiwa na Shanande Mushi…

Anna Rugaba akijaribu zoezi la paka- Yoga

Mshiriki na mtayarishaji Anna Rugaba wa Lucky akijaribu zoezi la kujinyoosha la Yoga mtindo wa Paka (Cat pose) ambalo husaidia viungo vingi ukiwemo mgongo, tumbo, miguu, mikono, mabega, mapigo ya moyo, kizazi na akili.

Asha Mtwangi (kushoto) na mwandishi chipukizi, Soma CafeWaliohudhuria semina Soma Cafe ambapo suala la kusoma vitabu linafanyiwa kazi na kampuni ya E & D Limited pale Mikocheni. Kushoto ni Asha Mtwangi na kulia ni mwandishi chipukizi,  Shanande Mushi.

Swai na viongozi wa Tayoa 

Innocent Swai wa Lucky Magazine- Ideas for Living- akiwa na viongozi wahamasishaji wa Tayoa (Tanzania Youth Alliance) wanaosaidia magonjwa ya zinaa katika Nyumba ya Sanaa.   Hawa walitukaribisha kwa mikono yote wakatupa ukumbi bure siku tatu. Katikati ni Meneja Mawasiliano, Benedicto Luvanda, mchapa kazi aliyehakikisha shughul hii inafanikiwa toka mwanzo hadi mwisho.

Prof Mulokozi, Soma Cafe

Kati ya wanafasihi wenye uzoefu mkubwa nchini ni Profesa Muyagbuso Mulokozi aliyehudhuria semina ya Soma Cafe. Baada ya kuwaeleza vijana kuwa mtaalamu huyu alikuwa kati ya wahamasishaji wangu wakubwa nikiwa naanza kuandika miaka ya Sabini  baadhi walikaa wakimsikiliza. Hapa Prof Mulokozi anatoa store kuhusu gwiji wa fasihi ya Kiswahili Shaaban Robert.

Ibrahim Boss -Kit drummer

Mwanamuziki mkongwe, Ibrahim Boss, aliyekuwa zamani mpiga ngoma (kit drums) bendi ya Revolutions (Kilimanjaro Hotel) miaka ya 80 alikuwepo Soma Cafe. Alisaidia pia kuchangamsha ngoma wakati  nikitumbuiza kwa gitaa na nyimbo.

DSCI0147Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mwandege Boys, Bw. Enock Walter na baadhi ya wanafunzi viongozi. Shule hii isiyotumia kengele ni kati ya shule za kipekee nchini zinazotoa elimu inayowatayarisha wanafunzi kuwa makini zaidi kinidhamu, kitabia na kiakili.

Wkshops -11

Nyumba ya Sanaa…

Muziki Mwandege Sec School

Muziki wa gitaa, mashairi na fasihi

Majadiliano Fasihi

Majadiliano kuhusu fasihi, maisha ughaibuni, afya; maswali na majibu:  Nyumba ya Sanaa…

Read Full Post »