Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Watanzania Uingereza’

 

9- Vitumbua vya Neema Kitilya

Jumuiya ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU)  ilizunduliwa kwa vigelegele na muziki mjini Northampton , katikati ya Uingereza jumamosi iliyopita. Tafrija hiyo ndogo lakini iliyowakutanisha zaidi ya Watanzania mia moja na marafiki zao wa Kenya, Uganda, Kongo , Nigeria, Uingereza nk, ilihudhuriwa na  Mheshimiwa Balozi Dk Asha Rose Migiro.

WASATU ilibuniwa mwaka jana kati ya wasanii wakiongozwa na mwanamuziki na mcheza sarakasi Fab Moses na promota wa vyakula vya Kitanzania, Bi Neema Kitilya.

Asilimia 20 ya kipato cha onesho  zilitolewa na WASATU kwa waliofikwa maafa ya mafuriko ya maji karibuni Tanzania.

1- Watanzania na marafiki zao wakijimwaga Northampton- pic by F Macha 2017

Watanzania na marafiki zao wakijimwaga ukumbi wa  The Eastern District Social Club, Northampton (more…)

Advertisements

Read Full Post »

Picha zote na Urban Pulse

1. Kadamnasi ikimsikiliza Waziri© 2013 Urban Pulse Creative_96
Kadamnasi ikimsikiliza Waziri kwa makini, ukumbi wa Ubalozi wetu London.

Wapo waliokuja kuuliza maswali. Au waliotaka tu kufahamishwa. Wapo waliojaribu kumbana Waziri wakijibishana naye masuala ya kisiasa. Wote walipewa nafasi katika hizo saa nne. Muhimu ilikua kuithamini nchi yako.
2. Evans Mela akiuliza swali© 2013 Urban Pulse Creative
Evans Mela akiuliza swali.

Balozi wetu London, Mheshimiwa Peter Kallaghe alipomkaribisha mgeni alisema hawa ni Watanzania wanaoipenda nchi yao. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mwenye miaka 58 ni mwanataaluma aliyebobea kielimu. Mbali na tuzo saba za kitaifa na kimataifa alizoshapewa ni mhariri wa jarida la kisayansi Afrika (Africa Earth Science Journal). Anaheshimika kiulimwengu na si ajabu anao wadhifa wa Makamu Rais wa Tume ya Ramani ya Madini duniani iliyoundwa 1881 Ufaransa. Lengo lake ni kuendeleza masuala ya mazingira, madini na hali ya hewa. Mtanzania huyu ni pia mwanachama wa Jumuiya mbalimbali za jiolojia, Tanzania, Marekani, China na Uingereza.
3. Balozi Kallaghe akimkaribisha Waziri kuongea na Watz UK© 2013 Urban Pulse Creative
Balozi Kallaghe akimkaribisha Waziri kuzungumza na wananchi.

Tunavyokuja kumsikiliza tunataka ukweli, maana wanayansi hawaropoki ovyo.
Lakini…
Mtanzania hahitaji usomi na taaluma pekee; anatalilia kutatuliwa matatizo ya mgao wa umeme, nyumba, chakula, kusomesha watoto wetu nk…
Na hayo sasa ndiyo ya kutafakari kuhusu makutano na Waziri Muhongo Jumanne iliyopita tarehe 26 ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania, Uingereza.
4. Prof Muhongo akiongea na Watanzania, kulia Balozi P Kallaghe © 2013 Urban Pulse Creative_99
Maongezi ya saa nne bila kupumzika. Waziri Sospeter Muhongo akiwa kazini na mwenyeji wake kando.

Waziri aligawa maongezi mafungu matatu.
1. Umeme
2. Madini
3. Maswali na majibu.
Kiwajihi na kisaikolojia hakuna hata nukta moja Mbunge huyu wa kuteuliwa alipopepesa pembeni kutazama kijikaratasi au kumwomba Katibu wake aliyeongozana naye (Bw Sosthenes Massola) amkumbushe kitu. Ni kiongozi anayefaham anachokisema. Kwa saa nne nzima takwimu, mahesabu na maelezo vilimbubujika kinywani bila kusita.
(more…)

Read Full Post »