Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Watanzania Ulaya’

 20180623_210120.jpg

Picha na Habari za Freddy Macha

 Kwa miaka mingi imesikika mikutano ya vyama na vilivyodai kushirikisha Watanzania Uingereza. Ila mwaka huu Jumuiya mpya iliyoundwa  (ATUK-” Association of Tanzania United Kingdom”)- imeahidi kuweka chombo tofauti.

(more…)

Advertisements

Read Full Post »

PICHA NA HABARI 

Za Freddy Macha

3-bango la WASATU

Jumuiya ya Wasanii Watanzania Uingereza (WASATU)  ilichemsha supu, ukumbi wa Heartlands , Birmingham, Uingereza Jumamosi iliyopita. Makutano haya yalikuwa pia sehemu ya mchango mahususi kusaidia wasichana wanaopewa mimba kabla ya kuwa watu wazima, vijijini,  Arusha. Fedha zilikusanywa na mjasiria mali mkazi wa Birmingham, Mtanzania Sia Travel. Sia alijaa mlangoni akihakikisha kila senti iiliyolipwa na wahudhuriaji watashiba chakula ,  sanaa  usiku kucha na kuwafariji vigoli wetu, Tengeru.
(more…)

Read Full Post »

 

9- Vitumbua vya Neema Kitilya

Jumuiya ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU)  ilizunduliwa kwa vigelegele na muziki mjini Northampton , katikati ya Uingereza jumamosi iliyopita. Tafrija hiyo ndogo lakini iliyowakutanisha zaidi ya Watanzania mia moja na marafiki zao wa Kenya, Uganda, Kongo , Nigeria, Uingereza nk, ilihudhuriwa na  Mheshimiwa Balozi Dk Asha Rose Migiro.

WASATU ilibuniwa mwaka jana kati ya wasanii wakiongozwa na mwanamuziki na mcheza sarakasi Fab Moses na promota wa vyakula vya Kitanzania, Bi Neema Kitilya.

Asilimia 20 ya kipato cha onesho  zilitolewa na WASATU kwa waliofikwa maafa ya mafuriko ya maji karibuni Tanzania.

1- Watanzania na marafiki zao wakijimwaga Northampton- pic by F Macha 2017

Watanzania na marafiki zao wakijimwaga ukumbi wa  The Eastern District Social Club, Northampton (more…)

Read Full Post »


Nikiwa na mwanamuziki wa Kijamaika Oneil “Lion” Kerr (Simba wa Reggae) mitaani Jumapili, jijini London, kudunda ngoma. Kutokana na kibaridi kikali cha msimu huu wa kipupwe,  mwenzangu kavalia madude mkononi. Tumejifunga makoti na kofia nzito nzito.
Mbali na kuwa sehemu ya ajira hili ni zoezi la kifani. Zamani sikuelewa nilivyowaona wanamuziki barabarani. Nilidhani “mwaga mwaga” ni kujishusha na njaa. Si jambo baya. Hukuweka karibu na watu na kukupa hisia kali kama mtumbuizaji. Kiingereza huitwa “basking”…. Ama kweli sanaa inathaminiwa sana nchi zilizoendelea.
Kifupi, kila kitu Uzunguni ni biashara.

Read Full Post »

UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI
MKUTANO MKUU 29.SEP. 2012Image
Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)  Unapenda kuwakaribisha  wanachama wote wa UTU, katika Mkutano mkuu wa UTU, utakaofanyika ukumbi Uliopo Ringstr. 109, 65479 Raunheim); Tarehe 29.09.2012, Kuanzia saa 08:00 Mchana. Tunawaomba wanachama wote  wa UTU mhudhurie katika mkutano huu muhimu. Na kwa wale ambao sio wanachama na wanahitaji kujiunga na UTU, tuandikie barua pepe kamati.utu@googlemail.com au unaweza kuwasiliana na Mwenyekiti kupitia simu ya mkononi. 0173-4298997 Karibuni sana
Ili uweze kupiga au kupigiwa kura inabidi uwe umelipia ada ya Kiingilio cha uanachama, na uwe umelipa  ada ya uanachama wa mwaka mzima.
Bank Informations
Union of Tanzania in German e.V
Acc. No.59641
BLZ 71160161
VR BANK Rosenheim-Chiemsee eG
 

 

   
   
 

Read Full Post »