Wabongo sio?
Tunasifika watu wa amani.
Miaka zaidi ya arobaini sisi tumekuwa ahueni ya majirani zetu (wakimbizi) wenye vita, tafrani, maafa na majanga. Lakini je kuwa mtu wa amani ina maana usijipende? Mbongo jipende ndugu yangu. Balozi wetu mmoja kapigwa na majambazi kule Bondeni. Watanzania wawili wakauawa Marekani mwaka juzi. Wiki iliyopita waandishi wawili wa habari wakapigwa mapanga na kumwagiwa tindikali na majambazi waliolipwa kufanya uchafu huo( na wenye mali).
Siri nini?
Jifunze kujitetea. Haina maana ukiwa mtu wa amani usijue kujilinda. Jifunze kujitetea.
La kwanza. Kumcha Mungu. Mlinzi na Muumba wetu. Muhimu. Lakini Mungu; kasema jisaidie mwenyewe na mimi n’takusaidia. Au bahati. Kuwa na bahati muhimu; ila ? Haitoshi. Kuna kukwepa majanga. Ndiyo. Je, ndumba? Hirizi, chanjo, kinga, kujilinda tokana na juju. Au elimu. Kujua mambo. Kusoma. Utaalamu. Ujinga huharibu maisha. Elimu ni silaha ya maisha na vita. Halafu kuna pesa. Lakini ukiwa na pesa kuna mawili. Kujikinga nazo au kutafutwa na kuibiwa. Pesa kuipata iko kazi. Mwisho nina hili pendekezo. Mwili wako mwenyewe. Mazoezi.
Wote tunamjua Bruce Lee. Hizi ni mashoati za Mashariki ya mbali. Je, wazifahamu? Je, una fahamu kuwa zipo nyingine nyingi, nchi mbalimbali? Mashio ati au sanaa ya kupigana husaidia akili, roho, mwili; hujenga kujiamini : kisilika na kihisia. Husaidia pia mtu kuishi marefu zaidi na kukinga baadhi ya maradhi. Masho ati pia yaweza kusaidia kukinga maisha yako ukiwa hatarini. Na ndiyo mada kuu ya hii blogu leo.
Hebu cheki hizi hapa muhimu na maarufu duniani.. Baadhi yake nimekuwekea pia video ufaidi kwa kituo zaidi.
Japani : Karate
Neno “Karate” lina maana mikono mitupu. Zipo staili chungu nzima za karate. Bongo wengi tunaifahamu Goju Ryu iliyoletwa mwaka 1973 na Mmarekani Mweusi, Bomani pale Zanaki, Dar. Goju Ryu ni mseto wa “ngumu” na “laini”… husisitiza kupigana na kushinda bila kutumia silaha yeyote.
Kwanza tazama zoezi la Karate liitwalo Kata. Ni kama dansi lakini muhimu sana:
http://uk.youtube.com/watch?v=DF7qWz7cceE&feature=related
Halafu jisomee zaidi :
Karate ipo pia Korea : Taekwando na Shotokan. Karibuni Taekwando imekua sana Bongo. Zote mbili zinaaminika kwa mateke yake ya haraka haraka. Taekwando najulikana zaidi kama mchezo hasa Olimpiki, na huwa na sheria zake.
Faidi kidogo :
http://uk.youtube.com/watch?v=CY1GqrXujOk&feature=related
Halafu Wajapani wanayo Aikido. Hii imeanza kuwa maarufu kutokana na sinema za Mmarekani Steven Seagal ingawa mwigizaji mbaya sana (mathalani siku zote yeye mbabe , na yeye tu ndiyo anashinda kwa kusema na kupigana). Aikido hutumia nguvu ya mpinzani wako kumtwanga mwenzako kwa hiyo ni nzuri sana kwa wanawake na watu wasiokuwa na miili mikubwa au musuli musuli.
Kwanza onyesho la Aikido :
Baada ya hapo sasa mtazame mwigizaji maarufu wa Kimarekani , Steven Seagal akionyesha vitu vyake wakati angali kijana darasani zamani sana:
http://uk.youtube.com/watch?v=y5dDwzwb3-8
Jisomee zaidi :
http://en.wikipedia.org/wiki/Aikido
Wajapani pia wanayo Judo ambayo ni mieleka ya urushaji na uangushaji. Lakini karibuni mseto wa Judo na Karate umeumba Jiu Jitsu ambayo hutumia pia ubinyaji wa sehemu muhimu za mwili na kumpinda adui bila kutumia maguvu. Inatumiwa sana na polisi, wanajeshi na mashushushu. Wabrazili nao wameunda JuJitsu yao ambayo ni ya kupigana zaidi chini chini, yaani ukimwangusha chini ukimkalia mpiganaji wa Ju Jitsu ya Kibrazili chini umejitakia mabaya.
Kwanza cheki sinema:
http://uk.youtube.com/watch?v=suXxYE3LFr0
Halafu jisomee zaidi:
http://en.wikipedia.org/wiki/Jujutsu
Japani ina mengi zaidi. Lakini hapa tuna gusa tu juu juu.
China: China na India ndipo vianzio vya mapigano mengi tunayoyajua. Inayofahamika zaidi ni Gung Fu ambayo Bwana Bruce Lee aliijengea sana jina. Huchezwa pia na mamonki au watawa wa dini ya Kibudhha. Mtindo huo unaitwa Shao Lin Gungu Fu. Waswahili na Waingereza tunasema Kung Fu.
Angalia:
http://uk.youtube.com/watch?v=ibiGZt9yLiQ
Kuna pia tizi hiyo hiyo lakini ya pole pole zaidi ambayo hufanywa zaidi na wazee. Usishangae kuona vijizee vya Kichina asubuhi asubuhi katika bustani vikicheza kitu kama dansi ya kijongoo na kijogoo, macho mbele, kwa mpangilio wa kigwaride. Tai Chi Chuan. Kifupi inaitwa Tai Chi. Mseto wa uvutaji pumzi, kujibalansi mwili na mapigano. Mapigano haya hufanywa na watu wa makamo kuanzia miaka 50 kuendelea hadi 100. Haina mipaka na inaendeleza sana maisha na afya.
Cheki inavyotumika katika mapigano:
http://uk.youtube.com/watch?v=5FRmv20w2UQ&feature=related
Cheki pia mseto wa Kung-fu, Wi Chun, boxing na mapigano mbalimbali ya mitaani aliyovumbua marehemu Bruce Lee. Haya ni ya haraka na kummaliza jambazi au muhuni anayejaribu kukuumiza. Yanaitwa Jeet Kune Do :
Hapa mcheki mwanafunzi wake Dan Innosanto(siku hizi mtu maarufu sana) akifundisha na Bruce Lee mwenyewe akionyesha kazi:
Thailand: Thai Boxing. Ngumi zinazochanganya pia, vigoti, vichwa, mateke, viwiko na mapigano ya haraka. Thai imechukuliwa na wazungu na kuitwa Kick Boxing. Aliyeitangaza Magharibi mwanzoni alikuwa marehemu Bruce Lee. Haya ni mapigano ya haraka sana na yanapendwa zaidi na vijana. Majuu mapigano haya yanatumiwa kupunguza vitambi na mafuta mwilini. Wanawake wengi wanachukua kick box kuondoa unene.
Cheki Thai kiduchu. Yapo pia maelezo ya asilia yake:
http://uk.youtube.com/watch?v=A0rltzN_1uc
Ubaya wake huharibu sana magoti kwa hiyo ni vigumu kwa wazee.
Philipines: Escrima, Pentak Silat. Mapigano ya Wafilipino ya kutumia visu, fimbo, chini, juu, haraka na taratibu.
Escrima pia huitwa Kali. Ni hatari sana na mtu anayejua Escrima vizuri ni kama nyoka. Bruce Lee aliipenda sana Escrima. Mmoja wa wanafunzi wake : Dan Inosanto, zambaye ni Mfilipino leo ni mwalimu mkubwa wa mseto huu, na kati wataalamu wakubwa duniani kwa mashio ati.
Cheki:
http://uk.youtube.com/watch?v=q7zlEKKA66Q
Soma zaidi:
http://en.wikipedia.org/wiki/Eskrima
India: Wahindi wengi leo hawafanyi tizi wanahusudu zaidi cricket na biashara. Lakini zamani sana inasemekana walikuwa waanzilishi wa mapigano yote hayo juu. Mashio ati inayofahamika zaidi ni ile iitwayo Kalaripayatu. Hii inasemekana ndiyo mwanzilishi wa kila kitu bara Asia. Kwa mfano nimewahi kuwaona wanawake wanaopigana wamefungwa macho. Unamkata kwa kisu anakikwepa ingawa hakuoni. Anahisi. Inafundisha mambo ya aina hiyo. Ukweli mmoja. Wanawake huwa hatari sana kwenye mafunzo yanayotumia zaidi silika na hisia.
http://www.youtube.com/watch?v=mwVjo_InpKU&mode=related&search=
Tuje Ulaya.
Ufaransa : Savate. Haya ni mapigano ya Wafaransa yanayotumia ngumi na mateke. Mateke yenyewe si tu ya kupiga kama kick box, bali pia kutega, ngwala na kutengua. Karne mbili zilizopita Savate ilikuwa ikitumiwa na wezi Ufaransa kupora. Leo mchezo wa mashioati. Ukitazama mwanzoni iko kama Kickbox lakini ukweli zinatofautiana.
Jionee mwenyewe:
http://uk.youtube.com/watch?v=WadTkRxeE5A
Brazili : Capoeira. Kapoiera ilikuzwa na watumwa wa Kiafrika waliopelekwa mkuku Brazili miaka mia tatu iliyopita. Mateso yalikuwa makubwa. Katika kujumuika na kufanya mazoezi ili kuwachapa na kupambana na wabaya wao wa Kireno ikabidi watumwa wafiche kile walichokuwa wakifanya. Kila bwana mkubwa akija wanajifanya wanapiga muziki na kuimba nyimbo. Kumbe wanajitayarisha kuwadunda. Kapoeira ilitumiwa pia katika vita vya ukombozi vilivyoongizwa na Zumbi. Huyu aliwajambisha kweli wakoloni hao.
Chombo kinachotumiwa katika Kapoeira kinafanana na ile “Mandondo” ya Kigogo; kinaitwa inaitwa Berimbau. Kapoeira ni mseto wa mateke, mieleka, sarakasi, ujanja wa kukwepa, kutania, uhuni na dansi inayokubabaisha adui. Ilipigwa marufuku na serikali ya Brazili hadi 1973. Hii leo baada ya mpira ni mchezo unaopendwa na maarufu Brazili. Ukweli uchezaji mpira wa Kibrazili unaosifika na kupendwa ulimwenguni umesaidiwa na fani mbili: muziki wa Samba na Kapoiera.
Cheki:
Kwanza cheki jamaa wakiwa kazini.
http://uk.youtube.com/watch?v=UJKR4cOt2Dc&feature=related
Halafu burudika na akina dada fiti wakisakata Samba na Kapoeira, mseto wa kila kitu:
Wengi hudhani “Breakdance” imeanzia Marekani ukweli asilia yake Kapoeira:
http://uk.youtube.com/watch?v=DdZXp0Tq6Jk&feature=related
Vale Tudo ni mapigano mengine kabambe yaliyojengwa na Wabrazili. Vale Tudo ina maana Kila Kitu Twende. Vichwa, mateke, mieleka, kung’ata, ngumi, kabali, nk.
Juu nimetaja Brazilian Ju Jitsu. Hii ni ya chini chini. Usiangushwe chini na mtu anayejua ju jitsu ya Kibrazili. Hutaamka.
Tazama Vale Tudo.
http://uk.youtube.com/watch?v=CJ01UYiLgJg&feature=related
Halafu Brazilian Jiu Jitsu.
http://uk.youtube.com/watch?v=eNR9IBuDGDc
Urusi: Systema ….
Katika mataifa yanayoaminika kwa kupigana vita duniani, ni Warusi. Walisaidia sana ushindi wa vita vya pili vya Ulaya dhidi ya manazi wa Kijerumani kati ya 1939 na 45. Warusi ni majasiri, majasiri, majasiri. Kati ya mtindo wa mapigano unaotumika hasa na wanajeshi na mashushu wao ni mashio ati ya Kirusi (Systema) iliyojengwa kama utamaduni wa mgambo (yaani kila mtu katika jamii kuijua) mamia ya miaka iliyopita. Haijulikani kabisa ulimwengu wa sasa; lakini ni kali sana. Baada ya mapinduzi ya mwaka 1917 Wakomunisti waliichukua Systema na kuifanya iwe mali ya mashushu na wanajeshi wachache. Miaka kumi na tano iliyopita mmoja wa wapiganaji hawa, mwanajeshi, Vladimir Vasiliev, alikimbilia Kanada ambapo alianza kuifundisha.
Leo Systema inasambaa Ulaya na duniani. Iko tofauti kabisa na mashio ati nyingine nilizozitaja hapo juu. Huhimiza uvutaji pumzi, kuwa laini (usisahau nyoka na wanyama ni viumbe laini sana) na kinyume na hizo mashi ati zote hapo juu si mchezo, wala wapiganaji wake hawashiriki katika mashindano maana lengo lake si kucheza bali kumaliza kazi. Tofauti kubwa ya mashio ati hii na nyingine pia ni namna inavyofundishwa. Kila kitu unachofanya unafanya kikweli kweli na kujaribu pale pale. Mathalani katika karate mtu unafanya kata na kukisia utapiganaje. Katika ngumi (boxing) unapiga begi au mchanga ilhali, Systema unajaribu lile teke lako au ngumi kama linafaa kwa binadamu mwenzako. Systema pia hufundisha kutumia silaha, si tu za kawaida kama visu bali chochote kile kama kalamu, simu ya mkononi, kitabu au kitana kujitetea maisha yako yakiwa hatarini.
Tazama wanajeshi wa Kirusi wakifanya tizi ya Systema:
http://www.youtube.com/watch?v=L__UQkPeICI&feature=related
Cheki Systema ikifundishwa kupigania chini:
Maelezo ya jamaa aliyefanya kipindi cha runinga karibuni:
http://www.youtube.com/watch?v=m1oRTEtKNsE&feature=related
Jisomee zaidi:
Wayahudi: Krav Maga.
Hii ni kiasi fulani kama Systema ( wengi wanasema imeanzia huko) ina kama miaka mia moja tu lakin si masihara. Hutumiwa na majeshi na mashushushu wa Kiizraeli. Kama Systema pia hufundisha kutumia chochote kile kiwe jiwe au meno yako kujilinda. Tofauti ya Krav Maga na mashio ati zote nyingine ni vile inavyoweza kutumiwa mara moja na vijizee, watoto, vilema, wanawake kujitetea pale pale. Mathalani kumfundisha mwanamke anayetaka kubakwa kutumbukiza vidole (wanawake wanazo kucha ndefu) ndani ya macho ya adui na kuyatumbua.
Cheki inavyotumika katika hali halisi kujikinga mijini:
http://www.youtube.com/watch?v=CgeU312nTH0&feature=related
Au Wayahudi wanavyojifunza:
Bila kusahau wapo watu mbalimbali wanaofundisha aina mbalimbali za kujihami ama na silaha au kupambana tu na wahuni na majambazi. Hawa huwa jamaa waliostaafu: wanajeshi, askari, au jamaa tu wenye uzoefu wa mapigano ya kujitetea mitaani. Hawaongelei tu nadharia ila washafanya, washaona, wana makovu na visa vya kuelezea. Kwa hiyo maarifa na elimu wanayotoa si ya vitabuni au kubuni buni:
Kwanza, visu. Kwa yeyote anayeishi Uingereza au anayefuatilia habari za jamii hii atakuwa anajua namna Kisu kilivyo silaha kuu ya wabaya wa Kitasha. Mwaka jana waliuawa watoto (au vijana) karibuni 50; kati yao asilimia hamsini waliuawa kwa visu.
Cheki hizi video kadhaa.
Huyu anawafundisha maofisa wa Polisi na kusititiza kosa linalofanywa na Masho Ati nyingi. Usikinge kisu kwa mikono. Utafiti uliofanywa unasisitiza kuwa maiti zilizouawa na visu huwa na majeruhi mikoni kutokana na marehemu kujaribu kujikinga kwa mikono anapokatwa.
Huyu chini anasisitiza kama hapo juu umuhimu wa kutojaribu kukinga kisu kwa mikono.
http://www.youtube.com/watch?v=DJGyxBgf0Is
Hawa chini wanaonyesha pia mazungumzo. Maana Masho Ati nyingi hazisisitizi umuhimu wa maongezi. Kiasi kikubwa cha mapigano huanzia katika maneno, pili majambazi hutishia kwa sauti na maneno makali yenye matusi. Cha zaidi nilichopendea video hii ni ile spidi ya mapigano. Ukweli wa hali halisi. Haraka haraka bila simile:
Hawa wanasisitiza umuhimu pia wakukimbia, ukiona huwezi (kama alivyosema marehemu Bruce Lee):
Na mwisho kabisa Bunduki. Silaha hatari kushinda zote (huyu jamaa kama sikosei kafanya Krav Maga ya Wayahudi vile vile):
Us non-swahilli speakers miss your words 😉
NIMEKUKUBALI M2 WANGU ILA TUTOE NA SISI KWENYE HIZI TRAINING IF POSSIBLE
Unene bongo ni sifa ya kuwa na hali nzuri kifedha na kimaisha.Kuna mtu mmoja nataka apite hapa apate chakula hiki
eeh bwana nbona ipo fresh sana hii makitu hata wabongo tunaweza na kujifunza tu ndio kitu kinachotakiwa au sio mazee
Ndiyo Edmundi. Inafaa. Lakini kabla ya kuanza yabidi kujua unataka kufanya nini. Ndiyo maana nimeanza kuelezea kwanza angalau kijuujuu.
JAMBO NDUGU NA DADA MUALIMU MKUU JUMA MSHABAZI http://www.jumamshabazi.webs.com
Cku zote katika maisha yng naamini hakuna mchezo wenyefaida nyingi duniani km mchezo wa ngumi 1mazoezi 2kujilinda3ajira
ASANTE SANA BROTHER KWA KUTUELEZA MENGI,NADHANI KUANZIA LEO NITAJITAHIDI KUJUA KWANI NAPENDA SANA HII MICHEZO.
HI bro nakuzungukia mara nying naomba msaada wako kuntoa nina msingi mzuri wa taichi chuan stail ya YANG hivyo kama utaweza tuanzishe kundi ili hata tupate mafunzo zaidi na kwa baadae tuwasaidie wengine pia
Athumani nimefurahi sana kusikia kuna Mtanzania anayefanya Tai Chi. Ni wazo zuri kuiendeleza kwa wenzetu waifaidi ila je, unaishi wapi?