Feeds:
Posts
Comments

https://youtu.be/jjk8Nca9sPQ

Picha na Habari za Freddy Macha

Wangapi tumewahi kusikia mashindano ya kimataifa ya mashua za upepo (“clipper race” )? Mimi sikuyajua hadi nilipomhoji Nassoro Mahruki, Mzanzibari mshiriki wa tukio hilo litakalochukua miezi kumi na moja hadi Agosti 2020.
Nassoro Mahruki ambaye huendesha shughuli zake za biashara za utalii visiwani Pemba na Unguja, ni Mwafrika Mashariki pekee na anasema alijitayarisha kwa miaka miwili kushiriki.
“Yakubidi ufanye mafunzo na kufaulu …” alisema akinionyesha mashua iitwayo “Zhuhai” ikiongozwa na nahodha Nick Leggatt. Zhuhai ni kati ya vyombo vingine kumi na moja vyenye majina kama “Korea”, “Punta Del Este”, “WTC Logistics”, nk.
Continue Reading »

https://www.youtube.com/channel/UCtVEe3zlUtuF6pTbn_OK8JQ/featured

1.

Mabango ya maonesho ya starehe na muziki mitaani London yamekuwa yakitangaza tamasha kubwa la kimataifa- Africa Uni Fest -uwanja maarufu wa Wembley Jumamosi 24 Agosti, 2019. Muziki huu wa kizazi kipya una mwakilishi kutoka Tanzania, Diamond Platnumz.

Continue Reading »

Picha na Habari za Freddy Macha

Hatimaye Watanzania Uingereza tumewachagua viongozi wa Jumuiya yetu ( Association of Tanzanians UK) yaani ATUK. Juni 2018 mkutano mkuu ulifanyika mjini Reading kufukuzia zoezi hili chini ya ulezi wa Balozi Mheshimiwa Asha Rose Migiro.
Mchecheto ulifukuzwa na wengi ila aliyewasha kiberiti alikuwa Joseph Warioba.
Baada ya mwaka, siku nzima ya Mtanzania, Jumapili 30 Juni , 2019, ilitayarishwa na wanakamati wa ATUK – ambao baadhi walikuja kuwa viongozi wa Jumuiya. Hapa inaonyesha namna juhudi za Balozi kutuunganisha zilivyoambatanika na ari na hamasa za Watanzania.
Continue Reading »

Picha na Habari za Freddy Macha

 

Siku nzima ya Mtanzania lilifana sana  wiki iliyopita (Jumapili 30 Juni, 2019),  London. Mafanikio ya shughuli yalitokana na ushirikiano wa vichwa vingi badala ya mtu mmoja( au wachache). Hafla ilihudhuriwa na kuhutubiwa rasmi na Balozi wetu Uingereza, Mheshimiwa  Asha Rose Migiro. Wenzake karibu wote ofisini pia, walikuwepo na Juma Sheha, wa kitengo cha Uhamiaji akachangia kufafanua masuala ya pasipoti mpya. Continue Reading »

 20180623_210120.jpg

Picha na Habari za Freddy Macha

 Kwa miaka mingi imesikika mikutano ya vyama na vilivyodai kushirikisha Watanzania Uingereza. Ila mwaka huu Jumuiya mpya iliyoundwa  (ATUK-” Association of Tanzania United Kingdom”)- imeahidi kuweka chombo tofauti.

Continue Reading »

PICHA NA HABARI 

Za Freddy Macha

3-bango la WASATU

Jumuiya ya Wasanii Watanzania Uingereza (WASATU)  ilichemsha supu, ukumbi wa Heartlands , Birmingham, Uingereza Jumamosi iliyopita. Makutano haya yalikuwa pia sehemu ya mchango mahususi kusaidia wasichana wanaopewa mimba kabla ya kuwa watu wazima, vijijini,  Arusha. Fedha zilikusanywa na mjasiria mali mkazi wa Birmingham, Mtanzania Sia Travel. Sia alijaa mlangoni akihakikisha kila senti iiliyolipwa na wahudhuriaji watashiba chakula ,  sanaa  usiku kucha na kuwafariji vigoli wetu, Tengeru.
Continue Reading »

1- Fab Moses akiitongoa shairi lake- Pic by F Macha.jpg

Hakuna aliyetegemea.

Kila mhusika pale alikuwa akimsalimia  Makamu wa rais, Mheshimiwa Samia Suluhu na wageni wengine. Ilipofika zamu yake mwanamuziki Fab Moses, hisia zilimkwea ghafla kama utiriri. Ingawa ki- itifaki haikupangwa, maneno na ari ya utenzi ule wa Kiswahili, (mbele ya wadau wa mataifa mbalimbali), yalichangamshaa na kupigiwa makofi na vigelegele.

Fab Moses ni msanii mwenye vipaji kadhaa ikiwemo uchezaji sarakasi, uimbaji wa nyimbo za Kiswahili,  utunzi wa muziki , tenzi, nk.

Sasa hivi ni pia mwenyekiti wa Wasanii Tanzania Uingereza (WASATU) inayotazamiwa kuendesha sherehe rasmi, ukumbi wa Heartlands, Birmingham Jumamosi ijayo, tarehe 28 April kuanzia saa moja jioni hadi tisa usiku.

Fuatilia habari zaidi Instagram

Alama Reli WASATU.

3-bango la WASATU.jpg