Picha na Habari za Freddy Macha
Siku nzima ya Mtanzania lilifana sana wiki iliyopita (Jumapili 30 Juni, 2019), London. Mafanikio ya shughuli yalitokana na ushirikiano wa vichwa vingi badala ya mtu mmoja( au wachache). Hafla ilihudhuriwa na kuhutubiwa rasmi na Balozi wetu Uingereza, Mheshimiwa Asha Rose Migiro. Wenzake karibu wote ofisini pia, walikuwepo na Juma Sheha, wa kitengo cha Uhamiaji akachangia kufafanua masuala ya pasipoti mpya.
Kila mshiriki alilipa paundi 20 tu ( kama shilingi nusu laki) kiasi kinachowezekana kwa mfanyakazi yeyote Uingereza kupata chakula, vinywaji na kusikia maelezo ya wataalamu mbalimbali asubuhi hadi usiku.
Mbali na Watanzania kuonana, tamasha lilikutanisha maarifa mbalimbali ya kisayansi, biashara, sanaa, nk. Baadhi ya wazungumzaji walirushwa moja kwa moja toka nyumbani kufafanua mada za fedha, uwekezaji, utalii na uchumi. Taswira ilionesha hali muafaka kimaendeleo, Bongo kutokana na uongozi wa Rais John Magufuli. Sehemu mosi ilikuwa majadiliano, ikafuatia sanaa na mitindo; hatimaye, jioni, chakula na densi.
Balozi alizungumza mengi ila muhimu alikumbusha Watanzania Ughaibuni kuelekeza ujuzi na uzoefu wetu nyumbani…
Dk Migiro : “Tunahitaji taaluma na weledi wenu kwa maendeleo ya taifa letu…”
Balozi wetu Uingereza, Mhe Asha Rose Migiro na Mbunifu-mitindo wa “Nyorido Fashion”, Jasmine Kissamo Assenga
Wanamuziki wa WASATU ( Wasanii Tanzania Uingereza), Saidi Kanda na Fab Moses, wakitumbuiza.
Nasriya Nassor, wa ZIPRA, alihimiza kupenda nyumbani, na “ukarimu wa wenyeji wa visiwani.” Akasema watalii si lazima wawe wageni, sisi wananchi pia.
Baadhi ya mavazi ya Kitanzania yaliyotandazwa na wajisiria mali mbalimbali wa mitindo.
Prince Katega alihimiza haja ya kuwa makini na baadhi ya dawa za kigeni zinazodhuru Watanzania. Akauliza swali kuhusu udumishaji wa tiba za kiasili Tanzania.
Wakati wa mapochopocho ya Kitanzania
Toka Ubalozi wa Tanzania, London, Juma Sheha, akifafanua ubadilishaji mpya wa pasipoti hapa na nyumbani .
Mjasiriamali na mtukuzaji mahiri wa bidhaa za Kitanzania, Hamida Mbaga (All Things African), na mmoja wa watoto walioonesha mitindo
Msemaji wa CRDB, Lucy Kimei, akitathmini kadhia za benki na fedha.
Cobby Majisu, akiuliza swali…
Balozi Migiro na Shabani Kawawa, mtoto wa mmoja wa waasisi wakuu wa TANU na Tanzania.
Huduma za vinywaji na vitafunio zikitolewa na bi Zam Zam Abdala na Sam Mbogo.
Toka kushoto. Wajasiria mali, Laila Hamza, Noeta, Anna Lukindo ( mwendeshaji wa mitindo ya “Anna Luks”) na Sia Travel (Biashara ya utalii na mwalimu wa Kiswahili )
George Mkono wa TIC (Shirika la Uwekezaji Tanzania) alifafanua kirefu sana kuhusu mchango wa walio ughaibuni kiuchumi, nyumbani.
Petronella Mlewa (wa pili kutoka kulia), anayejishughulisha sana kitaaluma na Watanzania na marafiki zao Uingereza, akiwa na baadhi ya wahudhuriaji. Wa kwanza kulia ni Neema Lake, mjasiria mali na mkazi Ufaransa.
Baadhi ya mavazi mengi ya Kitanzania, yaliyooneshwa
Mchapa kazi , Zuweina Kayugwa , akihudumia Watanzania
Washiriki, Wilkins Kiondo na David Mwakitangwe
Meza ya wanahabari. Kutoka kushoto, Simon Mzuwanda (pia mhusika mkuu wa matayarisho ya tukio), J Khamese na Deo Kamuhanda, mhariri wa gazeti la The East African
weell done.Kaka Fred
Well summarised
Keep good work well done
thanks mkuu
nimesambaza pia
Hamza
Sent from Outlook
________________________________