Mitaani na muziki wa Kizungu
Piano (au kinanda) ni chombo mahsusi cha Wazungu.
Kitaaluma muziki maana yake ni vitu vitatu : melodi (unayoisikia bila hata kujua maneno na kuipigia uluzi), ridhimu (mapigo), na mpangilio wa sauti (“harmony”). Kipengele cha tatu ndiyo kigumu zaidi….Kati ya vyombo muhimu vya kitengo cha utunzi na upangaji (“harmony”) wa muziki ni Piano na Gitaa.
Ila Piano inaongoza Uzunguni.
Ndiyo maana kila utakapokwenda, makanisani, mabaa, mashuleni, majumbani na hata vituo vya usafiri hukosi Piano. Kihistoria, watunzi mashuhuri wa muziki ulimwenguni wametumia Piano kupanga vibao vyao vilivyofahamika na kupendwa miaka mingi zaidi.
Mifano michache ni George Gershwin (“Summertime”- 1934), Stevie Wonder (“Superstition”, 1973 ), Billy Joel (“I love You Just the Way You are”- 1977) , Herbie Hancock (“Watermelon Man”, 1962), Paul McCartney ( “Nyimbo za Beatles, “Let it Be”, “Long Winding Road”, “Yesterday”, nk), Prince (”When Doves Cry”, 1984), Gill Scott Heron (Mtunzi mashuhuri wa Mashairi aliyefariki 2011), na Alicia Keys , binti , kijana anayewika sasa.
Mwandishi nikidunda Piano la Umeme na bendi ya Os Galas, Brazil, mwaka 1988.
Hata wanamuziki waimbaji walipiga piano, ingawa si sana hadharani. Prince, Michael Jackson, James Brown, nk.
Afrika yetu tunao marehem Fela Kuti na Abdullah Ibrahim (Afrika Kusini) anayeheshimika kama mmoja wa wapiga piano wakubwa duniani wa Jazz. Watanzania marehemu Patrick Balisidja na Kassim Magati (Sunburst) vile vile. Miaka yake ya mwisho marehem Balisidja alipiga Piano akiwa na King Kiki.
Kimuziki Piano ni kama kamusi. Ni muhimu kuijua kuelewa nini kinatendeka katika moyo, ngozi na mifupa ya muziki.
Kiafya upigaji Piano huoanisha pande mbili za Ubongo na kuzuia kuchakaa kwake. Hivyo kwa Wazee na watu wa makamo ni kinga maradhi ya kusinyaa na kulemaa Ubongo mathalan “Dementia” na “Alzheimer”…
Hii ni sababu mkono mmoja hufanya tendo tofauti na mwingine, unapotwanga Piano.
Kufuatana na maelezo ya mwanasayansi wa Kimarekani, Roger Sperry (aliyeshinda tuzo la Nobel 1981) upande wa kushoto wa Ubongo hufikiri, na kulia mambo ya hisia na utunzi. Bw Sperry alifikia ugunduzi huo akifanya utafiti wa kiini cha Kifafa.
Ni vizuri pia kwa watoto wadogo na huwasaidia kufanya vyema katika masomo yote. Ndiyo maana muziki na Sanaa (kijumla) huzingatiwa sana mashuleni Uzunguni.
Mwafrika jifunze Piano na wafundishe wanao muziki na sanaa.
Rick Schmull akionesha vitu
Na mdau nikionja embe.
Chini – mpiga piano na mtunzi, Billy Joel akiimba wake maarufu wa mapenzi, kimaudhui na kimuziki.
Wimbo ulifanywa maarufu zaidi na marehemu Barry White. Ulidunda sana madisko na redio za Tanzania enzi zake> Hata leo miaka 40 baadaye ungali juu.
Na chini -mpiga Piano maarufu wa Afrika Kusini, Abdullah Ibrahim. Gwiji wa jazz
Thanks for this entertaining article. How can I learn to play piano?
Wapi unaishi ndugu?