Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Watanzania Ughaibuni’

https://www.youtube.com/channel/UCtVEe3zlUtuF6pTbn_OK8JQ/featured

1.

Mabango ya maonesho ya starehe na muziki mitaani London yamekuwa yakitangaza tamasha kubwa la kimataifa- Africa Uni Fest -uwanja maarufu wa Wembley Jumamosi 24 Agosti, 2019. Muziki huu wa kizazi kipya una mwakilishi kutoka Tanzania, Diamond Platnumz.

(more…)

Read Full Post »

 20180623_210120.jpg

Picha na Habari za Freddy Macha

 Kwa miaka mingi imesikika mikutano ya vyama na vilivyodai kushirikisha Watanzania Uingereza. Ila mwaka huu Jumuiya mpya iliyoundwa  (ATUK-” Association of Tanzania United Kingdom”)- imeahidi kuweka chombo tofauti.

(more…)

Read Full Post »

PICHA NA HABARI 

Za Freddy Macha

3-bango la WASATU

Jumuiya ya Wasanii Watanzania Uingereza (WASATU)  ilichemsha supu, ukumbi wa Heartlands , Birmingham, Uingereza Jumamosi iliyopita. Makutano haya yalikuwa pia sehemu ya mchango mahususi kusaidia wasichana wanaopewa mimba kabla ya kuwa watu wazima, vijijini,  Arusha. Fedha zilikusanywa na mjasiria mali mkazi wa Birmingham, Mtanzania Sia Travel. Sia alijaa mlangoni akihakikisha kila senti iiliyolipwa na wahudhuriaji watashiba chakula ,  sanaa  usiku kucha na kuwafariji vigoli wetu, Tengeru.
(more…)

Read Full Post »

1- Fab Moses akiitongoa shairi lake- Pic by F Macha.jpg

Hakuna aliyetegemea.

Kila mhusika pale alikuwa akimsalimia  Makamu wa rais, Mheshimiwa Samia Suluhu na wageni wengine. Ilipofika zamu yake mwanamuziki Fab Moses, hisia zilimkwea ghafla kama utiriri. Ingawa ki- itifaki haikupangwa, maneno na ari ya utenzi ule wa Kiswahili, (mbele ya wadau wa mataifa mbalimbali), yalichangamshaa na kupigiwa makofi na vigelegele.

Fab Moses ni msanii mwenye vipaji kadhaa ikiwemo uchezaji sarakasi, uimbaji wa nyimbo za Kiswahili,  utunzi wa muziki , tenzi, nk.

Sasa hivi ni pia mwenyekiti wa Wasanii Tanzania Uingereza (WASATU) inayotazamiwa kuendesha sherehe rasmi, ukumbi wa Heartlands, Birmingham Jumamosi ijayo, tarehe 28 April kuanzia saa moja jioni hadi tisa usiku.

Fuatilia habari zaidi Instagram

Alama Reli WASATU.

3-bango la WASATU.jpg

 

Read Full Post »

1- Nembo ya muda ya Jumuiya - pic by F Macha 2016 Nembo iliyopendekezwa…

Jumamosi Mchana 7 Aprili ilikuwa siku ya jua kali Uingereza.  Wananchi wengi walijazana bustanini au sehemu za starehe wakiota jua na kula barafu za sukari yaani “Ice Cream.” Magari yalipiga honi, wenyeji waliheushwa na ujoto ujoto huu adimu mazingira ya Ulaya. Ndani ya ofisi ya Ubalozi wa Tanzania London, kundi la Watanzania wanane lilikaa mchana wote likijadili (kwa ari na mori) maslahi ya wananchi wenzao Uingereza. (more…)

Read Full Post »

MATUKIO MBALIMBALI MWEZI APRIL, LONDON, UINGEREZA

Naibu Balozi,Uingereza, Msafiri Marwa (kushoto) na Said Surur, Katibu Mwenezi wa Task Force ya Watanzania Uingereza (Tzuk- TF),  nje ya Westminster Abbey, Jumatatu 25 April 2016. Hii baada ya sala ya kuuombea na kuubariki Muungano wa Jamhuri ya Tanzania. Sala hii alisema , Mheshimiwa Marwa, “ ni suala la kijadi linalofanywa kila mwaka na Uingereza kwa mataifa yaliyoko jumuiya ya Madola…”

1-Msafiri Marwa na Said Surur - Westminster Abbey 2016-pic by F Macha

(more…)

Read Full Post »

Mwanamuziki na mwimbaji mashuhuri wa Tanzania, Lady JayDee, anatazamiwa kutua jijini London kesho kutwa Alhamisi tayari kwa onesho kabambe la Jumamosi.
Bango la shoo ya 5 Desemba 2015
Akizungumza nami Jumatatu usiku, promota wa shoo hilo, Frank Leo, alisema anawaomba Watanzania na marafiki zao wajiunge kumshangilia Mtanzania mwenzetu tarehe 5 Desemba. Kiingilio cha paundi 20 ( wastani wa shilingi 45,000) kitatozwa katika holi maridadi la Oasis Banqueting Suite mtaa wa Barking, Mashariki ya London.
(more…)

Read Full Post »

WAZIRI NA WENZAKE WASISITIZA HAJA YA WALOWEZI KUCHANGIA MAENDELEO BONGO
Imeandaliwa kwa ushirikiano wa Urban Pulse na Freddy Macha

Watanzania waliokuwepo wakichangamkia maongezi

Watanzania wakazi Uingereza wamehakikishiwa kuwa taaluma na uzoefu wao ughaibuni vitasaidiwa na vyombo husika vya serikali wakirejea na zana, mbinu na uwekezaji wa kilimo.
Kauli hii ilitolewa na msafara mzima wa viongozi uliofuatana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza alipokutana na Watanzania Ubalozini, London , Jumatano iliyopita.
Mininster Eng Chiza speaks at TZ Embassy UK-pic by Urban Pulse
Waziri Chiza alisema akiwa mtoto wali uliliwa siku za sikukuu tu. Leo mengine. Mchele unapandwa zaidi na bado hautoshi.

(more…)

Read Full Post »

Imeandikwa kwa ushirikiano wa Urban Pulse na Freddy Macha

Mara ya mwisho Tanzania kusikika kimataifa michezoni ilikuwa 1980 wakimbiaji Filbert Bayi na Suleiman Nyambui walipotwaa medali za Olimpiki, Moscow na timu yetu ya taifa ya mpira iliposhiriki fainali za kombe la Afrika mjini Lagos , Nigeria…
kids playing football at Academy of Light-oic by Urban Pulse
Watoto wadogo wakisakata gozi Academy of Light. Samaki mkunje angali mbichi…

Kiu ya miaka 30 imezungumziwa na kujadiliwa sana hatimaye tumeanza kuzoea kushangilia wengine. Tumezoea mtazamo huu kiasi ambacho ni rahisi kwa shabiki wa Kitanzania kuijua timu nzima ya wachezaji wa Manchester United au Barcelona kuliko Yanga na Simba.
Kati ya sababu kuu za kushindwa huku kila mwaka ni kutowekezea katika matayarisho na kutochangamkia tulicho nacho. Wenzetu wa Hispania, Brazil, Uingereza, Nigeria, Ivory Coast, Kenya nk wanatuzidi moja. Wanajipenda.
Ramani ya chuo kitakachojengwa Dar es Salaam
Rais akionyeshwa ramani ya mpango wa chuo cha mpira kitakachojengwa Dar es Salaam.
Sisi (kama hawa wenzetu) tunao wachezaji wenye vipaji. Tunao pia uchungu kwa nchi yetu; na kama alivyosema Rais Jakaya Kikwete alipoitembelea klabu ya Sunderland AFC Jumapili 16 , Juni, “Watanzania tunapenda michezo.”
(more…)

Read Full Post »

Picha zote na Urban Pulse

1. Kadamnasi ikimsikiliza Waziri© 2013 Urban Pulse Creative_96
Kadamnasi ikimsikiliza Waziri kwa makini, ukumbi wa Ubalozi wetu London.

Wapo waliokuja kuuliza maswali. Au waliotaka tu kufahamishwa. Wapo waliojaribu kumbana Waziri wakijibishana naye masuala ya kisiasa. Wote walipewa nafasi katika hizo saa nne. Muhimu ilikua kuithamini nchi yako.
2. Evans Mela akiuliza swali© 2013 Urban Pulse Creative
Evans Mela akiuliza swali.

Balozi wetu London, Mheshimiwa Peter Kallaghe alipomkaribisha mgeni alisema hawa ni Watanzania wanaoipenda nchi yao. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mwenye miaka 58 ni mwanataaluma aliyebobea kielimu. Mbali na tuzo saba za kitaifa na kimataifa alizoshapewa ni mhariri wa jarida la kisayansi Afrika (Africa Earth Science Journal). Anaheshimika kiulimwengu na si ajabu anao wadhifa wa Makamu Rais wa Tume ya Ramani ya Madini duniani iliyoundwa 1881 Ufaransa. Lengo lake ni kuendeleza masuala ya mazingira, madini na hali ya hewa. Mtanzania huyu ni pia mwanachama wa Jumuiya mbalimbali za jiolojia, Tanzania, Marekani, China na Uingereza.
3. Balozi Kallaghe akimkaribisha Waziri kuongea na Watz UK© 2013 Urban Pulse Creative
Balozi Kallaghe akimkaribisha Waziri kuzungumza na wananchi.

Tunavyokuja kumsikiliza tunataka ukweli, maana wanayansi hawaropoki ovyo.
Lakini…
Mtanzania hahitaji usomi na taaluma pekee; anatalilia kutatuliwa matatizo ya mgao wa umeme, nyumba, chakula, kusomesha watoto wetu nk…
Na hayo sasa ndiyo ya kutafakari kuhusu makutano na Waziri Muhongo Jumanne iliyopita tarehe 26 ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania, Uingereza.
4. Prof Muhongo akiongea na Watanzania, kulia Balozi P Kallaghe © 2013 Urban Pulse Creative_99
Maongezi ya saa nne bila kupumzika. Waziri Sospeter Muhongo akiwa kazini na mwenyeji wake kando.

Waziri aligawa maongezi mafungu matatu.
1. Umeme
2. Madini
3. Maswali na majibu.
Kiwajihi na kisaikolojia hakuna hata nukta moja Mbunge huyu wa kuteuliwa alipopepesa pembeni kutazama kijikaratasi au kumwomba Katibu wake aliyeongozana naye (Bw Sosthenes Massola) amkumbushe kitu. Ni kiongozi anayefaham anachokisema. Kwa saa nne nzima takwimu, mahesabu na maelezo vilimbubujika kinywani bila kusita.
(more…)

Read Full Post »

Older Posts »