TAREHE 29 OKTOBA, 2010….
Kuunganisha chuo cha SOAS na jumuiya ya Wazungumzaji KISWAHILI Uingereza…
‘Milima haikutani, bali wanadamu hukutana’
Sherehe itafanywa wapi?
Chumba cha G50, SOAS, Russell Square,
Thornhaugh Str.
London WC1H OXG
Saa moja jioni – MBili na nusu usiku. Kiingilio BURE. Karibuni
FAROUK TOPAN, mhadhiri wa KIswahili atafungua dimba la SWAHILI SOCIETY. Uzinduzi utatangaza rasmi tovuti ya Kiswahili:
‘www.swahilisociety.com‘
SHEIKH MBARAK ataongelea kuhusu ” Maisha ya Kiswahili Nje ya Afrika, mjini London.”
FREDDY MACHA atawasilisha mada kuhusu ‘ Mzizimo wa Jumuiya ya Kiswahili Mtandaoni”‘
SOKO, wauzaji wa mavazi ya Kitanzania , wataonyesha walicho nacho.
Mgawaha wa KILIMANJARO utauza Chakula cha Kiswahili
Mwishowe bendi ya KITOTO, itatumbuiza ukumbi wa JCR kuanzia saa tatu usiku.
Mtangazaji na mwanahabari, Ayoub Mzee toka Swahili Diaries SKY news, atawakilisha habari hizi!
KARIBUNI!!!
Habari zaidi ongea na Jason Tuff (pichani chini) akiwa Mdawi, Kilimanjaro, alikokuwa akifanya mazoezi ya Kiswahili…
Jason ni mmoja wa Waingereza wanaopigania hadhi ya Kiswahili nje ya Bongo na mchangiaji wa klabu hii mpya ya Waswahili SOAS.
Simu…. +44-7816-642296
Barua pepe : 212894@soas.ac.uk
Read Full Post »