Si wanamuziki wengi wanaoishi ughaibuni toka Bongo. Miaka mingi hata hivyo amekuwepo mtunzi na mwimbaji, Fab Moses , CD na shoo yake inayoitwa NENGUA.
Mtazame katika tovuti ya My Space:
http://vids.myspace.com/index.cfm?fuseaction=vids.individual&VideoID=42998197
Mbali na nyimbo zake mathalani: “Ngunguri Ngangari” na “Nyerere” , Fab Moses huonekana katika majukwaa kadhaa ya London akitungua nyimbo mbalimbali za Kiswahili na bendi mashuhuri ya Afrika Jambo. Bendi hii inasimamiwa na magwiji Kawele “Finger Printer”Mutimanwa, mpiga gitaa mashuhuri wa Kikongo, Uingereza na Ramadhani Athumani Mtunguja (“Rama Sax”) mpiga saxafoni mzawa wa Tanga aliyekuwa zamani na Simba wa Nyika na Les Wanyika na kushikiri katika kibao maarufu Sina Makosa kilichotolewa Nairobi mwaka, 1978. Afrika Jambo hutumbuiza klabu kadhaa mashariki ya London zikiwemo (East Side Bar, Ilford) Kila Jumapili na Railway Tavern klabu ya Waganda, Forest Gate.
Waliomsikia Fab Moses huvutiwa na uzuri wa sauti yake inayokumbusha vibao mbalimbali vya nyumbani kama nyimbo za Shabani Marijani (Georgina), Simba wa Nyika, Mlimani Park, nk. Moja ya Sifa anazopewa Fab Moses ni sauti inayolandana sana na ya mwanasokomoko, hayati Marijani.
Mwanamuziki Fab Moses ni vile vile mwanasarakasi wa siku nyingi aliyeshafanya kazi na vikundi kadhaa nyumbani ikiwepo Muungano (cha Mzee Nobert Chenga) na Black Eagles. Kwa takribani miaka minane sasa anaongoza kikundi chake cha sarakasi na michezo jukwaani kinachoitwa Highflyers. Walioshamshuhudia (nikiwemo) wanakubali Fab Moses ni mwalimu na kocha mzuri sana wa Sarakasi. Chini ya utaalamu wake mtu yeyote (watoto kwa wazima) anaweza kufundishwa kujinyonga nyonga na kuwa mwanasarakasi. Hilo latokana na uvumulivu na ufundi wake, Mtanzania huyu mwenye vipaji vingi…
Habari zaidi za NENGUA, kikundi cha Sarakasi (Highflyers) au Afrika Jambo; mpigie Fab Moses -+44-7950-604530
Barua pepe: fabrahs@yahoo.co.uk
Picha na Freddy Macha
Read Full Post »