Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘All Things African’

https://www.youtube.com/channel/UCtVEe3zlUtuF6pTbn_OK8JQ/featured

1.

Mabango ya maonesho ya starehe na muziki mitaani London yamekuwa yakitangaza tamasha kubwa la kimataifa- Africa Uni Fest -uwanja maarufu wa Wembley Jumamosi 24 Agosti, 2019. Muziki huu wa kizazi kipya una mwakilishi kutoka Tanzania, Diamond Platnumz.

(more…)

Read Full Post »

PICHA NA HABARI 

Za Freddy Macha

3-bango la WASATU

Jumuiya ya Wasanii Watanzania Uingereza (WASATU)  ilichemsha supu, ukumbi wa Heartlands , Birmingham, Uingereza Jumamosi iliyopita. Makutano haya yalikuwa pia sehemu ya mchango mahususi kusaidia wasichana wanaopewa mimba kabla ya kuwa watu wazima, vijijini,  Arusha. Fedha zilikusanywa na mjasiria mali mkazi wa Birmingham, Mtanzania Sia Travel. Sia alijaa mlangoni akihakikisha kila senti iiliyolipwa na wahudhuriaji watashiba chakula ,  sanaa  usiku kucha na kuwafariji vigoli wetu, Tengeru.
(more…)

Read Full Post »

fab-moses-a-r-migiro-na-saidi-kanda-pic-by-f-macha-2016

Mcheza  Sarakasi na mwanamuziki Fab Moses na mwenzake mwana muziki nguli Saidi Kanda wakiwa na Mheshimiwa Balozi, Asha Rose Migiro baada ya kikao cha Jumatano iliyopita London.

Wasanii wanane waligonga milango ya Bond Street. Ikafunguliwa. Wakakaribishwa. Msaidizi wake mheshimiwa akawataka kukaa. Kaeni. Bw Allen Kuzilwa huyo.. Juu  ghorofa ya kwanza. (more…)

Read Full Post »

All Things African-2

Si wengi wanaifahamu All Things African. Kampuni hii ndogo ya wanawake Uingereza imeanza kujenga jina kutokana rangi zake zenye bendera ya Tanzania na wanawake wachapa kazi wanaoongozwa na Hamida Mbaga. Jumamosi tarehe 5 Desemba 2015, All Things African, iliyapamba mazingira ya maonesho yake mwanamuziki Lady JayDee alipotumbuiza holi la Oasis, kitongoji cha Barking , mashariki ya London. Maonesho hayo yalitayarishwa na Upendo Events. Ushirikiano wa makampuni haya mawili unadhihirisha dira njema ya kazi na biashara baina ya Watanzania ughaibuni. Hali kadhalika wakati wa karamu ya kusheherekea miaka 40 kati ya Tanzania na Uingereza (British Tanzania Society) All Things African ilikuwa na meza yenye bidhaa mbalimbali za Kitanzania na Afrika mjini Reading.
1- All things African - models and Admn- pic by F Macha 2015
Warembo, wafanyakazi, wasanii na wapambaji wa “All Things African” wakijivunia bendera ya Tanzania, kimavazi.
(more…)

Read Full Post »

Mwanamuziki na mwimbaji mashuhuri wa Tanzania, Lady JayDee, anatazamiwa kutua jijini London kesho kutwa Alhamisi tayari kwa onesho kabambe la Jumamosi.
Bango la shoo ya 5 Desemba 2015
Akizungumza nami Jumatatu usiku, promota wa shoo hilo, Frank Leo, alisema anawaomba Watanzania na marafiki zao wajiunge kumshangilia Mtanzania mwenzetu tarehe 5 Desemba. Kiingilio cha paundi 20 ( wastani wa shilingi 45,000) kitatozwa katika holi maridadi la Oasis Banqueting Suite mtaa wa Barking, Mashariki ya London.
(more…)

Read Full Post »