Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Watanzania London’

Joyce Materego na jarida zenye habari hizo- pic by F Macha 2017

Baada ya kuhitimu masomo ya Uhasibu miaka zaidi ya kumi iliyopita, Joyce Materego alitulia kazini. Karibuni alikuwa Mwafrika pekee kati ya wataalamu wengine ndani ya Sekta yake kupewa zawadi ya ufanisi.

Mahojiano  na KSTL (Kwa Simu Toka London) yanatumegea ndogo ndogo…

Advertisements

Read Full Post »

Picha na Habari za Freddy Macha

 

Kila mwaka wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Ubalozi wa Tanzania huchagua usiku mmoja ambapo wananchi wa madhehebu yote hualikwa kufuturu.  Jumamosi 10 Juni, 2017 shughuli hii haikufanywa Ubalozini, wala haikuwa ya bure. Washiriki tulitakiwa kuchangia pauni 10 (kama shilingi 25,000) kutopoteza kodi za wananchi nje. Si kiasi kikubwa na kina mama nao walijitolea kupika na mikeka kukalia.

Pili,  mkutano wa takriban saa 3 na nusu uliwakutanisha Watanzania na Balozi Asha Rose Migiro kutathmini mada mbali mbali muhimu kabla ya kula. Desturi hii  ni ya kipekee kwa Watanzania na sijawahi kusikia ikifanywa na mataifa mengine. Zingatia pia kuwa kikao kilifanywa kanisa la Monravia, Hornsey kaskazini ya London.

(more…)

Read Full Post »

MATUKIO MBALIMBALI MWEZI APRIL, LONDON, UINGEREZA

Naibu Balozi,Uingereza, Msafiri Marwa (kushoto) na Said Surur, Katibu Mwenezi wa Task Force ya Watanzania Uingereza (Tzuk- TF),  nje ya Westminster Abbey, Jumatatu 25 April 2016. Hii baada ya sala ya kuuombea na kuubariki Muungano wa Jamhuri ya Tanzania. Sala hii alisema , Mheshimiwa Marwa, “ ni suala la kijadi linalofanywa kila mwaka na Uingereza kwa mataifa yaliyoko jumuiya ya Madola…”

1-Msafiri Marwa na Said Surur - Westminster Abbey 2016-pic by F Macha

(more…)

Advertisements

Read Full Post »

PICHA ZOTE NA F MACHA…

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewahakikishia Watanzania na wageni kwamba jitihada zitaendelea kufanywa na serikali kuboresha usafiri Bongo.

Sista Lucia wa kanisa la Wakatoliki aliyeshaishi Tanzania akiuliza maswali kuhusu ajali ya meli Zanzibar wakati wa mkutano wa Central Hall, Westminster.

Akiongea mjini London juzi katika “mkutano wa mwaka” wa jumuiya ya Watanzania na Waingereza (Britain-Tanzania Society) na Mfuko wa Udhamini wa Maendeleo (Tanzania Development Trust), alisema bado pana mengi sana ya kufanya toka ateuliwe miezi minne iliyopita.
Waziri Mwakyembe vile vile alifafanua kuhusu majadiliano ya katiba mpya inayotegemewa kutajwa mwaka 2015.

Dk Mwakyembe akisikiliza hoja mbalimbali kwa makini kutoka kwa wananchi na wageni ughaibuni wanaolilia shida za usafiri Bongo.

Akijibu maswali toka kwa Wazungu na Watanzania waliohudhuria kikao Central Hall, Westminster, hatua chache karibu na Ikulu ya Uingereza (Whitehall), Mwakyembe ambaye ni mbunge wa Kyela, alifahamisha kuwa moja ya tatizo lililojaribu kutafutiwa ufumbuzi karibuni ni kuzorota kwa bandari ya Dar es Salaam. Alisema Wizara ilibidi kubadili uongozi wa bandari hiyo baada ya ripoti ya kimataifa iliyoichamba Dar kuwa moja ya bandari mbaya duniani zisizotekeleza kazi zake sawasawa.
“Bandari ya Dar es Salaam ina uwezo wa kulisha uchumi wa nchi nzima ikiendeshwa vyema,” aliueleza mkutano uliomsikiliza kwa makini. “Tumezungukwa na nchi nyingi zisizo na bahari ambazo zinatutegemea kusafirisha mizigo yake. Kwa hiyo basi, wizara ya uchukuzi ikilala na taifa zima linalala.”
(more…)

Advertisements

Read Full Post »


Utamaduni na sanaa ya Mtanzania vimewasisimua watazamaji waliohudhuria maonyesho ya mchoraji Raza Mohammed mjini London.
Wenyeji wanaoendelea kuhudhuria maonyesho hayo yaliyoanza rasmi Ijumaa iliyopita katika jumba la Charlton House, Greenwich, kusini ya London wameelezea kuupenda wajihi wa Tanzania hapa ughaibuni.
Ofisa mhusika katika jumba hilo lilojengwa na Mfalme James wa kwanza mwaka 1607 kasema hii ni mara ya kwanza kwa Mwafrika kuonyesha sanaa ya uchoraji ndani ya mgahawa wa Mulberry ndani ya kasri hili la kihistoria.

Kaimu Balozi wa Tanzania, Uingereza, Bwana Chabaka Kilumanga (kushoto) akizungumza na wasanii Raza Mohammed na mwanae Eddy Raza, usiku huo mwanana

Akifungua maonyesho hayo kwa niaba ya serikali, Kaimu Balozi wa Tanzania Uingereza, Mheshimiwa Chabaka F. Kilumanga alilishukuru shirika la Global Fusion Music and Arts (GFMA) chini ya uongozi wa Louisa Le Marchand kwa kusaidia kutayarisha shughul hii.
Bwana Kilumanga alisema Raza alialikwa Uingereza awali kusaidia sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Bongo.
(more…)

Advertisements

Read Full Post »


Vielelezo vya kitabu cha hadithi za Daudi vilivyosanifiwa na Raza kufundishia Kiingereza mashuleni Bongo, miaka ya 80…

Mchoraji, msanii, mpambaji wa taswira, vitabu na stempu, Raza Mohamed anatazamiwa kufanya maonyesho ya picha zake katika ukumbi wa Mulberry Tea Room, Charlton House, kitongoji cha Greenwich, London, Ijumaa tarehe 17 Juni hadi Jumatano 20, Julai mwaka huu.
Msosi wa Biriani, kachumbari, pilipili, nyama kwa nazi aliopika binti yake Raza kutukaribisha wakati wa mahojiano jana. Ama kweli kila jambo katika ukoo huu lina tone na wajihi sanifu…

Charlton House ni kasri kubwa la kale lililojengwa karne ya 17 enzi za utawala wa mfalme James wa Kwanza. Lina miti, bustani kubwa maridadi, maktaba, maonyesho ya muziki, vyumba vya masomo mbalimbali, vyumba vya mikutano na mgahawa. Ni jengo linalotukuza utamaduni, elimu, burudani, historia na mila ya Waingereza na wageni wao, hasa wakazi wa Greenwich.

Charlton House

Kifupi, ni mahali pa hadhi. Raza na mwanae kukubaliwa kuonyesha kazi zao hapa ni heshima kubwa kwa jina la Watanzania wote. Ni mabalozi wanaowakilisha taifa kwa sanaa yao ya picha tupu.


Raza na picha ya “Watoto wakicheza Mdaku” iliyopikwa Unguja. Picha na F Macha.

Raza Mohamed ambaye ni hazina ya taifa letu amekuwa akichora toka akiwa mtoto wa miaka sita tu mwaka 1952. “Nilianza kwa mkaa…” alisema nilipomhoji nyumbani kwa mwanae, jana. (more…)

Advertisements

Read Full Post »