Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Jumuiya Ya Madola’

Picha na Habari za Freddy Macha

1- Mhe Suluhu Samia akisalimiana na Dk Miohammed Hamza - pic by F Macha 2018Makamu wa Rais Mhe Suluhu Samia akizungumza na Dk Mohammed Hamza, kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Uingereza

Ulikuwa mkutano mfupi uliokusudia kutoa shukrani kwa wafadhili na Watanzania London wanaosaidia nyumbani. Fadhila hupitia Jumuiya ya Waingereza na Watanzania  (BTS) na kitengo chake cha TDT = shirika la Mfuko wa Maendeleo Tanzania.  BTS ilianzishwa mwaka 1975, na mlezi wake sasa hivi ni Rais mstaafu Ali Mwinyi.

BTS ilimkaribisha Makamu wa Rais Mheshimiwa Suluhu Samia, aliyekuja London wiki hii kudhuruia mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Madola.

Kawaida viongozi hutegemewa  hotuba ndefu zenye maelezo yanayochosha masikio.

Mhe Suluhu alitua chuo kikuu cha lugha za Afrika na Mashariki ya Kati (SOAS)  akasalimiana na kupeana mikono na wananchi wa pande zote mbili. Hiyo tu ilitosha kuonesha imani yake kwa wananchi wachapa kazi wa pande hizi mbili.

2-Balozi Dk Asha Rose Migiro akizungumza na Kaimu Balozi Dar es Salaam Marc Thayre- pic by F Macha 2018Balozi wetu Uingereza, Dk Asha Rose Migiro akiwa na Kaimu Balozi Uingereza Tanzania, Mhe Marc Thayre

3- Dk Andrew Coulson mwenyekiti wa BTS aliyefungua na kufunga kikao- pic by F Macha 2018Mwenyekiti wa Jumuiya Ya Uingereza na Tanzania – BTS. Dk Andrew Coulson aliyefungua na kufunga kikao cha Brunei Gallery, SOAS.

4-Baadhi ya Watanzania waliohudhuriaBaadhi ya Watanzania waliohudhuria. Kutoka kushoto, Kiondo Wilkins, Dk Alex Paurine, Simon Mzuwanda na Joe Warioba
 

 

Read Full Post »