WAZIRI NA WENZAKE WASISITIZA HAJA YA WALOWEZI KUCHANGIA MAENDELEO BONGO
–Imeandaliwa kwa ushirikiano wa Urban Pulse na Freddy Macha
Watanzania wakazi Uingereza wamehakikishiwa kuwa taaluma na uzoefu wao ughaibuni vitasaidiwa na vyombo husika vya serikali wakirejea na zana, mbinu na uwekezaji wa kilimo.
Kauli hii ilitolewa na msafara mzima wa viongozi uliofuatana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza alipokutana na Watanzania Ubalozini, London , Jumatano iliyopita.
Waziri Chiza alisema akiwa mtoto wali uliliwa siku za sikukuu tu. Leo mengine. Mchele unapandwa zaidi na bado hautoshi.
(more…)