Feeds:
Posts
Comments

Joyce Materego na jarida zenye habari hizo- pic by F Macha 2017

Baada ya kuhitimu masomo ya Uhasibu miaka zaidi ya kumi iliyopita, Joyce Materego alitulia kazini. Karibuni alikuwa Mwafrika pekee kati ya wataalamu wengine ndani ya Sekta yake kupewa zawadi ya ufanisi.

Mahojiano  na KSTL (Kwa Simu Toka London) yanatumegea ndogo ndogo…

Habari na Picha za Freddy Macha

TUMEZOEA kuwaita wenye hali hii “taahira” – neno la asili ya Kiarabu lenye maana “mtu asiye sawa” (wazimu, chizi, bwege, nk). Ila sahihi ni “mtindio ubongo” – kwa Kiingereza “Down Syndrome”….
Continue Reading »

Picha na Habari za Freddy Macha

 

Kila mwaka wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Ubalozi wa Tanzania huchagua usiku mmoja ambapo wananchi wa madhehebu yote hualikwa kufuturu.  Jumamosi 10 Juni, 2017 shughuli hii haikufanywa Ubalozini, wala haikuwa ya bure. Washiriki tulitakiwa kuchangia pauni 10 (kama shilingi 25,000) kutopoteza kodi za wananchi nje. Si kiasi kikubwa na kina mama nao walijitolea kupika na mikeka kukalia.

Pili,  mkutano wa takriban saa 3 na nusu uliwakutanisha Watanzania na Balozi Asha Rose Migiro kutathmini mada mbali mbali muhimu kabla ya kula. Desturi hii  ni ya kipekee kwa Watanzania na sijawahi kusikia ikifanywa na mataifa mengine. Zingatia pia kuwa kikao kilifanywa kanisa la Monravia, Hornsey kaskazini ya London.

Continue Reading »

Janet Chapman ni kati ya Waingereza wanaojitolea (bila mshahara au malipo ),  miaka mingi kujaribu kusaidia Afrika, hususan Tanzania. Akiwa mwanachama wa Shirika la Misaada ya Maendeleo Tanzania (TDT) na Jumuiya ya Waingereza na Watanzania (BTS) karibuni amejihusisha na suala la kutokomeza Ukeketaji. Katika mahojiano na “Kwa Simu Toka London” Mei 11, 2017 anafafanua mradi mpya wa kujenga ramani vijijini Tanzania, yaani “Mapping”. Je maana  na faida yake ni ipi?   Kufaidi zaidi mahojiano bofya CC  dirisha la You Tube upate maelezo yaliyoandikwa kitaaluma kuelewa kinachosemwa.

The Strand London- pic by F Macha 2016

Ndogo Ndogo Mitaani Ulaya

Wazungumzaji , wanafunzi na wapenzi wa Kiswahili  wana-arifiwa safu mpya ya mwandishi Freddy Macha.

Baada ya miaka mingi akitathimini, kutafiti  na kutangaza habari, fasihi na makala, ameanzisha kipindi kipya (cha Video)  mtandaoni.

https://www.youtube.com/channel/UCtVEe3zlUtuF6pTbn_OK8JQ

Ndiyo nini?

“Kwa Simu Toka London” siyo toleo la hali ya juu au kustaajabisha. Macha anatumia weledi na ujuzi wake  kuelezea -kupitia simu ya mkononi- kadhia mitaani, maholi na majumbani,  London, na kwingineko anakotembelea Ughaibuni.  Teknolojia inakayotumika ni ya kawaida tu kwa chombo hiki tulichokizoea siku hizi. Continue Reading »

 

Ukumbi wa The Eastern District Social Club, Northampton haujulikani kwa wengi. Hata hivyo eneo hili nje kidogo ya mji, ulijikuta ukikaanga Maandazi , Vitumbua na Nyama Choma punde Wasanii mseto wa Kitanzania walipozindua WASATU – jumuiya ya kuwakutanisha na kuwaunganisha. Ilikuwa Jumamosi 1 April, 2017.
Wimbo maarufu wa Les Wa Nyika, SINA MAKOSA, uliotungwa na Omari Shaaban, kuimbwa na Issa Juma na kupambwa gitaa maridadi la John Ngereza, ulikuwa kati ya vibao mbalimbali vya Kiswahili vilivyotukumbusha tukokako, na tu wapi, duniani. Umoja ni nguvu. Kiswahili oyee! Tanzania Oyee! Afrika Mashariki na Kati oyee!

 

9- Vitumbua vya Neema Kitilya

Jumuiya ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU)  ilizunduliwa kwa vigelegele na muziki mjini Northampton , katikati ya Uingereza jumamosi iliyopita. Tafrija hiyo ndogo lakini iliyowakutanisha zaidi ya Watanzania mia moja na marafiki zao wa Kenya, Uganda, Kongo , Nigeria, Uingereza nk, ilihudhuriwa na  Mheshimiwa Balozi Dk Asha Rose Migiro.

WASATU ilibuniwa mwaka jana kati ya wasanii wakiongozwa na mwanamuziki na mcheza sarakasi Fab Moses na promota wa vyakula vya Kitanzania, Bi Neema Kitilya.

Asilimia 20 ya kipato cha onesho  zilitolewa na WASATU kwa waliofikwa maafa ya mafuriko ya maji karibuni Tanzania.

1- Watanzania na marafiki zao wakijimwaga Northampton- pic by F Macha 2017

Watanzania na marafiki zao wakijimwaga ukumbi wa  The Eastern District Social Club, Northampton Continue Reading »

5-Bango la shughuli

UZINDUZI WA WASATU LEO UINGEREZA KWA MUZIKI

Jumuiya ya Wasanii wa Tanzania Uingereza (WASATU) leo inazinduka kwa onesho la muziki Northampton.

Onesho hilo litajumuisha wanamuziki wakongwe wa Kitanzania wakiwemo Saidi Kanda ( na bendi Mvula Mandondo), mwimbaji sauti chiriku Fab Moses na bendi ya Afrika Jambo ikihusisha mpiga sax RamaSax. Ramasax aliwahi kupuliza “madude” na Simba wa Nyika. Mwingine ni mpiga gitaa Kawele Mutimanwa aliyeshiriki wimbo maarufu wa Mambo Bado na bendi ya Makassy miaka ya 80. Wengine ni pia wanamuziki walemavu kama  mpiga gitaa John Londo, Kea nk…

Mwenyekiti wa WASATU, Bi Neema Kitilya , mcheza dansi, Khadija ( Kibisa zamani) wasanii wengine wameeelezea mori wao kutangaza na kujumuiha wasanii wetu duniani.
TUTAWALETEA HABARI ZAIDI INSHALLAH MUNGU AKIPENDA

Tuko pamoja!

Tanzania oyeee !!!

Picha na Habari za Freddy Macha, London

1-balozi-migiro-akihutubia-jumuiya-ya-watanzania-na-waingereza-pic-by-f-macha

 Balozi wetu Uingereza, mheshimiwa Dk Asha Rose Migiro alihutubia  jumuiya ya Watanzania na Waingereza (British Tanzania Society- BTS)  Jumamosi iliyopita. Hotuba hiyo iliyofanyika ukumbi wa Central Hall Westminster, London ni mara ya pili kwa balozi huyu mgeni kukutana na BTS. Mwezi Julai alikaribishwa rasmi akiwa na Balozi mpya Uingereza Tanzania Bi Sarah Cooke na aliyestaafu, Bi Diana Melrose.

8-bango-la-bts-pic-by-f-macha-2016

Mada hiyo iliyoitwa “Maendeleo ya Sasa Tanzania”  Ilikuwa sehemu ya mkutano wa 41 wa mwaka wa BTS na kuhudhuriwa na Watanzania na Waingereza wakazi hapa. Continue Reading »