Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Fasihi ya Kitanzania’

Miriam-Kinunda_TasteOfTanzania_blogs

WATANZANIA hatuna tabia ya kusoma wala kuandika. Waandishi wachache waliopo ama hufanya kwa masomo (kupata shahada) au hadithi za chap chap zinazolipuliwa kupata fedha na umaarufu wa haraka haraka. Katika fani za kitaaluma pia tumezorota. Wageni (hasa Wazungu) wameandika kuhusu mavazi yetu( mathalan kanga), mila, desturi, imani, maradhi, wanyama, nk. Hatuandiki kuhusu mambo tunayoyafanya wenyewe kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo. Tunangojea tuandikiwe na wageni. Tumejaa uvivu, kutojali…nk
Vyombo vya habari tu ndivyo vinategemewa kuweka kumbukumbu. Na hivi vimeishia kulipua. Lugha ya wanahabari wanaonza leo hairidhishi kwa kuwa hawasomi. Mabloga wengi wananukuu tu na kunyofoa kazi za wenzao na kuzitoa upya. Mwanahabari apaswa kusoma kitabu kimoja kwa mwezi kuboresha nahau, maudhui, msamiati, maarifa nk.
Taaluma ya upishi ni muhimu sana. Taaluma hutaka utafiti na kazi.
(more…)

Read Full Post »