Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Unyago’

Zamani nikidhani sisi Wamatumbi ndiyo mabingwa wa kukatika viuno. Lakini  miaka inavyokwenda ndivyo nazidi kuona  baadhi ya tabia na desturi nyingi zetu zikidakwa, zikiigwa na wenzetu wa mataifa mengine. Kumbe pia si tu kuigana, tamaduni nyingine pia zina mikatiko. Kifupi, kuna viuno aina nyingi.

Kwa madem wa Kizungu hutumia sehemu nyingine za mwili kama mikono na miguu badala kuzingatia sana nyonga. Hii inatokana na utamaduni wao wa densi kama “Ballet” ambayo hailengi sana kiuno.

Ipo chakacha, ambayo asilia  ni ngoma ya mama mzazi kurekebisha tumbo la uzazi, kutoa unene, halafu kuna viuno vya makalioni.  Hivi vimetangazwa sana na Wajamaika siku za karibuni hasa baada ya mtindo wa Ragga (uliochepua mwaka 1990 na Shabba Ranks) ambapo wasichana wanaonyesha matako kwa ustadi sana, mara nyingine hata kuzidi ustadi, kuwa utani. Umesambaa sana : unaitwa “booty”….
Ingawa wengine wanaweza kudai tabia imevuka mipaka lakini inadhihirisha ukweli kuwa watu wa makabila fulani (hasa weusi na walatino) hupenda zaidi makalio. Ndiyo kukua kwa neno “booty”

(more…)

Read Full Post »