Wamesema mara ya mwisho baridi kali namna hii kutokea visiwa vya Uingereza ilikuwa miaka 30 iliyopita.
Leo kila mtu nliyekutana naye jijini: mzee, mtoto, mwanaume, mwanamke, alilalama na kulaani baridi.
Hata “maglovu” nliyovaa mkononi hayasaidii. Ngumi haikunjiki sawasawa. Mti kule nyuma umepukutika matawi- zimebaki tu kuni kavu. Ndevu zangu zimenyang’arika. Upepo wa kutoboa kisindano sindano ulikuwa ukisaidia baridi kuwa nyuki zaidi.
Aliyewazidi wote kwa malalamishi alikua ajuza mmoja mzawa wa visiwa vya Karibian. Alihamia hapa miaka 55 iliyopita.
“Nlikuja kusoma na kutafuta ajira. Sipendi na siizoei baridi hata kidogo.”
Nkamuuliza kama haipendi baridi kwanini harudi tu kwao kwenye ujoto joto?
Basi linapitisha abiria waliojikunyata ndani.
Ajuza akajibu keshapazoea; lakini asichokiweza baridi.
Rudi basi kwenu.
Ajuza akacheka.
“Baridi kama hii ya leo sijapata kuona.” Nilikisia umri wake ushapita miaka 70 na kitu.
Tulikua katika foleni posta. Foleni ndefu kidogo.Foleni za Ulaya, hizo; kila mtu kimya; nje baridi kali.
“Nkishaondoka hapa nakwenda kulala,” akatangaza.
Nkawambia leo ni siku ya kunywa supu ya makanyagio na mifupa. Supu ya moto, rafiki wa baridi.
Kweli nje palikua kiama.
Kawaida hii sehemu ya kuchezea watoto katika mtaa ninaoishi -huwa imejazana vijana wakicheza kila aina ya utoto, lakini leo palikuwa patupu kama jangwa la Sahara.
Kawaida barafu inapodondoka baridi hupungua, watoto wanacheza; lakini ya leo ilikua na matone machache tu ya barafu. Imeongozana na upepo mkali – wanasema toka Siberia.
Gari la kitajiri likiharakisha mbio mbio…ukichunguza sana picha utaona matone matone ya barafu yakianza kudondoka. Labda ndo’ kisa cha hala hala hii
Polleni….”Maisha ni kama bahari yapasa kuvumilia tufani na shwari yaani heri na shari”- Sheikh Shaaban Roberts
Wee Rajabu wee…unatupa pole ya nini? Maisha haya. Iwe baridi ; iwe joto, sio mwisho wa dunia huu. Lakini kuweka nukuu ya Sheikh Shaaban Robert;umecheza kama Lionel Messi alivyocheza leo na kufunga mabao mawili dhidi ya AC Milan. Unajua jambo moja ambalo wengi hatulijui vizuri? Kisa cha nguli Shabaan Robert kuchanganya jina la Kiislamu na Kikristo ilikua kufuta uhasama kati ya Wakristo na Waislamu? Ama kweli yule Babu wetu wa Kiswahili alikua akiona mbali (runinga ya Kiswahili!).
Hello to every one, for the reason that I am truly keen of reading
this website’s post to be updated on a regular basis.
It consists of good data.