Feeds:
Posts
Comments

About: freddy macha

Website
http://www.freddymacha.com
Details
Nilizaliwa Old Moshi, Kilimanjaro; nikasoma Tela, Natiro, kisha Kaloleni na Ilboru mjini Arusha. Baada ya kidato cha sita Mzumbe, nilijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, Mafinga, Iringa baadaye nikaanza kazi ya uandishi wa habari magazeti ya Chama, Kiswahili; Uhuru na Mzalendo,1976. Nilijiuzulu Uhuru mwaka 1978... Kuanzia hapo nimekuwa mwandishi, msanii na mwanamuziki wa kujitegemea. Nimewahi kuandikia magazeti mbalimbali Bongo (Nchi Yetu, Lengo, Kiongozi, Mfanyakazi, New Outlook, Guardian, Daily Mail, nk). Kuanzia 1981 nilikuwa mwana safu na mwandishi wa makala maalum Sunday News, kila Jumapili, ("Cultural Images") hadi 1984 na baadaye nikiwa ughaibuni hadi 1992. Nimeshachapa vitabu na kushinda tuzo za kifasihi yaani mashairi ya Kiingereza (BBC Prize, 1981) na hadithi (Tuzo ya Madola, Uingereza, 1996). Vitabu vilivyochapwa ni Twenzetu Ulaya (1984), Mwanamuziki Remi (1985), Papers! Papers! Papers! (1986) na Mpe Maneno Yake (2006). Nishatoa albam mbili Kitoto (Canada, 1995) na Constipation (London, 2000). Nilisomea muziki Brazili (1988- 1994) nikasafiri na kuishi Norway, Denmark, Uswisi, Ujerumani Kanada, Paraguay, Kenya nk. Kama mwanamuziki nimekuwa na bendi kadhaa zikiwemo Sayari (Tanzania, 1980-84) , Os Galas (Brazil, 1988-1992), Berimbau Blues Band (London, leo), N4 ( London, 2011), Groove and Bossa (Brazil-London 2010) na yangu mwenyewe, Kitoto niliyoiunda 1991. Maisha yangu saa 24 ni ya kupumua, kula, kunywa, kuoga sanaa, utamaduni, fasihi, michezo, afya, usingaji, kufundisha na kujifunza ala na fani mbalimbali mashuleni, vyuoni, majumba ya sanaa, utamaduni, jumuiya, michezo, lugha na ukalimani. Kama Mtanzania najitahidi kupigania afya na uhai wa lugha na fasihi ya Kiswahili, utamaduni na hadhi yetu; kujijua na kujihami kama watu wenye uwezo mkubwa kimaisha. Mungu ibariki Tanzania! Mungu Ibariki Afrika! Mungu tuletee amani na upendo Duniani!

Posts by freddy macha:

Older Posts »

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 171 other followers