Mganga na mtaalamu wa maradhi ya moyo katika hospitali ya Guy’s and St Thomas, mjini London kakumbusha kwamba unene ni moja ya asili ya vifo duniani. Kashauri mbali na kula na mazoezi wewe mwenyewe unaweza kutazama kama u hatarini kwa kujipima kiuno.
Daktari Graham Jackson anasema chukua rula ya mshipi (inayotumiwa na washoni) iweke sentimeta moja au mbili juu au chini ya kitovu. Zungusha nyongani. Kiuoni kikizidi sentimeta 100 (inchi 39) kwa wanaume na sentimeta 85 (inchi 33) kwa wanawake basi una hatari ya kupata kisukari na magonjwa mengine ya unene mathalan: kiharusi, hinikizo nk.
mimi naumwa nyonga ya mguu wa kushoto naona inaelekea kwenye kiuno kwa maana inaelekea kwenye uti wa mgongo. je haya ni maradhi gani. miaka ya 90 nilipimwa nikaambiwa kuna mfupa unalika, je ndio sababu ya maumivu makali hayo kwani nikiinama nainama kwa tabu, pamoja na kwamba sio muda wote. naomba jibu.
Unajua kawaida mtu unaposumbuliwa na maumivu ya musuli au mifupa. Si rahisi kutoa jibu kwa mbali kupitia blogu. Tunachoweza ni tu kugusia juu juu.
1. Je una umri gani? Je wewe mnene au mwembamba? Je umewahi kupata ajali yeyote?
2. Maumivu ya musuli, mgongo au sehemu zinazohusiana na mifupa yanaweza kutokana na majeraha, uzito wa mwili (unene) , kurithi, ukosefu wa jambo fulani (kama mzunguko mbaya wa damu) nk. Ningeshauri ukamwone Mganga akuchunguze kabla ya kuulizia ulizia hivi kiholela. Ukishajua kwa hakika nini hasa kinakusumbua ndiyo tuanze kupeana ushauri. Maana kawaida waganga watasema ama utumie dawa za kuzuia maumivu, nk. Wakisema hivyo ndipo tunaweza kukupa ushauri wa hakika zaidi.
3. Kutokana na jina lako yaelekea wewe mwanamke. Maumivu ya mgongo kwa wanawake huwa yanasababishwa (mara nyingine) na sababu tofauti na wanaume. Hukusema kama umeshawahi kuzaa au bado, kama unapata matatizo wakati wa hedhi, nk. Ningekushauri uniandikie barua binafsi nikujibu kama unaona si vizuri kuandika matatizo haya hadharani (au tumia jina la bandia). Kawaida wanawake hupatwa na maumivu ya mgongo (sehemu ya chini ya uti wa mgongo) kutokana matatizo ya kizazi, hedhi nk. Hivyo ni vigumu kutoa jibu sahihi hivi.
4. Ila ninavyojua mimi kama maumivu ya mgongo nyongani upande wa kushoto yanaanzia juu ya makalio kwenda chini yanahusiana na mshipa wa fahamu uitwao “Sciatica.” Hii huwapata zaidi watu wanene wasiofanya mazoezi ya viungo. Isipotibiwa mapema inaweza kusababisha mstuko wa moyo. Maana moyo unahusiana sana na mishipa ya fahamu (ubongo, uti wa mgongo, ngozi, hisia, nk).
5. Kama unalo tatizo la “Sciatica”… Ningekuomba uchunguze kwa makini. Moja ya kinga za Sciatica ni kufanyiwa masaji au usingaji na mtu anayejua anafanya nini. Je, unaishi mji gani Tanzania? Kama ni Dar es Salaam siku hizi wapo wasingaji wengi sana, wengine wa bandia wanaobabaisha (wasiosomea sawasawa) wengine wanajua wanachofanya. Usingaji unaweza kusaidia tatizo la Sciatica. Lakini kuliondoa kabisa yabidi ujibu maswali nliouliza juu. Je wewe mnene? Je unafanya mazoezi ya viungo kama kukimbia, kuogelea, michezo yeyote na je unafanya mazoezi ya kujinyoosha yaani “stetching”? Mara 3-4 kwa juma?
Kama una pesa ni vizuri pia kwenda kwa mganga anayetumia taaluma ya Kichina iitwayo Accupuncture ambayo ni nzuri sana kutibu maumivu ya mifupa, musuli, nk. Hebu Google neno hilo Accupuncture kama hulifahamu.
6. Soma zaidi kuhusu Sciatica hapa:
http://www.medicinenet.com/sciatica/article.htm
Dada Mwanaidi hiyo ni shida ndogo tu tatizo ni ule mshipa wa siatica nerve umeletashida waweza ni tafuta kamauko dar shida inaisha
Kufafanua anachosema bwana Adam juu…mshipa wa “Sciatica nerve” huanzia sehemu ya chini ya mgongo, nyuma ya mafigo (au juu ya makalio) hadi miguuni. Mshipa huu si tatizo bali “dalili” au ishara ya tatizo la mgongoni au nyongani.
Adam nawezaje kukupata?
Bpepe yake iko mwisho wa mahojiano ukiangalia
MIMI NI MWANAMKE, NI MNENE KIASI HIZO CM NAZIPITA NIKO KWENYE 44, MARADHI YANGU YALIVYOANZA YALIANZA KAMA SEHEMU NILIYOCHOMWA SINDANO KWENYE TAKO KUSHOTO NDIO IMEENDA MPAKA LEO HII NAUMWA SANA,
Rehema
Mimi nimeshazaa katikati ya mgongo nasikia maumivu nilienda hospitali nikaambiwa henia nikapewa dawa lakini bado nasikia maumivu ,mimi sio mnene niko wastani
pole dada Amina hiyo sio henia nitatizo tu la mgongo yapo matatizo mengi ya mgongo
naitwa tamim umri wa miaka 21 ni mwana mivhezo haswaa mpira wa miguu nina kilo 76, kama unavyojua kazi hyo ina purukushani sasa nikaangushwa nikaishi kuangukia makalio mpaka leo naskia nyonga upande wa mguu wa kulia inanisumbua nashindwa kuendelea na mchezo kama zaman tatizo lina wiki takriban 2 na nusu je nifanyaje?
Tatizo kama hilo, ungekwenda hospitali ukapigwa picha ya “X – Ray ” bwana Mambo. Je mnapocheza hamuwi na waganga au watu wa huduma ya kwanza? Inaweza kuwa umeteguka au kuumiza mifupa au viungo vinavyounganisha nyonga na uti wa mgongo au mfupa wa kukalia uitwao Sacrum na Coccyx. Bora sana ukachunguzwe na daktari.
Kama ulishawahi kwenda kwa mganga ukapimwa na bado yuna matatizo, hebu jisomeee hiki kiungo chini. Kinaelezea kiasi fulani tatizo la makalio na aina ya mazoezi ya kufanya.
http://www.livestrong.com/article/376631-exercises-for-sacral-pain/
Habari, naomba mnisaidie dawa au tiba ya kuondoa kabisa matatizo ya nyonga ni mwaka sasa yanasumbua.. ahsante, hospitali napewa dawa tuu lakini inakaa mda kidogo inarudi tena..
Whitney …nyonga inakuuma…je unafanya kazi gani? Je unafanya mazoezi yeyote? Je umewahi kupimwa na mganga? Akasemaje?
Ni vigumu sana kumwambia mtu afanye nini bila kujua shughuli zake? Elezea kwa undani zaidi
Niandikie Bpepe ukiweza
kitoto2004@yahoo.co.uk