Mjadala aliopopoa Maggid ” Mwenyekiti” Mjengwa (pichani, kulia, alipohudhuria semina zangu, Dar, Mei) blogu ya Kwanza Jamii umezua maoni kem kem. Ni mjadala muhimu kwa sababu kadhaa:
1-Zamani Mwalimu Nyerere alisisitiza sana juu ya utaifa ndiyo maana akashauri sote tuongee Kiswahili. Hii imechangia sana kutokuwa na kero za ukabila Tanzania kama zilivyo nchi nyingi bara Afrika. Hatujawa na vita vikubwa vya wenyewe (ukiacha kumtoa Amin, 1979) tangia 1907.
2-Kizazi kipya cha Watanzania kilichopumua hewa baada ya Mwalimu (Ujamaa) kimeanza “kukua na utata” wa kutojijua wewe nani (identity) hili linaonekana mathalan katika masuala ya lugha. Lugha ni kitanda kikuu cha mawasiliano na utamaduni. Wachache sana leo wanaweza kuandika au kuongea Kiswahili fasaha au Kiingereza fasaha bila kuchanganya maneno. Tatizo hili limeenea Afrika nzima. Wazaire, kwa mfano wakiimba au kuongea utakuta sentensi zimechanganya Kilingala na Kifaransa. Wakenya hivyo hivyo. Afrika Kusini hivyo hivyo.
3-Hata wale wanaondika Kiswahili utakuta wanachanganya herufi L na R ama DH na Z .
Mathalan : “luka” badala ya “ruka”; “luninga” kinyume cha “runinga”; “azabu” badala ya “adhabu” nk. Hili ni tatizo kubwa sana na linaonekana wazi wazi ndani ya mablogu, vyombo vya habari, simu za mkono (SmS) , nk.
4-Mfano bab kubwa wa karibuni ni malumbano na mgogoro kuhusu mwigizaji Steven Kanumba, alipokuwa katika Big Brother Afrika, anadaiwa na baadhi eti hakuongea Kiingereza fasaha (ingawa suala ni la lafudhi na nahau kuliko sarufi) na alikosea alipotoa zawadi ya shati rangi ya waridi – pink- (ambayo ni rangi ya Wasenge ughaibuni) badala ya kutoa kitu cha jadi kama vinyago, kanga, miziki ya Watanzania nk.
Mambo kama haya ya utoaji zawadi kutoka kwenu….(mila na desturi) hutokana na kujijua yaani “identity” anayoongelea Mwenyekiti Maggid.
Hebu angalia maoni chini:
http://mjengwa.blogspot.com/2009/09/watanzania-hatuna-kwetu.html#comments
Read Full Post »