Juma hili habari kwamba kitabu kipya cha mwandishi nguli, Adam Shafi (Kasr ya Mwinyi Fuad,Kuli, Vuta Nkuvute na Haini) kimetoka ni za kushangilia sana. “Mbali na Nyumbani” inaangalia maisha yake msanii huyu Ughaibuni takribani miaka 50 iliyopita…Kimetolewa na Longhorn Publishers wenye makao yao Nairobi Kenya na matawi mbalimbali Dar es Salaam, Kampala na Rwanda.
Mara ya mwisho nilipomhoji Mzee Shafi, Desemba 2007 alikuwa bado anakiandika kitabu hicho ambacho alisema kitaelezea maisha yake ya ujanani.
Shafi akiwa na mjukuu wake Lowell, mjini Milton Keynes, Uingereza. Picha na F Macha
Katika uchambuzi wa kitabu hicho, mwandishi hodari wa Kenya, Profesa Ken Walibora, anasema mtindo wake wa kuangalia tawasifu- ambapo mwandishi au mhusika anaelezea maisha yake haujaenea sana katika maandishi ya Kiswahili seuze ya Kiafrika. HIvyo anasema Walibora, ni jambo zuri la sisi wengine pia kulifanya.
Mbali na kutukuza kitabu hiki, Profesa Walibora anachangamkia namna maandishi na lugha ya Kiswahili inavyoendelea kukua duniani. Hivyo kututaka Waswahili kuendelea kuandika na kujenga na kuimarisha KISWAHILI.
Mwanafasihi Shafi akinionyesha muswaada wa kitabu hicho -wakati kikiwa bado jikoni miaka mitano iliyopita.
Ni jambo la kuchangamkia kwamba kimemalizika. Picha na F Macha.
Kuli, kilichotolewa mwaka 1979 (TPH) na 2005 na Longhorn, ni moja ya vitabu maarufu vya mwandishi ambavyo vimempatia sifa ya kuiangalia jamii yake kwa macho ya darubini kali ya kimaendeleo.
Kasr ya Mwinyi Fuad, toleo lake la kwanza kabisa, lilitolewa pia na TPH mwaka 1978. Kitabu hiki kimeshatafsiriwa katika Kifaransa, jambo linaloonyesha namna mwandishi huyu anavyosifika duniani.
SOMA TAHAKIKI YA PROFESA KEN WALIBORA (aliyehariri na kuchangia kitabu kizuri sana cha Kiswahili, pamoja na Profesa Said Ahmed Mohammed, DAMU NYEUSI, kilichotolewa na MacMillan Kenya, 2007!)
http://www.swahilihub.com/habari/MAKALA/-/1310220/1672466/-/ouhmen/-/index.html
naomba kupata namba za simu za shafi Adam shafi Adam tafashalini sana sana kama mwandishi huyu yupo hai kwa maana nashida nae sana sana tafadhalini jamani
Ntakujibu katika barua pepe
Kwa kweli Freddy Macha mchango wa Adam Shafi ni mkubwa sana kwa tanzu za riwaya na sasa tawasifu katika fasihi ya Kiswahili. Niliyasoma mapitio ya bingwa wa fasihi Prof. Ken Walibora na kuvutia sana na uhakiki wake unaothibitisha ubobevu wake katika ubunifu na uhakiki. Heko kaka kwa kurejelea mapitio hayo ya Prof. Walibora ya aina yake ambayo yameangazia tawasifu ya Shafi ya aina yake. Shukran sana.
Shukrani kama maelezo yako. Je, wajua kwamba Prof. Ken Walibora pia kaandika riwaya ya Siku Njema ambayo labda ndiyo riwaya bora na maarufu zaidi ndani na nje ya Kenya? Pia kaandika riwaya zifuatazo: Ndoto ya Almasi, Kufa Kuzikana, na Kidagaa Kimemwozea. Akishirikiana na Said A. Mohamed, amehariri mikusanyiko wa hadithi fupi kando na Damu Nyeusi, kama vile Kiti cha Moyoni.
Nashukuru kwa maelezo Fatma Juma. Hiyo “Damu Nyeusi” nishaisoma na kuipitia. Sema hivyo vingine ningependa kuvipata. Je, wawezaje kunisaidia- ili niwafahamishe wasomaji wengine wapenzi wa fasihi ya Kiswahili?
NImekuandikia anuani yako pepe imenirudia. Tafadhali nijibu suala langu katika kitoto2004@yahoo.co.uk
Au kilimanjaro1967@hotmail.com
kongole mpenzi wa kiswahili.nakuomba unitumie makala ya kitabu chako kipya MBALI NA NYUMBANI kwa anwani yangu,ambayo ni solomonmaswa@yahoo.com ili nijifundishe mengi zaidi.Asante.
Ahsante. Ila hawezi kukutumia kitabu kwa barua pepe. Hebu mpigie mwenyewe mwandishi simu akuelezekinapouzwa Dar es Salaam au Nairobi au Kampala.
Simu yake ni : 0713-266-560
Reblogged this on | Fasihi | Literature in Africa | and commented:
Katika uchambuzi wa kitabu hicho, mwandishi hodari wa Kenya, Profesa Ken Walibora, anasema mtindo wake wa kuangalia tawasifu- ambapo mwandishi au mhusika anaelezea maisha yake haujaenea sana katika maandishi ya Kiswahili seuze ya Kiafrika. HIvyo anasema Walibora, ni jambo zuri la sisi wengine pia kulifanya.
Kweli kabisa
Habari za majukumu mimi nlikua nataka kujua neno winked kwa maana halisi ya neno hilo.
Winked imetokana na “wink” yaani kukonyeza. Kisarufi ukiweka “ed” ina maana ya kupita. Ilikonyezwa, alikonyezwa au alikonyeza.
kongole kwa kazi nzuri naomba nakala cha hicho kitabu …………………….kogeinorman@gmail.com
Kinauzwa Dar es Salaam. Nenda Soma Cafe kaulizie