Feeds:
Posts
Comments

Posts Tagged ‘Swahili Writers’

Abdilatif Abdallah and Sauti ya Dhiki, London 2013-pic by F Macha
Angali kijana wa miaka 19, Abdilatif Abdalla alishiriki “harakati za kisirisiri” kupinga uongozi wa Rais Jomo Kenyatta, Kenya. Uongozi huo anaeleza leo, ulimnyima uhuru raia wa kawaida nchini humo (baada ya miaka mitatu tu ya utawala) uliopatikana Desemba 1963. Abdilatif alikuwa mwanachama wa chama cha upinzani, Kenya Peoples Union (KPU) kilichoongozwa na Jaramogi Oginga Odinga. Mchango wake mkuu ulikuwa kuandika. Alipofikisha makala ya saba iliyouliza “Kenya Twendapi?” alifungwa.
(more…)

Read Full Post »

Riwaya zako tatu zimepishana miaka 36. Je kwanini, muda mrefu toka Utengano hadi Nyuso? Asali Chungu (1977), Utengano(1980) na Nyuso za Mwanamke (2010), Mhanga Nafsi Yangu (2012).
Vile vile dhamira kuu inamwangalia mwanamke kwa macho na hisia za kumtetea. Mwandishi mwingine Mwafrika anayesimama upande wa kina mama (hasa vitabu vyake vya mwanzo) ni Msomali – Nuruddin Farah. Je, kwanini wanaume muwatetee wanawake? Kwani hawawezi kuandika wenyewe?

Nyuso za Mwanamke
Mwandishi Said Ahmed Mohammmed
Kuandika riwaya au kazi yoyote ya fasihi kunahitaji wakati, utulivu na wiitisho wa ndani wa nafsi ya mwandishi. Huwezi tu kujilazimisha kufululiza. Kisha nadhani vita vya wanawake ni vita vya wanaume pia kama ilivyo kwamba vita vya wanaume ni vita vya wanawake. Kwa hali hii hakuna suala la kwa nini? Kwa bahati mbaya waandishi wanaume wachache tu ndio wenye msimamo wa ukombozi wa wanawake katika fasihi ya Kiswahili. Ama suala la wanawake kutoandika wenyewe wapo wachache katika fasihi ya Kiswahili wanaoandika hata kwamba hawajitetei. Jambo hili linashikamana na historia ya wanawake katika jamii zetu. Wanawake popote pale wamekuwa katika historia ya ukandamizwaji, je kwa nini tusiwatetee?.
(more…)

Read Full Post »

adam-shafi.jpg

Nimepokea simu. Simu ya maana. Adam Shafi yuko Majuu. Kaja kikazi Uholanzi. Yeye mtaalamu wa lugha ya Kiswahili. Baada ya kumaliza kapitia Uingereza katika mji mmoja wenye wakazi wengi wa Kitanzania, yaani Milton Keynes. Ni wastani wa saa moja kwa treni toka London.  Mrefu, mchangamfu, mzungumzaji aliyesheheni “mastore” kibao. Nishakutana na waandishi wa kila sampuli. Wanaojificha: wakimya, wasioongea sana, wapole wanaokaa chumbani kati kati ya watu ukadhani hawapo. Wanaopiga kelele, wakijafaragua; ama wenye aibu…
Shafi ni mtu wa kawaida kabisa, naweza kuiita hulka, tabia na namna yake “Mfurahia Maisha” : kachangamkia  uhai, haswa. Kaishi, anaishi…hamalizi. Kila mara atasema ana mikakati ya kufanya jambo fulani, kuandika kitabu kingine kipya, kuendeleza fasihi na Kiswahili….
(more…)

Read Full Post »